Madiwani Musoma vijijini - mkurugenzi afukuzwe

Njele

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
275
121
SERIKALI imeombwa kumfukuza kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Musoma Vijijini, Karaine ole Kunei kwa madai ya kutoa zabuni ya upendeleo ya kusafirisha chakula kutoka Ghala la Taifa mkoani Shinyanga jambo ambalo limemfanya mzabuni huyo hadi juzi kushindwa kufikisha sehemu ya chakula kwa wananchi ikiwa imepita miezi saba sasa.

Madiwani wa Halmashauri ya Musoma Vijijini, walitoa ombi hilo katika Baraza la kawaida la Halmashauri hiyo juzi, ambapo walisema licha ya mtu huyo kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi hiyo lakini cha kushangaza Mkurugenzi huyo tayari amelipa karibu asilimia 70 ya fedha zilizotolewa na Serikali Kuu kwa ajili ya kusafirishia mahindi hayo ya msaada ili kuwezesha kukabiliana na njaa.

Kwa mujibu wa madiwani hao Serikali Kuu ilitoa kiasi cha zaidi ya Sh milioni 800 kwa ajili ya kusafirishia mahindi hayo zaidi ya tani 5,500 kutoka mkoani Shinyanga lakini inasemekana wakati mzabuni huyo akiwa ameleta tani 1,500, Halmashauri ilimlipa asilimia 60 ya fedha hizo kinyume cha taratibu za manunuzi.
 
Back
Top Bottom