Madiwani Kutumia Million 200 kwa Safari ni Ubinafsi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani Kutumia Million 200 kwa Safari ni Ubinafsi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tatanyengo, Sep 20, 2012.

 1. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hivi karibuni Mkuu wa mkoa wa kilimanjaro Leonidas Gama alisitisha safari ya Kigari, Rwanda ya madiwani wa Hamashauri ya Moshi.Hilo limeungwa mkono pia na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Muhongo Kwa hoja kwamba kiasi cha fedha ambacho kingetumika (Tsh 200) ni kikubwa ambacho kingetumika hata kuweka umeme katika shule zote za sekandari katika manipsaa hiyo.

  Safari hiyo ya Kigari ilitarajiwa kufanyika kati ya tarehe 15/9/2012 hadi 20/9/2012 na ingewahusisha watumishi 57 lengo kuu lilikuwa kwenda kujifunza usafi. Mwaka jana wa fedha bajeti ya manispaa ya Moshi ilipungua kwa asilmia 40 na haijulikani mwaka huu itapungua kwa kiasi gani.

  Maoni yangu.
  1). Kama safari ilikuwa ni ya muhimu idadi ya wana msafara ingeweza kupungua ili kupunguza gharama - watu 57 ni wengi mno. Baada ya safari wachache hao wangeweza kurudi na kuwafundisha wenzao kuhusu masuala ya usafi.
  2). Suala la usafi ni muhimu lakini siyo lazima twende tukajifunze nje ya nchi namna ya kufanya usafi.
  3). Viongozi wetu wajifunze kuweka vipao mbele na kujali zaidi maendeleo ya wanachi kuliko maslahi binafsi.
   
 2. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 180
  Naunga mkono hoja,ila sasa kuna pesa yetu iko uswis mhongo angeulizia pia kwani inatosha kununua ct scan kibao tu
   
 3. T

  Twasila JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2012
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,913
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  Kosa kubwa walilofanya Viongozi wa Manispaa ya Moshi ni kutomhusisha Gama katika ziara hiyo. Kama wangempa fedha za safari na hata kama asingeenda Kigali sh. 200m ni hela ndogo sana.
  Unajua safari moja ya Waziri Mkuu, achilia mbali Rais, hapa nchini anatumia kiasi gani yeye na kundi lake.
   
 4. M

  Magesi JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Una uhakika ni milini 200?Unajua utaratibu wa safar za mafunzo kw madiwan ukoje au mnakurupuka kimagamba 2.Mkuu wa mkoa ana hasira ya kunyimwa eneo la waz katika kata ya majengo eneo la shaurimoyo ndio kisa ya majungu yote.
   
 5. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  source plz! ama in ile ya "wewe mwenyewe?"
   
 6. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Meya wa Manispaa ya Moshi, Michael Jaffari, amemvaa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, kufuatia hatua yake ya kulizungumzia hadharani badala ya kwenye vikao vya ndani suala la ziara ya madiwani na watendaji wa manispaa hiyo kwenda jijini Kigali, Rwanda kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya siku sita.

  Gama alitangaza uamuzi huo mbele ya Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, baadhi ya madiwani wa Mansipaa ya Moshi na waandishi wa habari, na kueleza kuwa serikali mkoani hapa imeamua kusitisha ziara hiyo kwa sababu ambazo imeona ni za msingi.

  Alisema alipata barua ya kuomba kibali cha safari hiyo kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa, Agosti 31, mwaka huu, ambapo alitaka kujiridhisha kwanza kabla ya kuomba kibali kwa Waziri mwenye dhamana ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

  "Mimi ndio mwakilishi wa serikali hapa mkoani, hivyo sheria inataka kunapokuwa na safari ya nje ya nchi inayohusisha madiwani na watendaji wa halmashauri kwa kutegemea fedha za halmashauri, nijulishwe kisha nimshauri Waziri husika kwa ajili ya kupata kibali cha safari husika," alisema.

  Gama alisema kabla ya kumshauri Waziri, aliomba kujua baadhi ya mambo ikiwa ni pamoja na idadi ya watu watakaokwenda, muda, gharama na fedha hizo zitatokana na vyanzo gani vya mapato.

