Madiwani wa CCM wafungiwa ndani na uongozi wao wakati Dr. Slaa akihutubia Sengerema! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani wa CCM wafungiwa ndani na uongozi wao wakati Dr. Slaa akihutubia Sengerema!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyota Njema, Apr 23, 2012.

 1. N

  Nyota Njema Senior Member

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau, sisi tuliokuwepo kwenye mkutano wa hadhara wa Dr. Slaa pale Sengerema tulijulishwa na wadau kuwa madiwani wote wa CCM walikuwa wamefungiwa ndani ili wasihudhurie mkutano wa hadhara wa Dr. Slaa kwa hofu kuwa huenda na wao wangelirudisha kadi za chama chao na kujiunga na CDM kama alivyofanya mwezao ndugu Tabasamu. Hofu hii ilitokana na ukweli kuwa diwani Tabasamu alikuwa aeleze jinsi ambavyo fedha nyingi za Halmashauri ya Sengerema zilivyofujwa na uongozi wa halmashauri hiyo huku documents muhimu za wizi huo zikifichwa.

  Akielezea tukio la wizi huo, mheshimiwa Tabasamu aliueleza umati mkubwa uliohudhuria mkutano huo wa hadhara kuwa hata yeye asingelijua ni nini kilichofanyika katika kuficha uozo huo mpaka pale alipozipata nyaraka za mkaguzi wa serikali wa hesabu za halmashauri hiyo kupitia vyanzo mbalimbali kwa msaada wa ndugu Godbless Lema na vyanzo vinginevyo. Tukio hilo la kuwafungia madiwani hao pia lililenga kuwaficha madiwani hao juu ya uozo huo ingawa kwa sasa sio siri tena na huenda suala hili likaendelea kuitafuna CCM ndani ya Wilaya hiyo anakotoka Waziri wa Nishati na madini, ndugu Wiliam Gereja. Hata hivyo suala hilo lilikuwa limeshaelezwa na mheshimiwa Tabasamu katika mkutano wa hadhara uliotangulia katika mkoa mpya wa Geita, na huenda jambo hilo ndilo lililoufanya uongozi wa CCM wilaya ya Sengerema kuwafungia madiwani wake katika mkutano uliofanyika katika Wilaya yao.

  Mkutano huo uliofanyika huku mvua ikinyesha, ulishudia hujuma iliyotaka kufanywa na viongozi wasio waaminifu ndani ya CDM jimbo la Sengerema katika muendelezo wa hujuma za Ngereja pale tulipokuta hakuna viti wala vyombo vya kupazia sauti jambo lililolazimu kutumika kwa vyombo vilivyokuwepo kwenye gari ya msafara wa Dr. Slaa. Katibu wa CDM mkoa wa Mwanza aliweza kuinusuru hali hiyo pale alipofanya juhudi iliyozaa matuma kwa kutafuta vifaa hivyo na hivyo mkutano kupata usikivu mzuri kama ilivyotarajiwa. Akihutubia umati huo mkubwa, Dr. Slaa aliwaahidi wapenzi wote wa CDM kuwa angeliwachukulia hatua viongozi wote ndani ya Wilaya na Jimbo hilo waliohusika na hujuma hiyo, ikiwa ni pamoja na tuhuma nyinginezo ambazo zilikuwa zimeshawasilishwa kwenye ofisi yake pamoja na ushahidi uliokuwa utolewe kwenye mkutano wa ndani uliofanyika baada ya mkutano huo wa hadhara.

