Madiwani Moshi waishika pabaya CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani Moshi waishika pabaya CCM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Feb 1, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 82,452
  Likes Received: 47,369
  Trophy Points: 280
  Madiwani Moshi waishika pabaya CCM


  Na Heckton Chuwa, Moshi

  MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro jana waliweka pingamizi kwa Msajili wa Mahakama ya Ardhi kuzuia
  ubadilishaji au uendelezaji wa viwanja na nyumba ambavyo vinamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Moshi Mjini na jumuiya yake ya Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoani hapa.

  Akitoa tamko kuhusiana na uamuzi huo kwa niaba ya meya wa halmashauri hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira wa Halmashauri hiyo, Abdrahman Sharif, alisema madiwani wa halmashauri hiyo wameamua kuchukua hatua hiyo kutokana na taarifa za kiintelejinsia zinazoonyesha kuwa CCM wanahaha kubadili umiliki wa mali hizo.

  “Tumefanya uchunguzi wa kina kwa kuzingatia sheria zote na kubaini kuwa mali hizo ni mali halali za halmashauri ya manispaa ya Moshi,â€� alisema Diwani Sharif ambaye pia ni katibu wa madiwani wa CHADEMA katika Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo.

  Akitolea mfano wa uchunguzi huo, Bw. Sharif alisema kuwa viwanja na jengo linalotumiwa na UVCCM vyenye ukubwa wa ekari 2.7 vina hati miliki nambari 15686 na kwamba imemilikishwa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kwa miaka 33.

  “Kufuatia uhalali huu, CCM ilitakiwa iwe inailipa halmashauri sh. milioni 20 kwa mwaka na kiwanja na jengo ambalo CCM wilaya Moshi Mjini imefanya kuwa ofisi zake vina ukubwa wa square futi 18,790 na vimesajiliwa kwa hati nambari 056038/94,â€� alisema.

  Aliongeza kusema kuwa hatua walizochukua ni muhimu na zenye manufaa kwa umma na kwamba hazilengi kumkomoa mtu au taasisi yoyote zaidi ya kuzikomboa na kuzilinda mali za halmashauri hiyo.

  “Mchezo huu wa CCM umekuwa ukiidhulumu halmashauri ya manispaa ya Moshi zaidi ya sh. milioni 100 kwa mwaka na tunachotaka ni fedha hizi zitumike kwa ajili ya maendeleo ya watu wa Moshi,â€� alisema.

  Akijibu maswali kuhusiana na swala hilo, Bw. Sharif alisema uamuzi huo ni wa madiwani wa halmashauri hiyo na kwamba pamoja na kuwashirikisha madiwani wenzano wa CCM madiwani hao wa chama tawala hawakujitokeza wakati wa kutolewa kwa tamko hilo.

  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Moshi Mjini, Bw. Godfrey Mwangamilo alisema swala hilo linafuatiliwa na Katibu wa CCM wilaya ya Moshi Mjini na kwamba chama hicho kina uhalali kuhusiana na mali hizo, hivyo madiwani hao wamekurupuka.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 82,452
  Likes Received: 47,369
  Trophy Points: 280
  Hizi ni mvua za rasha rasha tu..........iko siku CCM itanyang'anywa miliki ya mali zake zote siyo kwa sababu ya kutolipa kodi za viwanja tu........bali mali hizo ni za kitaifa wakati wa mfumo wa chama kimoja na zilipaswa zirudishwe serikalini kwa sababu baada ya marekebisho ya katiba ya mwaka 1992............CCM ilikoma kuwa chama cha umma kikawa kina wenyewe .........Hivyo ni dhuluma kwa watanzania wote ambao siyo wana-CCM kuendelea kwa CCM kuhodhi mali tajwa.............ambazo ni za kitaifa na wala siyo za kichama..............
   
 3. H

  Haika JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,310
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  Jamani!!! mh
  Hata la kusema sina,
  Mie natamanisana serikali wazi, inayoendeshwa kwa misingi ya haki na usawa, kama tunaelekea huko nashukuru sana.
  Unajua ni rahisi sana kuandika humu JF lakini inapofika swala utekelezaji, mimi nami huwa napata kugugumizi, naogopa, na hofu ya hili dudu ambalo siujui mtandao wake ukoje,
  ndio maana huwa nawaheshimu sana watu wote waliojiunga na vyama vya upinzani, kwa uhakika wametoka CCM, wengi wao ni wakweli, (japo wanatetereka mara chache) na pia kuna wachache wenye tamaa,
  lakini majority wamejitolea muhanga waziwazi kupinga na kutupigania sie,

  Kuna wengi tu, wengine hadi wameshakufa hawajaiona hio Tanzania mpya,

  Mungu atawalipeni mara dufu.

  Mfano ni hili la majumba!!
  Nani asiyejua?
  sasa kuna hawa jamaa wameanza kufuatilia, wanataka haki itendeke, mjue wananchi tuko nyuma yenu, muendelee kifua mbele, mnafanya kazi ya watu, najua itakuwa ngumu sana hapo mbele, lakini inawezekana.
   
 4. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,292
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  warejeshe viwanja vyote vya michezo na maadhimisho
   
 5. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kah!!! yangu masikio na macho tu
   
 6. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Haya ndio mambo ambayo tume ya Nyalali ilishayagusia ila watawala wetu wamefumbia macho kwa makusudi kabisa. Chadema walisharudisha rasilimali za wananchi kwa wananchi kule Karatu na sasa ni zamu ya Moshi Mjini. Safi sana
   
 7. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hapa ndipo tunapoona umuhimu wa katiba mana wakati wa chama 1 ccm walitaifisha yote hayo kwa kisingizio cha chama kushika atamu
   
Loading...