Madiwani, wabunge badilisheni maisha ya wananchi - Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani, wabunge badilisheni maisha ya wananchi - Lowassa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'wanza Madaso, Jan 5, 2011.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Je hawa ipp hawajui kuwa huyu Bwana alijiuzuru sio kustaafu na Hapo chini pekundu huyu jamaa alikuwa ana maanisha nini?  Madiwani, wabunge badilisheni maisha ya wananchi-Lowassa


  Na Cynthia Mwilolezi
  5th January 2011

  [​IMG]
  Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa

  Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, ametoa wito kwa wabunge na madiwani waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu liliofanyika mwaka uliopita, kuhakikisha kuwa wanafanya kila liwezekanalo kubadilishahali ya maisha ya wananchi wao kiuchumi.

  Kadhalika, amewataka viongozi hao kuweka kipaumbele katika kujali maslahi ya wapigakura wao, ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu mzuri wakuwakopesha, ili waweze kuanzisha miradi ya kujikwamua kiuchumi, kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili wananchi wengi nchini.

  Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika kijiji cha Manyire,Kata ya Mlangarini, wilayani Arumeru, alipokuwa akizungumza katika sherehe za kuwapongeza na kuwashukuru wananchi wa kata hiyo kwa kumchagua Diwani wao, Mathias Manga (CCM).

  "Wakati umefika kwa viongozi katika maeneo mbalimbali hapa nchini kubadilika na kuacha tabia na mazoea ya kujinufaisha wao wenyewe na familia na jamaa zao na kuhakikisha kuwa wanajikita zaidi kuwatumikia wananchi hususani kujali wanakula nini," alisema Lowassa.

  Pia, Lowasa alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa uamuzi wake wa kukubali mabadiliko ya katiba na kutoa wito kwa wananchi, kuhakikisha kuwa wakati ukifika wajitokeze kwa wingi kutoa maoni yao.

  "Rais wetu hakusubiri wananchi waandamane na ndio maana kaamua kutangaza rasmi kuunda tume ya kurekebisha katiba, naomba wakati ukifika wananchi wengi jitokezeni na zoezi hilo lifanyike kwa amani na Utulivu," alisema Lowassa.

  Ama kwa upande wake, Diwani Manga aliwashukuru wananchi wa kata yake kwa kumchagua na kusema kuwa hawakukosea na atawalipa kwa utendaji wake kwa kuhakikisha kuwa anajitahidi kutatua kero sugu ambazo zimekuwa zikiwakabili kwa muda mrefu.

  "Nawaahidi hakuna mtoto hata mmoja katika kata yangu ambaye atashindwa kusoma sekondari kutokana na kukosa ada, nitajitahidi sana kwa hilo kwani hakuna urithi mzuri kama elimu," alisema Diwani Manga.

  CHANZO: NIPASHE


  Hapo pekundu huyu jamaa alikuwa ana maanisha nini?
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mbabaishaji kwa maneno tu hakuna anayemtosha, lakini mwizi mkubwa ambaye kwa miaka yote hiyo wananchi wake maskini wa kutupwa pamoja na utajiri wao wa ng'ombe. Swaini! bora akae kimya ananitia kinyaa
   
Loading...