  Habari zilizopatika baadaye kutoka kwenye kikao cha ndani ni kuwa uongozi wote wa jimbo pamoja na baraza la mashauriano la Wilaya ya Sengerema walisimamishwa kazi na hivyo kuundwa uongozi wa muda wa watu wanne kulisimamia jimbo la Sengerema mpaka pale uongozi mpya utakapochaguliwa katika vikaao vya kikatiba vitakavyokaa hapo baadaye. Katika mikutano yote ya ndani na nje Dr. Slaa alizungumzia suala la kukisafisha chama katika harakati za kukiandaa kuchukua madaraka ya nchi ifikapo mwaka 2015. Alinukuliwa akisema kuwa, alipokuwa akigombea nafasi ya urais wa nchi aliahidi kuusafisha uozo wote uliopo serikalini, hivyo katika kuonyesha kuwa alikuwa anamaanisha hivyo, ameamua kufanya usafi huo ndani ya chama chake pia akiamini kuwa hawezi kuwa na serikali safi kama hana chama kisafi. Katika kutimiza azima hiyo, pamoja na kuuvua madaraka uongozi wa Wilaya na Jimbo la Sengerema, lakini pia alisimamia kumvua uanachama Mwenyekiti wa Wilaya ya Geita ambaye pia ndiye diwani wa Katoro ndugu Gervas Daudi, uongozi wa vijana wa Wilaya na Jimbo la Geita, pamoja na kuwavua uanachama baadhi ya viongozi hao wa vijana. Tukio jingine lilikuwa ni kumpa onyo kali diwani mmoja wa viti maalum ndani ya jimbo la Geita kwa kitendo chake cha kushiriki katika vurugu zilizokuwa zikiendeshwa na vijana hao kwa lengo la kukidhohofisha chama.
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Wanadhani imesaidia?
  Kimbunga kinakuja, jk akitaka kuokoa chama chake awe mtu wa maamuzi. amezubaa sana
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,494
  Trophy Points: 280
  io haisaidii kama mtu anataka kurudisha kadi ya magamba sio lazima mpaka dk awepo
   
 4. Ciphertext

  Ciphertext Senior Member

  #4
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Khaaaa! Sasa ndo nini? Wakitaka kuondoka si wataondoka tu? Akili nyingine bwana.
   
 5. kevin nathan

  kevin nathan Member

  #5
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mnayoyasema ya ukweliii
   
 6. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Dr amefanya uchunguzi wa kutosha? siasa chafu zina mambo mengi.

  Maamuzi magumu yanahitaji uchunguzi usioacha shaka.

  Je aliwapa nafasi ya kujitetea?

  kukurupaka katika maamuzi magumu kumeua vyama vya siasa kadhaa hapa nchini
   
 7. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Mama Rwakatare,
  Mambo ya magwanda yanakuhusu nini??
   
 8. The hammer

  The hammer JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 1,236
  Trophy Points: 280
  Uchunguzi wa kutosha na usioacha shaka ndio uliofikisha TANZANI hapa tulipo na hata hatuelewi tunakoenda...


  kukurupaka katika maamuzi magumu kumeua vyama vya siasa kadhaa hapa nchini....
   
 9. Asante

  Asante JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2012
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,960
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 180
  Mtoa taarifa anasema vilifanyika vikao vya ndani, bila shaka walipewa nafasi ya kujitetea, ndipo wakateuliwa wengine kukaimu nafasi zao.
   
 10. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kuna msemo huwa anapenda kuutumia ritz kuwa wanaziba shimo la panya kwa kipande cha mkate.
   
 11. MWANA WA UFALME

  MWANA WA UFALME JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Suluhisho sio kuwafungia, tatizo wanafikiri huu ni upepo wakati ni kimbunga na sio cha msimu bali ni endelevu. You cannot hide public information, otherwise you are mad man.
   
 12. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ccm bana!! Akili zao kama mbayuwayu
   
 13. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hahaa shimo la panya halizibwi kwa kipande cha mkate, by Ritz-Pro CCM
   
 14. O

  OPORO Member

  #14
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uzuri walifuingiwa kimwili uku wakiwa ndani wanawaza na kuimba nyimbo za ukombozi za CHADEMA
   
 15. d

  dguyana JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ila wametumia njia nzuri kwao ingawa inasaidia only 14% ya kimbunga. Yaani wangewaruhusu hao Madiwan kusikiliza mistari ya Dr na timu yake wangelegea kama vile wachungaji wa makanisa ya kiroho wanavyowaombeaga walokole wenye mapepo na kuanguka.
   
 16. D

  Deofm JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sasa hii ndio DEMOKRASIA gani??????, watajibuje hoja kama hawataruhusiwa kusikiliza upande wa pili?.
   
Loading...