Madiwani wamtaka Mkurugenzi kuchunguza wizi wa dawa Mafinga

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,364
8,096
1667908184066.png

Madiwani wa Halmshauri ya Mji Mafinga wilayani hapa, wamemwomba Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuunda kamati ya kwa ajili ya uchunguzi wa tuhuma wizi wa dawa katika kituo cha afya Ihongole unaolalamikiwa na wananchi.

Hayo yamebainishwa na Diwani wa viti maalum Dainess Msola katika kikao cha Baraza la Madiwani kipindi cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2022/23 kilichofanyika leo Novemba 8 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo. Diwani Msola amesema kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya tuhuma za wizi wa dawa katika hospitali hiyo hivyo inatakiwa kuundwa kwa Kamati hiyo ili kuweza kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo.

"Tumwombe Mkurugenzi kukubaliana jambo hili ili kujuwa ni mtumishi gani anayekabiliwa na tuhuma za wizi huo wa dawa kama anataka uthibitisho ataupata baadae," amesema Msola.

Akijibu tuhuma hizo Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, Dk Bonaventura Chitopela amesema amelipokea suala hilo na atalifanyia kazi ili kuweze kuleta majibu juu ya tuhuma hizo. Hata hivyo, Mwanasheria wa Halmashauri hiyo, Gasper Kalinga amesema kuwa kuunda kwa kamati hiyo hiyo ni mapema mno.

"Mwenyekiti ni mapema sana kuunda Kamati ya Uchaguzi wakati Mkurugenzi hajajulishwa ni mtumishi gani ambaye amefanya kosa hilo la jinai ili waweze kuchuliwa hatua za kinidhamu," amesema Kalinga. Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Happiness Laizer amesema kuwa hadi sasa hajapokea jina la mtumishi yoyote anayetuhumiwa kufanya wizi huo, hivyo akataka uwepo ushahidi ili aanze uchunguzi.

"Unaposema unafanya uchunguzi unachunguza nini ombi langu watuletee kwa maandishi au kielelezo chochote kinachoonesha mtumishi kakamatwa akiiba dawa. “Kwa hiyo ukisema unakwenda kuchunguza na huna jina la mtumishi anayetuhumiwa, unaweza kuunda kamati na isifanye kazi yake,” amesema Laizer.

Lakini akihitimisha hoja hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga, Regnant Kivinge amemtaka Mkurugenzi huyo kufuatilia tuhuma hizo ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kwa haraka zaidi.

" Sisi Madiwani tutaendelea kukusanya ushaidi kwa kushiriana na wataalamu wa afya ili taarifa hiyo ipelekwe kwenye baraza hilo, kama itakuwa haiendani na taarifa yao basi watalazima kuunda Kamati kabla ya baraza lijalo kwa sababu wanaushaidi,” amesitiza Kivinge.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom