Madiwani watatu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Iringa wamejiuzulu

Mgogoro upo mkubwa sana kat ya msigwa na madiwan....mpango ulikuwepo wa kumwondoa msigwa kwenye kura za maoni 2015 ila dili likabuma...!! Kwa vyovyote vile msigwa anakabiliana na wakat mgumu kuliko maelezo at the same tym...mkuu wa wilaya ya iringa anakuja juu sana na kundi kubwa linamkubali hata baadh ya makada wa chadema hapo irunga wanamkubali...jamaa naye ana mpango wa kugombea 2020...safar hii msigwa itabd aongeze waganga
Mijitu mingine sijui inatumia kiungo gani kufikiri na kuchanganua mambo! Unamsifu mkuu wa wilaya kuwaondolea utangamano wenu badala ya kumuonya aache kuuvuruga umoja wenu ahangaikie viwanda mpate pesa za kunywea bia badala ya ulanzi wenu na komoni. Mtaishia kuwashangilia hao wateule na vijisenti vyao wanavyowahonga ili mvurugike. Tafakarini na mkatalieni hiyo mipango yake na badala yake awajengee kiwanda na sio kuwaachia waarabu wa ASAS na takor kuwatumikisha kwa ujira mdogo. Lieni badala ya kuuchekelea umaskini unaowaadabisha hapo.
 
Madiwani hao ambao ni:-

LEAH MLELEU.

BARAKA KIMATA na HUSNA DAUDI
 
Hii imetokea leo manispaa ya Iringa ambapo madiwani watatu wa chadema wamebwaga manyanga kwa maelezo kuwa ndani ya chama hicho kuna ubabaishaji mwingi, Rushwa na ufisadi, umangimeza na ubabe usio na maana. Zaidi fungua hii link hapa chini.
MWANGAZA WA HABARI: MADIWANI WATATU WA CHADEMA MANISPAA YA IRINGA WAJIVUA UWANACHA NA UDIWANI
Wale wa arumeru walipeni hela zao,ccm mambo ya kikekike mnapenda sana eti mtu anajiuzulu kisa kumuunga fenti fodi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siwashangai kabisaaaaaa kwa hayo yaliyowasababisha kuamua hivyo.

Sielewi mtu unawezaje kukaa kwenye chama kama hamna kile ulichotaka kuona kinakuwa. Ni habari nzuri sana wamejitambua, kuliko kukaa kwenye chama kinachoshikilia yale walilalamika na kuyaponda kuwa hawataki kuyaona awamu zilizopita.

Tuwashangilie jamani na kufurahia kwamba JPM lori lake linawezesha watu kuliona na kuamua kulishangilia kabisaaaa.

Magufuli oyeeee
 
Mijitu mingine sijui inatumia kiungo gani kufikiri na kuchanganua mambo! Unamsifu mkuu wa wilaya kuwaondolea utangamano wenu badala ya kumuonya aache kuuvuruga umoja wenu ahangaikie viwanda mpate pesa za kunywea bia badala ya ulanzi wenu na komoni. Mtaishia kuwashangilia hao wateule na vijisenti vyao wanavyowahonga ili mvurugike. Tafakarini na mkatalieni hiyo mipango yake na badala yake awajengee kiwanda na sio kuwaachia waarabu wa ASAS na takor kuwatumikisha kwa ujira mdogo. Lieni badala ya kuuchekelea umaskini unaowaadabisha hapo.

Mbna una temper sana....unacomment kama unakimbizwa...mimi nimezungumzia hali ya kisiasa iliyopo pale iringa kwa sasa...nani kahongwa, nani kahonga, nani anatakiwa afanye nin is non of my bussines... Usikurupuke tu ili upate like we vip
 
Huyo Diwani wa Kitwiru (mwanaume) kachukuliwa tu kuwapa kampani hao madiwani akina mama (viti maalum) ambao wanahongwa kirahisi.
 
Hii ni michezo ya watu , ukikubali kununuliwa kwa ahadi ya kupewa fedha au cheo ni Usaliti mkubwa sana kwa waliokuchagua
 
Madiwani watatu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Iringa wamejiuzulu nafasi zao na kukihama chama hicho kwa kile wanachodai kuwa viongozi wao ngazi wametawaliwa na rushwa na ubaguzi dhidi ya baadhi ya madiwani.

Akiongea kwa niaba ya wenzake Baraka Kimata diwani wa Kitwiru amesema ameamua kufanya maamuzi hayo magumu ili hali anatambua kuwa wapo watu watachukizwa na maamuzi hayo lakini hana jinsi kwa kuwa amevumilia mambo mengi ndani ya chama hicho.

"Najua wapo watu wataumia kutokana na maamuzi haya lakini sina jinsi imebidi nifanye maamuzi magumu kwani kuna wakati watu mnafanya vikao hafikii maamuzi kutokana na mabishano mpaka muda mwingine mnatishiana maisha sasa tunaendelea kutafakari hichi chama ambacho kimewaaminisha Watanzania kuwa chama mbadala kikachukua dola kitawaletea Watanzania nini" alihoji Baraka

Diwani huyo aliendelea kufafanua mambo mengine mengi mtazame hapo chini

Chanzo: EATV

Udiwani ni dili ckuhiz acha na mm nisubir 2020

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama unataka kutengeneza pesa awamu Hii kupitia udiwani ni kupoteza muda! Tenda Za Halmashauri hamna, vikao vingi no posho mbaya zaidi uwe upinzani, presha tupu!

Hivyo wasitafute visingizio. Hawajanunuliwa wala kurubuniwa, jibu rahisi ni HAKUNA MADILI....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ipo namna nyingine kufikiria zaidi ya kusema rushwa Rushwa. CHADEMA wasipojichungiza imekula kwao,wapo wanachama wengi sana ambao hawana vyeo ndani ya chama na hwana uwezo wa kuitwa Press conference wanahama kimya kimya bila nyinyi kujua na mmebakia kuwarukia watu wachache sana(madiwani) kati ya wengi wanaokihama chama na kwenda CCm..Acheni kujipa moyo.
 
Hela za Bwana Slow hazitowaacha Madiwani Walafi walioko CDM salama.......!!!!

Aiseee! Anataka arejeshe mgao aliotembeza wakati wa kampeini kwa shortcut..! Kweli hali tete!

Back
Top Bottom