Madiwani ludewa waishikisha serikali adabu, wamkataa mkurugenzi hilda lauwo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani ludewa waishikisha serikali adabu, wamkataa mkurugenzi hilda lauwo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Feb 12, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  MADIWANI katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mkoa mpya wa Njombe wamkataa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Hilda Lauwo kuwa hana uwezo wa kuongoza Halmashauri hiyo. Sura hiyo ya kukataliwa ilimkumba Mkurugenzi huyo Februari 7 mwaka huu katika kikao maalum cha baraza hilo kilichoitishwa na kufanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo ambapo pamoja na mambo mengine madiwani hao walitaka kujua matumizi ya shilingi m.6.3 zilizodaiwa kutumika kununua
  vifaa vya komputa kinyume na utaratibu.

  Hatua ya madiwani hao imekuja kutokana na Mkurugenzi kukaidi agizo lao walilolitoa januari 13 mwaka huu katika kikao cha kawaida cha balaza kilichomtaka kurudi haraka popote alipo kuja kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya fedha hizo baada ya taarifa ya mkaguzi wa ndani kuwasilishwa taarifa ya fedha hiyo mbele ya balaza hilo huku yeye akiingia mitini.

  Habari kutoka ndani ya kamati zinasema kuwa madiwani hao walikuwa wamefikia hatua ya kumtimua mkurugenzi wao lakini wakatumia busara kwa kumpa onyo asirudie kufanya kosa wakati huhuo wakimtaka ahangaike kutafuta uhamisho ama sivyo yatamkuta yaliyomkuta katika halmashauri ya mwanga alikofukuzwa na madiwani baada ya kuripoti miezi mine tu.

  Kikao hicho kilianza majira ya saa nne asubuhi kwa mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mathey Kongo kuweka bayana nia ya kikao ””kikao hiki ni kikao maalumu kwa ajili ya shughuli za Halmashauri kikao chenye tafsiri na kuona mwelekeo wa yetu,yapo mambo ndani ya Halmashauri yanahitaji muda na fursa zaidi ili yaweze kurekebishwa”” alisema kongo.

  Mbali ya madiwani hao kumakataa mkurugenzi wao pia miezi michache iliyopita mwaka jana walimkataa aliyekuwa afisa utumishi wa wilaya hiyo Juma Ally kwa madai mbali mbali yakiwemo ya kupandisha vyeo rafiki zake kinyume na utaratibu huku mbunge wa jimbo hilo la Ludewa Deo Filikunjombe akimkataa mhandisi wa maji na ujenzi kwa kufanya kazi chini ya kiwango na kuisababishia halmashauri hiyo hasaara kubwa.
   
 2. N

  Njangula Senior Member

  #2
  Feb 12, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana madiwani wetu, Filikunjombe D upo juu. Wamezoea hao kufanya wilaya shamba la bibi. Sasa makali yaelekezwe kwa wakuu wa shule wasio na jitihada yeyote ktk kufaulisha
   
 3. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwa Watumishi wa Serikali, Ludewa si mahala salama pa kufanyia kazi......unaweza hata kuzuliwa jambo!
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Filikunjombe kishachafua hali ya hewa huko, umesema kweli watumishi wa serikali ni machungu tu na mbunge huyu mwenye ucungu na wapiga kura wake.
   
 5. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  safi sana,naona taratiiiiiiiiibu watz tunaamka na kudai haki zetu
   
 6. Masimbwe

  Masimbwe Member

  #6
  Feb 12, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 5
  Safi sana madiwani ludewa kwa maamuzi hayo magumu ,endeleeni kusimamia yale mnayoyaamini
   
 7. N

  Njele JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watu wamezoea na kujenga mazoea kama ndio mfumo wa maisha.
  Lakini wakiamshwa na kusimamia kidete wanaweza kuinyoosha serikali.
  Hapa nimekubali kumbe tunaweza kuchukua Wilaya ya Ludewa kama special district for governmental corruption for research field.
   
 8. Mihayo

  Mihayo JF-Expert Member

  #8
  Feb 12, 2012
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Tatizo la Ludewa ni huyo internal Auditor aliwahi kukaa na faili langu kwa wiki mbili, kisa anahitaji kuonana na mwenye kampuni na sio kijana niliyekuwa nimekabidhi kazi ya kufatilia malipo. Nilifika Ludewa in two days alimanusra ni mchape makonde baada ya kumfungia ofisini na nikakoma kumpa chochote na malipo yangu yalitoka the next day. Nilimweleza huyu mama mtendaji wake huyu anampeleka kubaya na leonayaona yanatimia. Pole zako mama
   
 9. N

  Njele JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawa akina mama wachache waliopewa nafasi wanazitumia vibaya kuwadhalilisha wanawake wengine waonekane hawafai kupeea nafasi za uongozi kama akina Blandina Nyoni.
   
 10. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #10
  Feb 12, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama huko nako wamemkataa, arudi kwa kazi yake ya awli mama maendeleo jamii oh! afisa maendeleo
   
 11. L

  Ludewa JF-Expert Member

  #11
  Feb 12, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilda Lauwo, ana uwezo mdogo sana kiutendaji. Filikunjombe hataki ******. Am glad kwamba madiwani wapo pamoja na mbunge wao - kwenye hili.
   
 12. N

  Njele JF-Expert Member

  #12
  Feb 13, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ludewa umeona Ee! Wilaya za huko pembezoni watumishi wa serikali wamekuwa wakishindana kuchuma na bahati mbaya au nzuri sasa hivi Ludewa wameshtukiwa baada ya mbunge wao kuwafungua akili madiwani ambao kwa asa wameshikamana, mafisadi wote wataondoka sasa kwa kushinikizwa au waombe kwa ridhaa yao uhamisho. Kazi kweli kweli.
   
Loading...