Madiwani ruksa kushindania zabuni!!

Morani75

JF-Expert Member
Mar 1, 2007
613
19
Duh jamani hapa naona kuna "conflict of interest" manake nakumbuka kwenye "Tender Committee" kwenye wilaya hapa nchini hawa waheshimiwa (at least mwenyekiti wa Council) ni active member... Well hapo ni kitu ambacho nadhani hiyo sheria inabidi iangaliwe upya manake tumeshaingiza sio mwanya bali ni pengo la ubadhirifu wa mali ya umma.... Hivi hili la "UBADHIRIFU WA MALI YA UMMA" bado ni kosa ee?? Manake naona kama vile kimekuwa kitu cha kawaida sana.... Jamani wale mnaojua "Tender Process within "TAMISEMI" na wilayani naomba mnisaidie kama nipo sawa hapa!!

Hii inalingana na kusema Katibu Mkuu wa Miundombinu anaweza kuwa mzabuni wa wazabuni ya ujenzi wa barabara... Hata kama hakai kwenye "Tender Committee" ule uoga wa kujua mmoja wa wakubwa ameweka "BID" yake kutapelekea kufanya mbinu apate kazi manake huwezi jua jamaa anaweza ulizia nani alinyima chakula pale halafu ikawa soo...

Si mnajua kwamba hawa madiwani wana mikwala an nguvu na sauti sana huko "maeneo yao ya kujidai" jamani!!


Madiwani ruksa kushindania zabuni
2007-12-17 08:32:28
Na Bigambo Jeje, PST Musoma


Serikali imezitaka halmashauri zote nchini kutowanyima zabuni madiwani kwa kusingizia kuwa hawastahili kufanya biashara na halmashauri zao.

Aidha, hakuna sheria inayowazuia madiwani kufanya biashara na halmashauri yoyote ile.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Ofisa Ugavi kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Athuman Ngwalo.

Aliyasema hayo mjini Musoma, wakati akiwasilisha mada ya ununuzi wa vifaa vya umma katika semina ya siku mbili ya Mradi wa Uwekezaji katika Kilimo Vijijini (DASIP).

Semina hiyo ilihudhuriwa na maofisa wa mradi huo kutoka Wilaya sita za Mikoa ya Mara, Mwanza na Shinyanga.

Bw. Ngwalo alisema kwa mujibu wa Sheria ya ununuzi wa vifaa vya umma ya mwaka 2004, kifungu cha tatu kimewataja watumishi wote wa serikali wasiotakiwa kufanya biashara yoyote na halmashauri au serikali kuu zikiwemo na zabuni mbalimbali.

Alisema sheria hiyo haijawataja madiwani kwamba ni watumishi wa umma hivyo wanaruhusiwa kufanya biashara hiyo.

Alisema amesikitishwa kusikia kwamba baadhi ya halmashauri zimekuwa zikiwanyima zabuni madiwani wanapoomba kazi katika halmashauri kupitia kampuni zao.

Alisema uamuzi huo ni wa uonevu na unawanyima haki zao za msingi.

Alisema awali, madiwani walikataliwa kupewa zabuni kisheria kulingana na Sheria ya ununuzi ya vifaa vya umma ya mwaka 2001 kwa kuwa walikuwa ni wajumbe wa bodi za zabuni katika halmashauri zao.

Alisema baada ya Sheria hiyo kufanyiwa marekebisho na kuwaondoa madiwani kwa kuwavua ujumbe wa bodi hizo mwaka 2004, sasa kushindania zabuni kwao si dhambi tena.

Alisisitiza kuwa kama kampuni ya diwani ina vigezo vyote vinavyotakiwa kwa mujibu wa zabuni iliyotangazwa na kuonekana imeshinda zabuni hiyo halmashauri husika inatakiwa kuitangaza kama mshindi kampuni hiyo.

Ofisa huyo alizishauri halmashauri kuzitumia taasisi za serikali kama vile vikosi vya Jeshi, Magereza na Ujenzi kufanya kazi za maendeleo katika halmashauri badala ya kutegemea wazabuni.

SOURCE: Nipashe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom