Madiwani na wabunge wa UKAWA Manispaa ya Kinondoni tumeiomba Ikulu (OFISI YA RAIS) iteue Tume huru

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,706
8,875
LEO MADIWANI NA WABUNGE WA UKAWA MANISPAA YA KINONDONI
tumeiomba Ikulu (OFISI YA RAIS) iteue TUME HURU YA UCHUNGUZI "a free and independent inquirery Commission" dhidi ya tuhuma za mkurugenzi aliyesimamishwa kazi kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zake 3:-

,i/uduni wa ubora wa barabara zilizo jengwa manispaa yabkinondoni na kushindwa kuwaadhibu wahandisi wahusika
ii/kushindwa kusimamia idara ya ardhi na mipangomiji ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi,iii/kukosa uadilifu katika ubinafsishwaji wa fukwe za cocobeach

UKAWA MANISPAA YA KINONDONI,tumegundua kuhusishwa na siasa za baada ya uchaguzi,kwa kuwakomoa,kufitinisha na kuadhibu wakurugenzi walioshindwa kuzuia UKAWA tusitangazwe kwenye uchaguzi mkuu 2015,sasa kwakubambikiwa tuhuma na kuhusishwa na ufisadi au uzembe......pia tumekiri ambapo tume itagundua mkurugenzi alikuwa na hatia ya ufisadi au uzembe pia awajibishwe kulingana na alichokitenda kwakuwa si dhumuni letu kutetea ubadhirifu au ufisadi

Tumekataa TAMISEMI kuhusika na hatua zinazofuata kwa uchunguzi kwakuwa wanajua kila kitu kinachoendelea katika UFISADI wa fukwe za COCOBEACH,kwakuwa ukweli wanaujua ila wameuficha na kumzunguka mheshimiwa Rais na kubambikia wengine.

TUMEUWEKA HADHARANI MAKATABA WA COCOBEACH,wananchi waone waliobinafsisha fukwe ya
COCOBEACH 2007, NA Majina ya waliotia saini mkataba huo mwaka 2007,wakati mkurugenzi Eng MUSSA NATTY,Aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa KINONDONI 2013.

Ukweli huu wa kusingiziwa swala la cocobeach uwe chachu ya Tume kutafuta ukweli halisi wa tuhuma zingine,kwa kuwa TAMISEMI walihusika kila hatua ya uuzaji wa fukwe hizo.

 
Hayo ndo tunaka kutoka kwa wabunge sio uonevu tu mambo ya siasa mtu afanyeje sasa watu.wameshinda na walifatilia matokeo mpaka mwisho mtegemee mkulugezi abadilishe matokeo mara usiku nyumba imechomwA moto haaa nanyie upinzani msilegelege hii ishuuu komaeni mpaka kieleweke kama kweli anahusika.basi sheria ichukue mkodo
 
Tumechoka na kuundwa kwa Tume Mhe Rais JPM kasema hadharani COCO BEACH hapewi mtu hao waliotiliana saini na mikataba yao waende Mahakamani wakaumbuane,mnataka kuleta ujanja wenu soda moja mtuuzie shs 4000/=
 
madiwani wa ukawa lazima muwe active jamani ili uwe diwani ni lazima uwe mkazi wa eneo usika na ukazi wako unathibitishwa na kitambulisho chako cha kupigia kura je hao wabunge wa viti maalum kutoka zanzibar walipiga kura zao wapi??? kama walipiga kura zanzibar basi si wakazi wa dar es salaam na hawaruhusiwi kuwa madiwani wa dar es salaam.

