Madiwani watatu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Iringa wamejiuzulu

wamechagua kule kwenye viongozi wapumbavu... kuacha udiwani ili uwe mwanachama wa kawaida ni zaidi ya upumbavu....
 
Madiwani watatu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Iringa wamejiuzulu nafasi zao na kukihama chama hicho kwa kile wanachodai kuwa viongozi wao ngazi wametawaliwa na rushwa na ubaguzi dhidi ya baadhi ya madiwani.

Akiongea kwa niaba ya wenzake Baraka Kimata diwani wa Kitwiru amesema ameamua kufanya maamuzi hayo magumu ili hali anatambua kuwa wapo watu watachukizwa na maamuzi hayo lakini hana jinsi kwa kuwa amevumilia mambo mengi ndani ya chama hicho.

"Najua wapo watu wataumia kutokana na maamuzi haya lakini sina jinsi imebidi nifanye maamuzi magumu kwani kuna wakati watu mnafanya vikao hafikii maamuzi kutokana na mabishano mpaka muda mwingine mnatishiana maisha sasa tunaendelea kutafakari hichi chama ambacho kimewaaminisha Watanzania kuwa chama mbadala kikachukua dola kitawaletea Watanzania nini" alihoji Baraka

Diwani huyo aliendelea kufafanua mambo mengine mengi mtazame hapo chini



Chanzo: EATV

Waende zao wakalambe matapishi yao huko fisiemu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti wana sema ni CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO... Hakuna DEMOKRASIA yoyote ndani ya CDM na hawa wanaokaza ubongo mtaani kubisha na kujenga hoja juu ya CDM kwanza hata kadi tu hawana wala si wanachama....Kijana ingia ndani ya CDM Afu jaribu kuutambua ukweli na huo ukweli utakuweka huru....

Ai kotoni ende mai kondisheni...
 
Kuna diwani mmoja wa ccm huku Lake Zone ambaye pia alishawahi kuwa mwenyekiti wa halmashauri aliwaambia wapambe wake kuwa hatagombea tena udiwani maana madili hayapo yamebaki ngazi za juu tu hivyo kwake ameingia hasara sasa madiwani walioko chadema hata ukiwahonga milioni 5 tu wanauza udiwani.
Na ikumbukwe ukiwa diwani wa chadema ni full kufanya kazi ya kujitolea maana ukifanya ufisadi tu unaishia jela kwakuwa unakuwa huna kinga ya ccm.
Maisha ya upinzani ni magumu sana vikwazo vya kimaisha ni vingi mno mtu anaona kulaza familia njaa ni bora tu asalimu amri kwa ccm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashangaamzwa sana na akili za watanzania wanaokubaliana na huu Upuuzi.

Hivi hawa watu wazima na sharubu zao, waliwaza nini kua wagombea WA chama cha upinzani na leo bila hata soni, wanadai kuachana na nafasi zao?

Mi bado naamini wamenunuliwa iwe kwa ahadi ama pesa kamili.
Na nijuavyo mwisho WA muovu hubaki huovu.

Time will tell.
Usaliti ni dhambi yenye laana kuu.
Ni mara 100 wasingegombea.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mgogoro upo mkubwa sana kat ya msigwa na madiwan....mpango ulikuwepo wa kumwondoa msigwa kwenye kura za maoni 2015 ila dili likabuma...!! Kwa vyovyote vile msigwa anakabiliana na wakat mgumu kuliko maelezo at the same tym...mkuu wa wilaya ya iringa anakuja juu sana na kundi kubwa linamkubali hata baadh ya makada wa chadema hapo irunga wanamkubali...jamaa naye ana mpango wa kugombea 2020...safar hii msigwa itabd aongeze waganga
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom