Madiwani wa CCM wahojiwa Hanang' kwa tuhuma za kutoa siri

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Mke wa Dk. Slaa abanwa
Adaiwa kutoa siri za ubadhirifu Hanang
na Ramadhani Siwayombe, Hanang’

MKE wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, Rozi Kamili, ambaye ni diwani wa Kata ya Basotu (CCM), yupo matatani baada ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Madiwani wa Halmashauri ya Hanang', akituhumiwa kutoa siri za ubadhirifu wa fedha ndani ya halmashauri hiyo.
Licha ya kamati hiyo ya maadili kuwahoji lakini juzi imeshindwa kutangaza hatua za kinidhamu atakazochukuliwa diwani huyo na wengine watatu wa halmashauri hiyo wanaotuhumiwa kwa kukiuka kanuni za maadili za madiwani.

Madiwani wengine waliohojiwa na kamati hiyo ambao wanasubiri maamuzi ni Anju Mang'ola (CCM), Kata ya Gehandu, Leonard Gepchojiga (CCM), Kata ya Mogitu na Venosa Bura, Viti Maalumu (CHADEMA).
_________________________ Weka kando iyo kisa iko nakutokea.

Je Slaa ameshindwa kumshawishi Mkewe ajiunge na Chadema ?
Ikiwa ameshindwa kumshawishi Mkewe itawezekana kweli kuwashawishi WaTanzania waipinge na kuikataa CCM ?
Kweli ni Demokrasia lakini si kwa mke na mume ,tumeona kwengineko mara zote kwenye kampeni ya kugombea Uraisi Mgombea huwa anafuatana na Mumewe ,sasa watu hawa mbona wanatuchanganya ?
Ao ndio tuamini kuwa ni mapandikizi katika upinzani ,ile kesi ya kuwekewa vinasa sauti imeishia wapi ? Mbona imekufa tu na hakuna lolote ? This is too macha !!
 
Last edited by a moderator:
Je Slaa ameshindwa kumshawishi Mkewe ajiunge na Chadema ?
Ikiwa ameshindwa kumshawishi Mkewe itawezekana kweli kuwashawishi WaTanzania waipinge na kuikataa CCM ?

Duh! Kuna kaaazi kweli kweli. Ina maana wao ndio couple wa kwanza duniani kuwa na mtazamo tofauti wa kiitikadi/ kisiasa?

Kweli ni Demokrasia lakini si kwa mke na mume ,tumeona kwengineko mara zote kwenye kampeni ya kugombea Uraisi Mgombea huwa anafuatana na Mumewe,sasa watu hawa mbona wanatuchanganya ?

Wanakuchanganya wewe tu ndugu Mwiba. Hivi hujawahi kuona mume na mke wakiwa wanachama wa vyama tofauti na mmoja wao akagombea nafasi ya uongozi? Unaishi dunia gani ndugu Mwiba? Habari zako unazitoa wapi? Jamiiforums? Lol

Ao ndio tuamini kuwa ni mapandikizi katika upinzani ,ile kesi ya kuwekewa vinasa sauti imeishia wapi ? Mbona imekufa tu na hakuna lolote ? This is too macha !!

Unaweza kuamini chochote na lolote unalotaka lakini nakushangaa wewe kwa kuwashangaa wao. Duh! Wee kiboko.
 
Mpe mfano wa James Carville (a democratic strategist and Clinton WH senior advisor) na Mary Matalin (a republican strategist and VP Dick Cheney senior advisor)...lakini wapo kwenye ndoa kwa miaka dahali na just recently wamerudi kwao New Orleans.....siasa ni mchezo tu na sio vita!! Mweeeh

Sidhani hata kama anawajua hao maana angewajua wala asingetubutu kushangaa kama alivyoshangaa...

Mfano mwingine..Arnold na Maria...

Na kuna wengine wengi tu eg. mimi na Cupcake...
 
