Madiwani wa CCM na CHADEMA Nyamagana jijini Mwanza kupiga kura kutokuwa na Iman Meya Wao Mr.Mabula

Pilato

Member
May 29, 2008
60
1
Katika Hali isiyokuwa ya kawaida Meya ya jiji Hilo CCM nyamagana Bwana Mabula amenusurika kwenye kura ya Madiwani wenzake ya kutokuwa na Imani na yeye fununu: za kikao cha Mwisho cha Madiwani wa ilemela Kiliamua, kupiga kura hiyo kwenye kikao chao cha Mwisho ndio zilipotokea hoja nyingine tofauti na kusababisha kuhairishwa kwa kura hiyo.

Kwa sasa Meya hiyo yuko tumbo joto kwani ni muda wowote kitakaa kikao na kupigiwa kura za kutokuwa na Imani naye, kura hizo zitahusisha Madiwani CCM na CHADEMA ambao wote wamechaguliwa na wananchi, inasemekana sababu kubwa hasa nyingine ni kutokuwa na mahusiano mazuri na viongozi wake wa CCM na hasa nia yake ya kutaka kugombea jimbo la Nyamagana 2015 kukata mawasiliano kutopokea simu zao kipindi kunapokuwa na mambo ya msingi na pia kujiona ameota mapembe

Habari hizi ni faraja kwa CHADEMA kwani vita vya Panzi furaha ya Kunguru, maana kumekuwa na migogoro mikubwa na hadi uchakachuaji wa umeya kipindi cha nyuma wakati kukiwa na Meya wa jiji Hilo kupitia CHADEMA kabla ya kuchakachuliwa,

Ndugu wana JF mwenye zaidi atujuze....!
 
Mabula ni mstahiki meya wa halmashauri ya jiji la Mwanza sasa inakuwaje madiwani wa halmashauri ya manispaa ya ilemela wapige kura?:kev:
 
Uko sawa babu mkuu nadhanni kuna makosa kwa nilivyoelezea ila unaweza kusahihisha pale kwenye makosa kwani hiyo ndio Habari Kamili na hilo swala lipo
 
Uko sawa babu mkuu nadhanni kuna makosa kwa nilivyoelezea ila unaweza kusahihisha pale kwenye makosa kwani hiyo ndio Habari Kamili na hilo swala lipo

Mbona sijaona sehemu ilipotajwa Ilemela? Huyo babu mkuu ameiona wapi?
 
Inawezekana kabisa kwamba linapokuja suala la kumchagua meya wa JIJI ni lazima madiwani wa hizi halmashauri mbili (nyamagana na ilemela) wakutane na kukaa pamoja na kuchagua meya wa JIJI maana ndizo halmashauri zinazounda halmashauri ya JIJI.

Kitu ambacho nakikataaa hapa ni hiyo ishu ya meya wa jiji kutokupokea simu za wananzengo, kwa ninavomfahamu mimi huyu bwana haaachi kupokea simu ya mtu, labda tu awe kwenye kikao, vinginevo anapokea simu hata akiwa anaendesha gari au anakula chakula (kwa kifupi anapokea simu za watu kwa kadri inavowezekana)

Na kama kuna mtu anataka anikanushe maneno yangu basi ani-in box nimpatie namba ya huyu meya ajaribu kumpigia kwa wakati wake yeye mwenyewe binafsi na kuthibitisha haya ninayoyasema.

Napenda kuwasilisha.

Nakala kwa:

1. Great thinkers wote.

2. Meya wa JIJI la Mwanza
 
Nadhanni babu mkuu atakua amechanganya ila mada itakua sawa na imeeleweka tafadhali wana JF mwenye Mwendelezo anakaribishwa
 
hadi nakala???? Kweli uko kikazi zaidiiii. Ha ha ha.Wala siyo kwamba niko ki-kazi zaidi, bali najaribu kuweka mambo sawa (kumbuka kwamba hili ni jukwaa la GREAT THINKERS) siyo kama kule kwenye facebook nk ambako watu huzungumzia majungu, humu tunategemea mtu azungumze hoja na siyo udaku kwa maslahi yake binafsi. Na kwa msingi huo baso pale inapoonekana kunaupotoshaji basi ni vema watu tukachukua hatua kusahihisha.