unakumbuka sakata la Rais Shein kuzuiwa kujipigia kura zanzibar mwaka 2010 ni suala la ukazi ndio lilimzuia kupiga kura kwani hakuwa mkazi wa zanzibar kwahiyo alikosa sifa za kupiga kura zanzibar kwahiyo ili wabunge hao wa viti maalum kutoka zanzibar hawawezi kuwa madiwani kwa sababu si wakazi wa eneo usika kulingana na kukubalika kwao kupiga kura zanzibar otherwise yangewakuta yaliyomkuta Rais Shein mwaka 2010 kwa kuwa hakuwa mkazi wa zanzibar kwahiyo alizuiwa kupiga kura huko zenji kwa kuwa wausika hawa walipiga kura hiyo inathibitisha wazi kuwa si wakazi wa dsm
 
Rais Magufuli alishasema, mambo ya mchakato na uundaji wa tume hayana nafasi katika utawala wake. Michakato na tume zinapoteza muda na pesa za wananchi.

Ukiharibu, biashara yako/kazi yako inamaliza hapo hapo.

Mahakama zipo kwa ajili ya kutafuta haki. Huyo aliyesimamishwa/kufukuzwa aende kwenye mahakama akatafute haki yake.

By the way, Huwataki TAMISEMI lakini unamtaka Rais ambaye kwa sasa TAMISEMI imehamishiwa kwenye ofisi yake! This is fun!

CHADEMA siku hizi wamekuwa watetezi wa mafisadi. Ama kweli, Mabadiliko Lowassa tuliyoyataka yamewadia!
 
Tumechoka na kuundwa kwa Tume Mhe Rais JPM kasema hadharani COCO BEACH hapewi mtu hao waliotiliana saini na mikataba yao waende Mahakamani wakaubuane,mnataka kuleta ujanja wenu soda moja mtuuzie shs 4000/=

Vichwa vya watanzania wenzetu sijui vikoje.
Huu ni wakati wa kazi mambo ya tume tupa kule yalikuwa mambo ya awamu iliyopita mnapiga hela zetu then manendeleza kuzipiga kupitia tume sisizo na tija kwetu.hakuna Haja ya tume umekosa ni kamata mahakamani segerea. Eti uadirifu kwenye kubinafsisha fukwe -hakuna uadurifu unaotakiwa katika hilo kubinafsisha tu tayari kunawaondoa kwenye ramani so hakuna ambaye angekuwa na uadirifu katika hili.
 
CCM ni ile ile usitegemee tume huru hapo, inawezekana kabisa Magufuli mwenyewe ndio ameamuru huyo mkurugenzi kubambikiwa tuhuma peke yake na kuwaacha wahandisi ambao walisimamia miradi ya barabara bila kuguswa. Pia mkumbuke kuwa huyo Mkurugenzi alikataa katakata kuburuzwa na yule DC wa Kinondoni mwenye kiherehere
 
Vichwa vya watanzania wenzetu sijui vikoje.
Huu ni wakati wa kazi mambo ya tume tupa kule yalikuwa mambo ya awamu iliyopita mnapiga hela zetu then manendeleza kuzipiga kupitia tume sisizo na tija kwetu.hakuna Haja ya tume umekosa ni kamata mahakamani segerea. Eti uadirifu kwenye kubinafsisha fukwe -hakuna uadurifu unaotakiwa katika hilo kubinafsisha tu tayari kunawaondoa kwenye ramani so hakuna ambaye angekuwa na uadirifu katika hili.

Mkuu chukuwa like 2015
Tume zinatuwekea usiku tena wakiza kinene na kwanza UKAWA Rais hawamtambui sasa hiyo tume huru akiunda wataikubali. Mambo ya Tume tupa kule,kama kuna mtu kakosea apelekwe Mahakamani kwisha.kumbuka usemi wa Mhe Lowassa alipokuwa akijibu juu ya shutuma zake alisema nini "mwenye ushahidi apeleke Mahakamani" full stop.
 
Kumbe Mussa Natty anachukiwa kwa sababu hakufanya zengwe kwa wapinzani. Sasa angewezaje na hii ni Dar watu wajanja hivi?
 