Hamna kitu kwa Tanzania ,siasa ni mbinde ,vipi Slaa ataweza kuwashawishi watu wengine ? Kwa kweli haingii akilini ?Asimame mbele ya Wananchi na kusema jamani Chadema ni hivi na vile nawaomba mkiunge mkono na mtupe kura zenu ,we wacha tu !! Si bora kwanza ashawishi kura ya Mkewe ? Yaani Mkeo anakushinda unakuja kwetu ! Nitamshangaa tu ! Ikiwa mkeo anaekupenda anashindwa kukuunga mkono huoni kama kuna hitilafu hapo ya uongozi unashindwa kuiongoza nyumba yako katika njia ambayo unaiona wewe ni bora hivi tukuelewe vipi? Yeye hapendelei maendeleo ambayo Mumewe anayapigia debe ?
Msilinganishe na Ulaya kwa hivi sasa wenezetu wametoka mbali sana ,na kwenye kiti Cha Uraisi sijui ni wapi ?Na iwe iwavyo lakini kwa hapa kwetu bado ni pachanga sana au kufikia stage hiyo ,ukiangalia utawala unaoungwa mkono na mkewe ni mbovu wa kupindukia ,ambao umejaa ufisadi kila kona bado hapo wanagombana kwa ubadhirifu au ufisadi ndani ya mahekalu yao ? Slaa kwa nini hamshauri mkewe kuachana na siasa za CCM ,nyinyi mnaona na kulinganisha na hao wa Ulaya lakini nina uhakika kabisa kuwa Slaa jambo hili linamzalilisha kabisa ,hasa katika wakati huu alliokuwepo wa kuomba omba kura mitaani ,mkeo ataweza kabisa kuwashawishi wanawake wenziwe kirahisi.
Jamaa amtoe mkewe kwenye CCM hakuna njia mbadala ya kubabaisha watu hapa ,na akifanikiwa basi atakuwa amepiga hatua moja ndefu sana au yeye arudi CCM yajishie ,huwezi huwezi kabisa kwa hapa Tanzania mke kuwa CCM wewe kuwepo Chama kingine mtakuwa mnadanganya tu na kuwazuga wananchi mnaweka mirija kote kote ,tukikosa huku tunapata huku au vipi ?
 
Sijui inakuaje.
Lakini hapa nadhani "hiki" ni chanzo cha habari na ndio maana Slaa anaendelea kuwa kinara wa kufichua siri nyingi dhidi ya CCM pia unaona mke wake yupo matatani sasa(ameshamaliza kazi yake).
Kama hisia zangu zipo tofauti na hayo,naomba mwenye historia sahihi ya wanandoa hao aiweke hapa JF
 
Umenifurahisha sana, bora hata Republicans wangekupa wewe kazi ya kujibu hotuba ya Obama maana naamini kabisa ungefanya kazi nzuri kuliko yule diminishing star Bobby Jindal alias Slum dog millionaire :)
 
Mke wa Dk. Slaa abanwa
Adaiwa kutoa siri za ubadhirifu Hanang
na Ramadhani Siwayombe, Hanang’

MKE wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, Rozi Kamili, ambaye ni diwani wa Kata ya Basotu (CCM), yupo matatani baada ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Madiwani wa Halmashauri ya Hanang', akituhumiwa kutoa siri za ubadhirifu wa fedha ndani ya halmashauri hiyo.
Licha ya kamati hiyo ya maadili kuwahoji lakini juzi imeshindwa kutangaza hatua za kinidhamu atakazochukuliwa diwani huyo na wengine watatu wa halmashauri hiyo wanaotuhumiwa kwa kukiuka kanuni za maadili za madiwani.

Madiwani wengine waliohojiwa na kamati hiyo ambao wanasubiri maamuzi ni Anju Mang'ola (CCM), Kata ya Gehandu, Leonard Gepchojiga (CCM), Kata ya Mogitu na Venosa Bura, Viti Maalumu (CHADEMA).
_________________________ Weka kando iyo kisa iko nakutokea.

