Madiwani walionunuliwa, Magufuli akwepa swali la Wanaarusha walipomuuliza asema sio mda wa kampeni huu ni kazi tu

"Uchaguzi umeshakwisha sasa ni maendeleo mliamua mkamchagua Magufuli na ndiyo Rais na mimi nitakuwa Rais wala sibadiliki na nitawatumikia Watanzania wote,
Hivi hii statement huwa anamaanisha au anaongea kwa mazoea tu kwa kuwa watanzania ni wasahaulifu .......... hii sentence kwa kweli haifanani na anachokifanya na kukisema majukwaani kila siku!! Halafu huwa anapenda kuirudia rudia!!
 
Hivi Kwa speed ya msafara wa Rais ni mtu gani anaweza kuingia barabarani na kuusimamisha? Tatizo letu ni Kiswahili au ni ujinga wa kudanganya wananchi? Hivi Rais anaweza kusimama tu bila kupangiwa au kupanga kwamba atasimama sehemu fulani?

Kwa nini tusiseme Rais alisemama kuwasalimia wananchi. Walau hilo linaweza kuwa na Ukweli.
Mwandawazimu aliyechoka maisha na asiyeogopa watu wasiojulikana pekee anaweza kusimamisha msafara huo!!
Naam maneno sahihi ni kusema "alisimama kusalimia wananchi" lakini kwa kuwa walishatupa kiwango cha chini cha kufikiri wanadhani tunafanana sote na kina "woyee"
 
Back
Top Bottom