Madiwani Kagera wamliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani Kagera wamliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wakurogwa, Apr 16, 2012.

 1. W

  Wakurogwa JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Katika hali isiyo ya kawaida madiwani wa Halmashauri ya wilaya Muleba huko Mkoa wa kagera wamegomea bajeti ya halmashauri hiyo hali iliyopelekea Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kulia mbele ya madiwani baada ya kushindwa kuitetea bajeti hiyo.Ikafikia wakati mkurugenzi huyo(Mwanamama) kuwatupia lawama wakuu wa idara kwa kutoa bajeti feki isiyoozingatia viwango na kudai amedhalilishwa sana na wakuu hao wa Idara kula posho nyingi halafu wanatoa bajeti mufilisi.


  Source:ITV Habari
   
 2. R

  Rweza Member

  #2
  Apr 16, 2012
  Joined: Jun 18, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chezea maDiwani wa Muleba wewe!! Hapo ndo anatoka mama Tibaijuka na yeye anawajua vyema akina Hassan Milanga, Julius Rwakyendera, Khalid Swarehe, Steven wa Mbunda n.k. Nawakubali sana makamanda na lazima Muleba inyooke. Mama Tibaijuka anapaona pachungu sana na anajuta kuwa mbunge wa eneo hilo ambalo kadri siku zinavyokwenda CDM inazidi kujiimarisha na kupata wafuasi kibao.
   
 3. Kahema

  Kahema JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2012
  Joined: May 21, 2010
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mkuu kama sikosei harimashauri hiyo inadaiwa kufuja zaidi ya bilioni kama kawaida yetu, vp hao madiwani unaowasifia hawakujua hilo? Na hau madiwani ni wa chama gani?
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  CHADEMA inafanya kazi kubwa sana ya kuwaamsha waliolala!
  Dawa ya viongozi wanaoshindwa kutekeleza mahitaji ya wananchi ndiyo hiyo.
   
 5. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,836
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Mimi Nimeona kama Mchezo wa Sandakalawe!! Madiwani wa Magamba wanajifanya wanauchungu na wananchi!! Bajeti yote Maulaji Hakuna hata hela ya kununua Madawati!! Kujenga masoko, Kuboresha Huduma za mahosipitalini, Ujenze wa barabara Duh!! Kweli kwa Bongo mvunja nchi ni Mwananchi mwenyewe!! Sasa imekuwaje hadi Wanahabari wakawepo? Planned?
   
 6. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,630
  Likes Received: 3,014
  Trophy Points: 280
  Inaonyesha aikua na maslai na wananchi,sasa yeye kinamliza nini,kwani ni bajet yake binafsi,nimemuona akimwaga chozi,
   
 7. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  safi sana..bado na pinda aangue kilio bajeti ijayo ikikwamishwa maana hii M4C huenda ikawabadilisha mpaka magmba walioko bungeni!!!!!
   
 8. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hii habari nimeiona ITV. Kwa kweli yule Mwanamama amelia mpaka basi na ameliambia Baraza la Madiwani yupo tayari kuondolewa Muleba maana anaamini Bajeti yake ilikuwa sahihi na ilizingatia vipaumbele! Hoja kuu ya Madiwani ni kuhusu Mapato ya ndani ambayo yanakadiriwa kufikia Shilingi 3.2 Billions (Kama sikosei). Kwenye hiyo Bajeti Mkurugenzi wa Halmashauri amewasilisha makisio ya matumizi kama ya Shilingi 2.7 Billions kutoa kwenye hizi Shilingi 3.2 Billions kwa ajili ya kuendesha Halmashauri na zilizobaki ndizo zitapelekwa kwenye Miradi ya Maendeleo.

  Madiwani wanataka kiasi kikubwa cha pesa kiwarudie Wananchi kwa kugharimia Miradi ya Maendeleo. Sasa Mkurugenzi yeye anasisitiza hakuna jinsi ya kuiboresha zaidi hiyo bajeti. Hapo ilipofika ndipo ukomo wake wa kiutendaji ulipokomea. Analia kwamba wamekesha maofisini na wakuu wake wa idara madiwani wanaenda kuwadhalilisha. Mama wa watu ambaye ndiye Mkurugenzi wa Halmashauri analia mpaka anatia huruma! Ndiyo usawa huo wanaoutaka kina Mama wetu. Kazi ikiwashinda wanabaki kulia kulia!
   
 9. R

  Rweza Member

  #9
  Apr 17, 2012
  Joined: Jun 18, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu hao madiwani niliowataja ni wa vyama vya upinzani. Kwa miaka mingi wilaya ya Muleba yenye majimbo ya Muleba kaskazini na Kusini imekuwa ngome ya CCM lakini kwa miaka ya karibuni wananchi wa majimbo hayo wamekuwa wakibadilika siku hadi siku na kutambua kuwa CDM ndilo tegemeo pekee na tumaini lao.
  Ukitaka kuona fika maeneo ya Ilemera, Mubunda, Kashasrunga, Magata, Kishanda, Kamachumu na maeneo mengine alafu sema Magamba ni wazuri uone utakavyopigwa mawe.
  Nadhani uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 ndo utakaodhihirisha kwamba Muleba si ngome ya magamba tena.
   
Loading...