Na ijulikane wazi kwamba tangu kuchaguliwa kwa meya aliyepo hivi sasa katika UONGOZI wa halmashauri ya JIJI, hakujawahi kukaa kikao cha kutokuwa na imani na meya wa JIJI la Mwanza hata siku moja. Pia kama ni kufanya mambo basi huyu meya amefanya mambo ya ukweli, uliza madiwani wa nyamagana na ilemela wakuthibitishie jinsi alivombunifu wa mambo!!!
 
Binafsi nimempigia Mei Mosi, ukweli alipokea tena bila kujua namba yangu; sijui inakuwaje. Kugombea ni haki yake kama ambavyo mimi nilimpigia kumuuliza kuhusu hayo maswala ya kugombea. Kama wananchi wanamtaka atawakilisha tu, kelele za mlango, mwenye nyumba .....
 
Du jamani inatosha tumeupata Ukweli hapahapa GT kuwa haya ni Majungu watu wanaleta siasa na mambo ya upinzani badala ya kuuendeleza Mji wa Mwanza.
Ngoja nimpigie na mimi huyo Mstahiki Mabula
 
huyu Mabula yupo anawalisha wanasiasa matumbo/njaa dinner kila siku Pizzeria pale, nadhan ndo ameona njia ya mkato kupata kura 2015. CDM tujipange kuchukua kata zote sasa.
 
Katika Hali isiyokuwa ya kawaida Meya ya jiji Hilo CCM nyamagana Bwana Mabula amenusurika kwenye kura ya Madiwani wenzake ya kutokuwa na Imani na yeye fununu: za kikao cha Mwisho cha Madiwani wa ilemela Kiliamua, kupiga kura hiyo kwenye kikao chao cha Mwisho ndio zilipotokea hoja nyingine tofauti na kusababisha kuhairishwa kwa kura hiyo.

Kwa sasa Meya hiyo yuko tumbo joto kwani ni muda wowote kitakaa kikao na kupigiwa kura za kutokuwa na Imani naye, kura hizo zitahusisha Madiwani CCM na CHADEMA ambao wote wamechaguliwa na wananchi, inasemekana sababu kubwa hasa nyingine ni kutokuwa na mahusiano mazuri na viongozi wake wa CCM na hasa nia yake ya kutaka kugombea jimbo la Nyamagana 2015 kukata mawasiliano kutopokea simu zao kipindi kunapokuwa na mambo ya msingi na pia kujiona ameota mapembe

Habari hizi ni faraja kwa CHADEMA kwani vita vya Panzi furaha ya Kunguru, maana kumekuwa na migogoro mikubwa na hadi uchakachuaji wa umeya kipindi cha nyuma wakati kukiwa na Meya wa jiji Hilo kupitia CHADEMA kabla ya kuchakachuliwa,

Ndugu wana JF mwenye zaidi atujuze....!

Wewe umeleta uzi halafu unataka ujuzwe nini,kichwa chako kimejaa majivu kweli.Hakuna wa kumtoa Mabula na Chadomo tumewachoka mwanza,hamieni moshi tu
 
JF senior expert member,nadhanni unaongea kishabiki zaidi yawezekana una Ndoa na Meya husika ,tunataka hoja iendelezwe,Ndoa zenu baadae
 
Wewe umeleta uzi halafu unataka ujuzwe nini,kichwa chako kimejaa majivu kweli.Hakuna wa kumtoa Mabula na Chadomo tumewachoka mwanza,hamieni moshi tu

Nadhanni Hauko kwenye hoja na uzalendo ,jibe hoja JF senior Expert member
 
Mabula ashugulikie wananchi wake walodhulumiwa viwanja kule mahina na luchelele kwanza
 
Back
Top Bottom