Madiwani wa Geita waweka vizuizi lango Kuu la Geita Gold Mine kushinikiza malipo ya kodi ya Huduma

Safi sana kama hawataki kulipa wafungashe virago waende zao. Tutachimba wenyewe
 
geita+pic.jpg


Madiwani na wananchi wilaya ya Geita wamefunga barabara inayoingia mgodini kuzuia magari ya mgodi yasiingie kuelekea mgodi wa GGM mpaka walipe kodi Dola 12milioni wanazodaiwa.

Madiwani wa halmashauri mbili za wilaya ya Geita wamezuia magari ya mgodi kuingia au kutoka mgodini hadi watakapolipa kodi ya huduma wanayodai kuanzia mwaka 2003 hadi 2013

Ofisa uhusiano Mgodi huo Manase Ndoroma amesema wao wamelipa kihalali kwa mujibu wa sheria na kwamba kilichotokea ni migongano ya kisheria ambazo zote zimetungwa na bunge.

Polisi wameimarisha ulinzi katika maeneo ya Nungwe uliko mradi wa maji unaosambaza maji mgodini,eneo la uwanja Wa Ndege na geti la kuingia mgodini ambako kote kuna askari wenye silaha.

Wafanyakazi wa mgodi huo wametakiwa wasifike kazini kutokana na mgogoro uliopo mpaka watakapotangaziwa.

Habari zaidi

Polisi Geita watumia mabomu ya machozi kuwatawanya madiwani walioandamana katika mgodi wa GGM. Wawili wanashikiliwa.

CHANZO: Mwananchi
 
ha ha nchi ya wagagigigogo I never trusted Magufuli and I was right we are in the lost era, we don't have rule or law, unorganized frustrated and completely lost kama kweli hizo halmashauri zinaweza fanya fujo za kizembe namna hiyo sasa nani atasimamia sera ya uwekezaji jee hivyo viwanda vitakuja na wananchi wakianza kuehuka namna hii kwa hisia za sifa za akina msukuma
 
$12,000,000/= au nimesoma vibaya? kwani wahusika walikua wapi kudai hili deni Mpaka wasikie makinikia yamezuiwa ndio wanaibuka? Hapa iko jambo
baada ya posho kukata ndio wamezinduka, mbunge wao nae ameunga mkono au...?
 
Musukuma kazuia shughuli za GGM ni kutaka kufifisha hoja iliyoko mezani ya watu wasiojulikana.
 
Tangia juzi kumekuwepo na mgogoro wa madiwani wa Geita dhidi ya mgodi wa GGM, lakini cha ajabu umekuwa hairipotiwi humu JF wakati ni ishu kubwa kabisa.
 
Maombi siyo lazima wakusanyikae!.

Wanapiga marufuju mikusanyiko lakini hawatpiga marufuku maombi!.

Wanakamata wanaojitolea kutoa damu, lakkini hawana ubavu wa kumkamata mwombaji yeyote!

Wanaweza kupiga marufuku wasomaji albadili, lakini kwa wasomaji wa neno itakula kwao.

Wao na Bashite, sisi na Mungu!
 
Lazima iwe kimya kwa sababu Chadema walitegemea hao madiwani wa CCM wataachwa waandamane illi waseme unaona wameachwa, Sisi tukiandamana tunapigwa, nchi haifai.
Sasa hakuna cha CCM, Chadema, Cuf wala Act.
Ndo maana Uzi wanaupitia pembeni, hauna mtaji wa kisiasa upande Wao.
 
Lazima iwe kimya kwa sababu Chadema walitegemea hao madiwani wa CCM wataachwa waandamane illi waseme unaona wameachwa, Sisi tukiandamana tunapigwa, nchi haifai.
Sasa hakuna cha CCM, Chadema, Cuf wala Act.
Ndo maana Uzi wanaupitia pembeni, hauna mtaji wa kisiasa upande Wao.
Kwani JF ina wana CHADEMA peke yao?
 
Back
Top Bottom