Je Slaa ameshindwa kumshawishi Mkewe ajiunge na Chadema ?
Ikiwa ameshindwa kumshawishi Mkewe itawezekana kweli kuwashawishi WaTanzania waipinge na kuikataa CCM ?
Kweli ni Demokrasia lakini si kwa mke na mume ,tumeona kwengineko mara zote kwenye kampeni ya kugombea Uraisi Mgombea huwa anafuatana na Mumewe ,sasa watu hawa mbona wanatuchanganya ?
Ao ndio tuamini kuwa ni mapandikizi katika upinzani ,ile kesi ya kuwekewa vinasa sauti imeishia wapi ? Mbona imekufa tu na hakuna lolote ? This is too macha !!

Hiyo ni system at work, yaani nyinyi hamjuwi siku zote kuwa Slaa ni system?
 
Hamna kitu kwa Tanzania ,siasa ni mbinde ,vipi Slaa ataweza kuwashawishi watu wengine ? Kwa kweli haingii akilini ?Asimame mbele ya Wananchi na kusema jamani Chadema ni hivi na vile nawaomba mkiunge mkono na mtupe kura zenu ,we wacha tu !! Si bora kwanza ashawishi kura ya Mkewe ? Yaani Mkeo anakushinda unakuja kwetu ! Nitamshangaa tu ! Ikiwa mkeo anaekupenda anashindwa kukuunga mkono huoni kama kuna hitilafu hapo ya uongozi unashindwa kuiongoza nyumba yako katika njia ambayo unaiona wewe ni bora hivi tukuelewe vipi? Yeye hapendelei maendeleo ambayo Mumewe anayapigia debe ?
Msilinganishe na Ulaya kwa hivi sasa wenezetu wametoka mbali sana ,na kwenye kiti Cha Uraisi sijui ni wapi ?Na iwe iwavyo lakini kwa hapa kwetu bado ni pachanga sana au kufikia stage hiyo ,ukiangalia utawala unaoungwa mkono na mkewe ni mbovu wa kupindukia ,ambao umejaa ufisadi kila kona bado hapo wanagombana kwa ubadhirifu au ufisadi ndani ya mahekalu yao ? Slaa kwa nini hamshauri mkewe kuachana na siasa za CCM ,nyinyi mnaona na kulinganisha na hao wa Ulaya lakini nina uhakika kabisa kuwa Slaa jambo hili linamzalilisha kabisa ,hasa katika wakati huu alliokuwepo wa kuomba omba kura mitaani ,mkeo ataweza kabisa kuwashawishi wanawake wenziwe kirahisi.
Jamaa amtoe mkewe kwenye CCM hakuna njia mbadala ya kubabaisha watu hapa ,na akifanikiwa basi atakuwa amepiga hatua moja ndefu sana au yeye arudi CCM yajishie ,huwezi huwezi kabisa kwa hapa Tanzania mke kuwa CCM wewe kuwepo Chama kingine mtakuwa mnadanganya tu na kuwazuga wananchi mnaweka mirija kote kote ,tukikosa huku tunapata huku au vipi ?

Mwiba bwana .Unanifanya hata nishindwe pa kuanzia kutoa mawazo yangu .Yaani kama Slaa hajamfanya mkewe awe mwanachama wa Chadema basi Slaa si kiongozi wa kuheshimiwa na kusikilizwa ?Duh!Democracy at work .Slaa na system kweli ina connection na matukio ya mkewe huko kwao ?
 
Sasa ulizia ile kesi ya vinara sauti imefikia wapi nafikiri pale mlengwa alikuwa jamaa wa CUF.Si unaona hata kichwa cha habali ambacho ni cha asili wamikiondoa na kubambikiza kichwa kisicho na mvuto. ...Wana tofauti gani na hawa wanaolindana ?
 