Rais Magufuli alishasema, mambo ya mchakato na uundaji wa tume hayana nafasi katika utawala wake. Michakato na tume zinapoteza muda na pesa za wananchi.

Ukiharibu, biashara yako/kazi yako inamaliza hapo hapo.

Mahakama zipo kwa ajili ya kutafuta haki. Huyo aliyesimamishwa/kufukuzwa aende kwenye mahakama akatafute haki yake.

By the way, Huwataki TAMISEMI lakini unamtaka Rais ambaye kwa sasa TAMISEMI imehamishiwa kwenye ofisi yake! This is fun!

CHADEMA siku hizi wamekuwa watetezi wa mafisadi. Ama kweli, Mabadiliko Lowassa tuliyoyataka yamewadia!

Ha ha ha.
Huyo mkurugenzi alikuwa kamanda, kada mkubwa wa team lowassa.
Lazima wambebe mwenzao.

Wanachokosea madiwani wa ukawa na ile team kubenea ni kudhani kuwa, mkurugenzi alikuwa anawajibika kisheria kuendeleza na kutekeleza mchakato usio halali ulioanzishwa na watu wengine.

Ukikuta kuna matatizo wakati wa utekelezaji wa mkataba unarakiwa kuyatatua na kuyarekebisha na sio kuendeleza uozo na uvunjaji wa sheria.

Kwa hiyo kitakachofanyika hapo ni kuongeza idadi ya watuhumiwa na sio kumuondolea jamaa yao hatia.

Naona wanamwomba rais msaada. Je wameshatambua uhalali wake? Ni kichekesho kumuomba msaada rais ambaye humtambui.
 
Ufisadi sio tena agenda ya CHADEMA. Tutegemee sana tena sana kuendelea kuona mafisadi wakitetewa na viongozi wakiwemo wabunge na madiwani kutoka CHADEMA. Mungu Mkuu ameshatunusuru na mabadiliko ambayo yangetetea ufisadi kwa kwenda mbele.

Ha ha ha.
Huyo mkurugenzi alikuwa kamanda, kada mkubwa wa team lowassa.
Lazima wambebe mwenzao.

Wanachokosea madiwani wa ukawa na ile team kubenea ni kudhani kuwa, mkurugenzi alikuwa anawajibika kisheria kuendeleza na kutekeleza mchakato usio halali ulioanzishwa na watu wengine.

Ukikuta kuna matatizo wakati wa utekelezaji wa mkataba unarakiwa kuyatatua na kuyarekebisha na sio kuendeleza uozo na uvunjaji wa sheria.

Kwa hiyo kitakachofanyika hapo ni kuongeza idadi ya watuhumiwa na sio kumuondolea jamaa yao hatia.

Naona wanamwomba rais msaada. Je wameshatambua uhalali wake? Ni kichekesho kumuomba msaada rais ambaye humtambui.
 
Siku hizi kuna mabadiliko kweli. Wezi, mafisadi na wazembe ndio wanatetewa na CHADEMA. Asante Lowassa kwa kuzidi kukiua hiko chama.

Aidha, hakuna mambo ya michakato wala tume katika utawala wa rais Dkt Magufuli. Hao madiwani na wabunge wa UKAWA wana vichwa vigumu sana kuelewa mambo madogo madogo.

CCM Mbele kwa mbele.
 
kuna watu wana akili za ajabu kweli,mtu umeambiwa kasimamishwa ili kuchunguza tuhuma dhidi yake ambao nao ni mchakato unatoka povu jingi eti serikali ya Jpm haitaki michakato wla tume nan kakuambia kua tuhuma za watendaji zitachunguzwa bila kupitia michakato kadhaa hebu tuweni na akili jaman sio kutetea vitu tu ambavyo kiuhalisia havipo vile unavyotaka.
 
Kama kawaida yenu UKAWA mmeanza kuwatetea wezi

Lkini kwa taarifa hii jinsi nilivyoelewa mimi ni kwamba UKAWA wanataka waliohusika wawajibishwe.