  Alisema alijulishwa kuwa safari hiyo ingetumia Sh. milioni 123.2, ambapo kila mshiriki angelipwa Dola 420 (Sh. 6,61500), washiriki ni wakuu wa idara 14, watendaji wa halmashauri 14 na madiwani 29, hivyo kuwa na jumla ya watu 57. Ziara hiyo ilipangwa kuanza Septemba 15 hadi 20, mwaka huu huku wakieleza kuwa vyanzo vya mapato ni ruzuku ya
  malipo ya safari za nje ya nchi na vyanzo vya ndani.

  "Nimewauliza bajeti yenu ya mwaka ya kujengeana uwezo na amfunzo ni kiasi gani, wamenieleza ni Sh. milioni 130, wataalamu wangu wamepiga mahesabu na kuonyesha kuwa fedha waliyopanga kutumia ni ndogo sana kwani ziara hiyo inaweza kugharimu kati ya Sh. milioni 150 hadi 200…busara ya kawaida kabisa inakataa matumizi ya fedha yote kwenye ziara moja," alisema.

  Gama alisema kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma, mtumishi anapojiandaa kusafiri ni lazima apewe fedha za kujiweka sawa, posho za njiani na siku anayosafiri, hivyo uwezekano wa watumishi kwenda kwa siku sita na kukubali malipo ya siku tatu pekee ni mdogo kwani wangerudi kuandika madai na kungekuwa hakuna jinsi ni lazima
  walipwe.

  Aidha, alilitaka Baraza la madiwani kujipanga upya kwenye safari za mafunzo kwani kimsingi hazikataliwi bali kinachokataliwa ni matumizi ya fedha zote za bajeti ya eneo husika kwa wakati mmoja kiasi cha kukosa bakishi iwapo patatokea dharura.

  "Bajeti ya Manispaa kwa mwaka jana ilipungua kwa asilimia 40, kwa mwaka huu bado hatujajua itapungua kwa asilimia ngapi…mimi kama msimamizi wa halmashauri katika masuala ya mapato na matumizi, siwezi
  kukubali uwepo wa safari hii na ndio maana sijamshauri Waziri, bali nimeamua kutoa maamuzi," alisema.

  Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Bernadetta Kinabo, alisema wamepokea ushauri wa Gama na wameona si vyema kwa fedha yote ya ruzuku na vyanzo vya ndani kutumika yote kwa wakati mmoja na kwamba kwa kuwa wawakilishi wa madiwani hao watano walihudhuria kikao hicho ni vyema wakafikisha taarifa kwa wengine.

  Kufuatia hatua hiyo ya Gama, Meya wa manispaa hiyo, Michael Jaffari, alisema amesikitishwa na uamuzi huo wa Mkuu wa Mkoa kulizungumzia suala hilo kwenye vikao vya wazi wakati lilikuwa ni suala la ndani kwa ndani na lingefikishwa kwenye kikao cha madiwani kwa ajili ya maamuzi.

  Alisema hatua ya Gama kuweka wazi suala hilo ni kuonyesha ana maslahi ya kisiasa na kufanya kazi kwa niaba ya wanasiasa, kwani suala hilo lilikuwa la ndani na alipaswa kuwajibu kwa utaratibu huo huo na kwamba ushauri wake wanausubiri kwa maandishi ili waweze kuufanyia kazi.

  "Kabla ya kupanga safari hii tumejipanga na kuona hasara na faida, safari hizi ni za kisheria na kanuni, tumeona kuliko madiwani na watendaj kwenda kwa kamati zao ambazo wajumbe wake wanajirudia na hivyo mmoja anaweza kwenda safari zote na ni gharama kubwa ndio maana tumepanga kwenda kwa wakati mmoja ili kupunguza gharama," alisema.

  Meya alisema kiasi cha fedha kilichotengwa kingetosha na wala watumishi wasingeweza kudai kwa kuwa ni ziara ya madiwani na ilishakubaliwa kulipwa kwa siku tatu na nyingine zingebaki kuwa fedha za kuingiza kwenye maendeleo ya wananchi kama ilivyotokea kwenye ziara ya Mombasa nchini Kenya ambako alilipwa siku mbili badala ya siku tano.

  Alisema walichagua Jiji la Kigali kwa kuwa ni moja ya jiji la mfano kwenye masuala ya usafi katika nchi za Afrika Mashariki, kama ilivyo kwa Manispaa ya Moshi, hivyo yapo mengi ambayo wangejifunza kwa manufaa ya wananchi.  SOURCE: NIPASHE
   
Loading...