Sijui inakuaje.
Lakini hapa nadhani "hiki" ni chanzo cha habari na ndio maana Slaa anaendelea kuwa kinara wa kufichua siri nyingi dhidi ya CCM pia unaona mke wake yupo matatani sasa(ameshamaliza kazi yake).
Kama hisia zangu zipo tofauti na hayo,naomba mwenye historia sahihi ya wanandoa hao aiweke hapa JF
ShayCas,
Usihangaike. Historia sahihi ni ifuatavyo:
i) Dr.Slaa na familia yake wamejenga Bassotu na wanashamba Muguch, Tarafa ya Bassotu.
2) Mwaka 1994 Mama Slaa, akiwa anakaa muda mwingi Bassotu kusimamia shughuli mbalimbali za familia hasa kilimo, aliingia kwenye kinyang'anyiro cha kugombea Udiwani, na akashindana na kaka yake, Bwana Joseph Marki aliyekuwa Diwani wa siku nyingi, na kumshinda kwa Tiket ya CCM.
3) Mwaka 1995 kwenye Uchaguzi Mkuu, wananchi wa Karatu, walimfuata kijana wao Dr. Slaa, ambaye wakati huo akikaa Dar ambako alikuwa akifanya kazi na Taasisi isiyo ya Serikali na kumwomba agombee. Ujumbe uliomfuata ulikuwa wa CCM, NCCR-Mageuzi, UDP na viongozi wa Kanisa Mapadre wa Kanisa Katoliki wakijua kuwa Dr. Slaa alikuwa Padre wa Kansa Katoliki). Walimwomba Dr. Slaa agombee kwa Tiket yeyote atakayochagua mwenyewe. Kutokanana historia yake ndani ya CCM, Dr. Slaa alichagua kugombea kwa Tiket ya CCM ambako alishinda kwenye kura za maoni ndani ya CCM. Kwa wanaofahamu yaliyotokea Dodoma, Dr. Slaa alihesabia kuwa siyo "mwenzetu" na jina lake kukatwa.
4) Dr. Slaa alirejea Kazini kwake Dar, na kutulia. Hata hivyo wananchi wa Karatu walimfuata wakisema kuwa walimchagua mtu na siyo Chama, hivyo walijaza formu ya chama pekee kilichokuwa wazi wakati huo, Chadema, na kumpelekea Fomu kwa saini yake (waliisha kuijaza wao). Dr. Slaa baada ya kuwasikiliza kilio chao alikubaliana nao, na kuingia kwenye uchaguzi kwa Tiket ya Chadema ( jambo ambalo leo silijutii kamwe japo wakati ule moyo uliuma lakini pia ilionyesha mambo yalivyo ndani ya CCM).Dr. Slaa alishinda uchaguzi Mkuu. Mwaka 2000 siyo tu alishinda bali pia alichukua Halmashauri ya Karatu kwa kupata Madiwani wengi zaidi kuliko CCM na hivyo kuifanya CCM kuwa chama cha Upinzani Karatu. Vivyo hivyo kwa matokeo ya 2005 CCM ilibaki kuwa chama cha Upinzani Karatu.
5) Mama Slaa aliendelea kuchaguliwa kuwa Diwani wa Bassotu kwa Tiket ya CCM mwaka 2000 na hivyo hivyo mwaka 2005. Kama kuna anayetaka kuona Demokrasia inavyofanya kazi ni vema akatembelea familia ya Dokta Slaa Karatu na Bassotu ndipo afanye "judgment" inayostahili.
6) Wasiofahamu Demokrasia wakiwemo wana CCM wamekwisha kumjadili Mama Slaa kwenye vikao vyao mbalimbali hata kwa kupanda tu gari la mumewe. Demokrasia ni vema ikaachwa ikomae kwa misingi yake bila kulazimishwa. Mama Slaa ana utashi wake wa kisiasa, na ana maamuzi yake. Kama mwelewa wa demokrasia sina sababu ya kumwingilia uhuru wake naye kama mwanademokrasia anajua anasimamia nini, na ndivyo inavyotokea siyo mara ya kwanza kuingia matatani kwa kusimamia "principles" na ukweli.
7) Nadhani kwa anayependa kupata historia kamili hayo machache yanajitosheleza.
 
Safi sana Dr.Slaa sasa wacha wenye maswali waje tena .Kaa utulie kabisa panga mkakati wa namna Chadema inaweza kupata majimbo zaidi .Mambo yawe kama Tarime .
 
Back
Top Bottom