Madiwani watwangana makonde Moshi:Kisa? Ulaji kwenye Kamati. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani watwangana makonde Moshi:Kisa? Ulaji kwenye Kamati.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MpigaFilimbi, Aug 3, 2009.

 1. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Daniel Mjema, Moshi

  MADIWANI watatu wa Baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, wametoa kali ya mwaka baada ya kuchapana makonde wakigombea kuingia kwenye kamati ya mipango miji ya halmashauri hiyo.

  Haijafahamika mara moja kamati hiyo ina maslahi gani manono ukilinganisha na kamati nyingine, lakini kamati hiyo ndiyo inasimamia suala la ugawaji viwanja, suala ambalo ni nyeti kwa mkoa Kilimanjaro kutokana na uhaba wa ardhi.

  Habari za uhakika zilizopatikana jana zilidokeza kuwa kiini cha kasheshe hilo kilitokana na mmoja wa madiwani wa jinsia ya kiume kutaka diwani mwingine mwenye jinsia ya kike ndiye aingie katika kamati hiyo badala ya diwani mwanaume aliyekuwa akitaka.

  Chanzo cha habari cha kuaminika kilisema kutokana na mvutano huo, diwani mmoja alinyanyuka na kudai diwani mwenzake alikuwa akimfuatafuata na kuamua kumzaba kibao diwani mwenzake.

  Habari hizo zilisema kuwa baada ya kuzabwa kibao, diwani huyo alitaharuki na kuamua kujibu mapigo ambapo walianza kutangwana ngumi na mateke, ugomvi ambao ulimkumbwa diwani wa kike ambaye naye alizabwa vibao.

  Inaelezwa kuwa madiwani hao wamekuwa wakiingia katika kamati hizo kwa kupokezana lakini mmoja kati ya madiwani hao alikuwa akishinikiza yeye ndiyo apewa fursa hiyo badala ya Diwani wa viti maalumu.

  Makamu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Alhaji Omar Shamba alithibitisha kupokea taarifa za vurugu hizo lakini akasema hawezi kuzizungumzia kwa kuwa zilitokea nje ya vikao vya Baraza la Madiwani.

  “Ni kweli nimezipata hizo habari lakini siwezi kuzizungumzia kwa sababu na mimi nimezipata kama wewe ulivyozipata…tunasubiri kama zitaletwa kama malalamiko zitafanyiwa kazi na kamati ya maadili”alisema Shamba.

  Hata hivyo Alhaji Shamba ambaye pia ni Diwani wa kata ya Njoro kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM) alisema tukio hilo limewadhalilisha madiwani hao ambao kimsingi walipaswa kuwa kioo cha jamii na kuonyesha mfano.

  Manispaa ya Moshi inaongozwa na madiwani wa CCM ambao ndio wengi lakini wapo pia madiwani watano kutoka chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA). Madiwani waliotangwana wanatoka moja ya vyama hivyo.


  Source: Mwananchi


  Kamati hizo zinasababisha watu wazipige, unadhani nini wanakimbilia huko? Fedha za rushwa au posho? Kila mtu alipo anataka kula tu??
   
 2. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,790
  Likes Received: 2,451
  Trophy Points: 280
  kweli kuwa uyaone ebu angali hiki kioja cha hawa ndugu tuliowachaguwa wenyewe!

  Madiwani watatu baraza la madiwani la halmashauri ya manisapaa moshi wametoa kali ya mwaka baada ya kuchapana makonde wakigombea kuingia kwenye kamati ya mipango miji ya halmashauri hiyo.

  haijajulikana kuwa kamati hiyo ina maslahi gani ukilinganishwa na kamati nyingine.Lakini kikubwa ni kwamba kamati hii ndo inayoratibu na kushughulikia mausala yote ya ugawaji wa viwanja suala ambalo ni nyeti kwa mkoa wa kilimanjaro.

  Angalizo.

  Hivi ni kweli mababa mazima wanaweza fika sehemu yakupigana kisa kwenda kupeana viwanja au ndo masuala ya rushwa yap huko.

  Kwa kweli natamani kutopiga kura mpaka naingia kaburini.
   
 3. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  Duh! Haya bwana.
   
 4. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kyachakiche vipi tena huko Moshi??
   
 5. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Aisee wangechapana makonde kugombania maendeleo ingekuwa murua, mipango miji hii itakuwa na ulaji hasa kwa sababu mji wa moshi umeanza tena kukua kwa kasi
   
 6. M

  MC JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45

  Kwa mtazamo huo, ni bora yao hao waliopigana kuliko wewe, kwa kuwa huelewi kuwa kupiga kwako kura ndio kunaweza tu ondoa mambo kama hayo.
   
 7. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2009
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Chaku
  Tunakuomba utusaidie kuyajua majina ya hao waliochapana makonde. Pengine kuna tunaowajua ili wajadiliwe wao kama wao na wala si madiwani wote wa Moshi kwa ujumla wao.
   
 8. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2009
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tunaomba majina yao tafadhali
   
 9. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Kama ni kweli ni aibu sana, uchu wa pesa kwa kutaka kuifanya hiyo kazi. Wakina nani kwa majina?huh!
   
 10. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2009
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Taarifa nilizo nazo ni kuwa madiwani hao hawakupigana. Bali walitishiana na baadhi yao wawili walikwenda kituoni kuomba PF3 kwa ajili tu ya kujihami na pengine kuestablish kesi ya fidia.

  Hapakuwepo dalili zozote za kugombania maslahi katika kamati husika.

  Wanaojua siasa za Moshi wanajua jinsi ambavyo CCM wanainvest katika mIgogoro ndani ya CHADEMA.
   
 11. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Mchaga na Pesa Aisee!!!!! We acha tu Ati!!!!
   
 12. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #12
  Aug 4, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mi nlijua wamemtwangana kwa kulaumiana ulaji hela kumbe wanatafuta ulaji? duh nasema hawa wanaombaga kura kwa ajili ya kula basi na si vinginevyo, sijui tuanyeje nduguz JF!
   
 13. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #13
  Aug 4, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,790
  Likes Received: 2,451
  Trophy Points: 280
  jamani PF3 polisi siyo ugomvi huo?unachukuwa ili eweje?
   
Loading...