Madiwani wamzomea mwenyekiti CCM MKOA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani wamzomea mwenyekiti CCM MKOA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 16, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2]MONDAY, JULY 16, 2012[/h]


  Na John Maduhu, Mwanza


  MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Clement Mabina, mwishoni mwa wiki alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.


  Dhahama hiyo ilitokea wakati wa kikao cha ndani baina ya Mabina na madiwani hao, ambapo hatua hiyo ilisababisha kuvunjika kwa kikao cha Baraza la Madiwani.


  Hatua hiyo ilikuja baada ya Mabina kudaiwa kuwatuhumu baadhi ya madiwani hao, kwamba wamehongwa fedha ili kumlinda Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Benard Polly.


  Mabina alitoa matamshi hayo katika ukumbi wa CCM wa wilaya na kuwachefua madiwani hao. Katika kikao hicho Mabina aliongozana na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mariamu Rugaila.


  Wajumbe wengine waliokuwapo katika msafara huo ni pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Joyce Magunga na wajumbe wawili wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa.


  Katika mkutano huo mwenyekiti huyo aliwatuhumu madiwani hao kuwa, wameshindwa kumwajibisha mwenyekiti wa halmashauri hiyo kutokana na wao kuhongwa Sh milioni saba.


  Kufuatia kauli hiyo madiwani hao walimtaka Mabina kuthibitisha kauli yake na kutoa ushahidi kwa kuwa tuhuma alizozitoa dhidi yao ni nzito na hazikupaswa kutolewa katika kikao hicho.


  "Mheshimiwa mwenyekiti tuhuma hizo ni nzito dhidi yetu, tuhongwe fedha kwa ajili ya nini hasa? wewe mwenyewe mbona umekuwa ukituhumiwa kwa rushwa tena katika vikao na hujachukua hatua, tunaomba utuombe radhi vinginevyo tutakuchukulia hatua", alisema diwani mmoja, huku wengine wakizomea.


  "Hakika baada ya kauli hiyo ya Mwenyekiti dhidi ya madiwani hali ya hewa ilichafuka na kila diwani alitoa kauli nzito dhidi ya Mabina.


  “Madiwani walimzomea kwani alitudhalilisha suala la mwenyekiti wetu kwa mujibu wa msimamo wa baraza la madiwani ni kuviachia vyombo vya dola vifanye kazi bila kuingiliwa na kama ana kosa basi afikishwe mahakamani sio kutumia ngao ya CCM kumwadhibu kutokana na chuki binafsi", alisema diwani mwingine.


  Kutokana na zomea zomea hizo Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mariamu Rugaila aliomba kikao hicho kifungwe, ili kuepusha kutokea kwa vurugu zaidi hali ambayo inaweza kuhatarisha hali ya usalama.

  Chanzo: Mtanzania   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  safi sana..
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  2015 Mi naona ni mbali sana!
   
 4. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Madiwani nomaaa siku hizi, daaaaah!!!!
   
 5. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,378
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Iko poa sana....
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ccm mwanza sasa basi
   
 7. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Hiyo ni mwanzo wa sinema tu mamabo mengi yataibuka kama kusajili meli za iran zanzibar, sumajkt kufanya ufisadi, tanesco kutimuana, nape kuhodhi madaraka, kova kufanya kazi za TISS waziri wa fedha kusoma bajeti ya mkulo mbovu, bunge kuwa serikali, haya yoye ni CCM mbovu kutaka itawale daima.tusubiri operation sangara snigida kama kama serikali itaweza kuwafunga wanachama wote wa magwanda?!
   
 8. piper

  piper JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hata ukishona kiraka kwa namna yoyote nguo bado itachanika, kiama cha magamba sasa ni zamu ya fungulia dog kila mtu anabweka kivyake
   
 9. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Safi sana... Hawa madiwani si nilisikia wanataka kuvua magamba na kuvaa gwanda, karibuni sana cdm... Nape 'oil chafu' hiyooo inamwagika...
   
Loading...