Madiwani na bajeti ya kuaga mwaka 2010 sherehe mwezi ujao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani na bajeti ya kuaga mwaka 2010 sherehe mwezi ujao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinine, May 20, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,856
  Likes Received: 11,977
  Trophy Points: 280
  Baraza la Madiwani la Manispaa ya Sumbawanga, limepitisha bajeti ya sherehe za kuuaga mwaka uliopita na kuukaribisha mwaka 2011. Hata hivyo, madiwani wa chama cha upinzani Chadema, wameahidi kususia kushiriki katika sherehe hizo kwa madai kuwa kufanya hivyo ni sawa na kuendelea kubariki matumizi mabaya ya fedha za umma.

  Akizungumza katika kikao hicho kilichokuwa na mvutano mkubwa baada ya kuibuka hoja ya sherehe hizo, Diwani wa Kata ya Izia, Field Kasitu (Chadema), alisema hakuna haja ya sherehe hizo kwani sasa ni nusu ya mwaka.

  “Si busara kufanya sherehe hizo, kwani tunasherehekea kuuaga mwaka upi na kuukaribisha mwaka upi kwa sababu muda umepita na tayari tupo nusu ya mwaka…endapo baraza litakubaliana kufanya sherehe hizo, tutakuwa tumebariki ufujaji wa fedha za umma.

  “Lakini niwahadharishe madiwani wenzangu kuwa hili ni Baraza la wazi na wananchi wanaotusikiliza watatushangaa kusikia tunabariki matumizi mabaya ya fedha za wananchi kwa sherehe zilizopitwa na wakati, ni vyema busara itumike kufanya uamuzi huu,” alisema Diwani Kasitu.

  Hata hivyo Baraza hilo lilipitisha hoja ya kufanyika sherehe hizo kwa njia ya kupiga kura ambapo madiwani watano wa Chadema walipinga na 17 wa CCM wakaunga mkono hoja.

  My take: Haya ni matumizi mabaya ya mali ya umma kwanini pesa hizo zisitumike kununua madawati hata ya shule moja?
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Priorities za ccm huwa ni kutumia tuu na si kuwekeza ktk huduma muhimu za jamii!walianza na kujishonea suti,sasa sherehe
   
 3. Mtumishi Mkuu

  Mtumishi Mkuu JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Matumizi mabaya ya fedha za umma yanafanyika katika kila ngazi. Hili ni janga kwa taifa na kama hali hii haitakemewa vikali tuendeko ni hatari. Wananchi wa leo sio wale tuliozoea waliokuwa hawaulizi chochote. Nadhani katika hali ningeshauri madiwani wenye uzalendo wasusie shughuli hiyo na kuwahamasisha wananchi kufuatilia na kupinga matumizi hayo!
   
 4. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Nasikia wamemwalika Nape akatoe show, kweli?
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,477
  Trophy Points: 280
  madiwani 17 wamechaguliwa na wananhi wengi wape ngoja zitumbuliwe nao waendelee kupigika
   
 6. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,269
  Trophy Points: 280
  Siku na saa yaja, watalia na kusaga meno.
   
Loading...