Madiwani watatu CHADEMA wasimamishwa vikao 3 baada ya kuihoji Serikali

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Madiwani watatu wa CHADEMA halmashauri ya Mji wa Njombe wametolewa nje ya kikao cha baraza la madiwani na kusimamishwa kuhudhuria vikao 3 kutokana na kujadili mkataba wa halmashauri na kampuni iliyowekwa kukusanya ushuru ambayo inawanyanyasa wananchi

Madiwani hao ni pamoja na George Sanga diwani Kata Ramadhani, Sigrada Mligo, diwani viti maalum, Legnard Danda, diwani kata Ihungilo ambao walitolewa kwenye mkutano na kusimamishwa kuhudhuria vikao vitatu baada ya kuhoji mkataba wa halmashauri na kampuni ya Ihagara inayo kusanya ushuru mjini Njombe ambayo inadaiwa kuwanyanyasa wananchi.

Awali Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Njombe, Edwin Mwanzinga alipiga marufuku kujadili suala hilo kwa madai kuwa baraza halina mkataba huo na hakuna palipo andikwa jina la kampuni hiyo.

"Ihagala kama nani? Tumewaambia sisi hatujamwajiri na baraza hili halijamwajiri huyo Ihagala hivyo sisi tunamjadili kama nani? Nimewaambia hayo mapendekezo yote wayapeleke kwa Mkurugenzi yeye ndiye mwajiri wa Ihagala" alisema Mwanzinga.

Chanzo: EATV
 
Moja, huyu Mwenyekiti sijui kama anajua wajibu wa baraza la madiwani!, pili, elimu yake plz huenda tatizo linaanzia hapo.
 
Habari hii haiko balanced, ahojiwe na mwenyekiti sababu zilizopelekea kuwatoa nje ndo ije tuchambue nani mkosefu, bila hivyo ni siasa taka
 
mleta uzi hufai kuwa mwandishi wa habari. Na endapo ungekuwa mwandishi wa habari basi kila siku ungekuwa unapigwa au kufunguliwa kesi... Hii kutuletea taharifa za upande mmoja haileti maana maana huna ukweli wowote wa upande wa pili sababu zilizo mfanya mwenyekiti kuwatimua hao wendawazimu
 
Baba yao ndyo anataka hvyo huon hata bunge limekuwa bubu na kibogoyo.hapo anayotakiwa kuibua ni ufisad n mku wa wilaya ilionekane serikali inafanya kazi.juz waziri jafo kasema rc dc na ded watunze siri za serikali,siri zenyewe ndyo hzo
 
Hii sio habari!!! Lakin tukiiita umbeya INA fit kabisa EATV munazingua pamoja na ww mleta mada
 
Back
Top Bottom