Yaani mkataba ulisainiwa 2007, kipindi hicho huyu Mkurgenzi alikuwa bado kwa nafasi hiyo kwani inaonyesha aliteuliwa mwaka 2013. Hivyo hakuhusika watafutwe kwanza waliohusika, ndipo na huyu naye awajibishwe kwa nini anaendeleza mkataba wenye utata??

Mfano leo Rais magufuli amekuta mikataba mbalimbali imesainiwa na marais waliomtangulia, hivyo asipokuwa makini akaipokea kama ilivyo litakuwa ni kosa, anapaswa kuifuatilia na kuona uhalali wake.

Ndivyo ilivyo katika suala hili.

Lakini hapa mtoa mada angefanya la maana endapo kama angetuwekea hadharani huo mkataba ili tuone au aseme ni Web ipi unapatikana tupate ushahidi cha walichokisema hao UKAWA.
 
Ukawa kweli malofa wamekuwa watetezi wa mafisadi!!huyu mzee anajulikana wala hakuna hata kuunda tume

Tuwe watu wa kufikiri nje ya vyama vitu ili tutendee kazi akili zetu, Eng. Natty ametuhumiwa mambo yafuatayo, mosi, ufukwe wa coco beach, pili, migororo ya ardhi na tatu ujenzi wa bara bara chini ya ya kiwango. Kwa mujibu wa taarifa zilizopo na zilizonukuliwa katika Uzi huu, mkataba wa Coco beach ulisainiwa miaka sita kabla ya Natty hajakuwa Mkurugenzi. Swali je angeweza kuuvunja? kwa mazingira ya kisheria sanjari na mazingira ya kiutawala kipindi kile ilikuwa vigumu au haiwezekani. Na kama ajenda ilikuwa ni mkataba mbovu na ufidadi kwa maoni yangu ilipaswa tuwaone Mwanasheria wa manispaa kipindi hicho, afisa ardhi, afisa mipango mini na mkuu wa wilaya nao wakiwajibishwa. Swala LA migogoro ya ardhi kwa maoni yangu limepungua sana toka 2013. Migogoro mingi us ardhi kinondoni ni muendelezo wa "makosa" yaliyofanyika kuanzia mwoshoni mwa miaka ya 90. Migogoro iliyosababishwa kuanzia mwaka 2013 ni ya kutafuta kwa microscope. Nini nafasi ya utatuzi wa Migogoro kiutawala? Ni imani yangu kuwa suala LA utatuzi wa Migogoro kwa mgawanyo wa mamlaka katika manispaa ni suala LA kisiasa hivyo linaangukia kwa mkuu wa wilaya, na ndio maana basi katika Migogoro yote uwe nchini au mahali popote wanajitokeza wanasiasa. Hii haina maana kuwa watendaji hawana nafasi LA hasha ili wanafuata maagizo na maelekezo ya wanasiasa katika kutatua jambo husika. Barabara kujengwa chini ya kiwango, Hapana nitaongea kwa kifupi tu tena kwa kuuliza swali, kwa hali ya bara bara zetu zilivyo nchi nzima , kama kigezo cha kusimamishwa kazi ni hicho ni nani atasimama? Serikali hii imeleta tumaini jipya kwa watanzania, ninaamini haki itatendeka. Kuna baadhi ya watu humu jukwaani wanaamini kuwa watu wote million sita waliomuunga mkono au kumpigia kura Lowassa ni watu waovu. Rais Magufuli ameonyesha mpenzi kwa watanzania wote bila kubagua, tumuunge mkono kwa hilo huku tukitunza na kuhesha tuni adhimu kutoka kwa Muumba, nayo ni Uhuru wa mawazo
mpaka hapo atakapopatikana na hatia kwa jicho LA kibidamu bado nitaamini katika uadilifu na uchamungu wa Eng. Natty.
 
Back
Top Bottom