Madiwani-CUF Kilwa wamzuia Mbunge Zainab Kawawa kupiga kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani-CUF Kilwa wamzuia Mbunge Zainab Kawawa kupiga kura

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jul 21, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Mbunge wa Viti Maalum (CCM)
  jimbo la Liwale, Zainabu Kawawa


  Madiwani wa chama cha CUF wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi, wamemzuia Mbunge wa Viti Maalum (CCM) wa jimbo la Liwale, Zainabu Kawawa, kupiga kura ya kuchagua viongozi kwa maelezo kuwa kiapo alichokula ni cha nje ya Halmashauri ya Kilwa.

  Tukio la kumzuia Zainabu kupiga kura lilifanyika wiki hii wakati wa kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo, kwenye mji mdogo wa Masoko.

  Kawawa aliyekuwa kwenye ziara ya siku moja wilayani Kilwa, alivaa joho la madiwani na kuhudhuria kikao hicho, kilichokwenda na uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilwa na madiwani watatu kuingia vikao vya Baraza la Mji Mdogo.

  Wagombea wa wadhifa huo walikuwa Abdallah Kuchao (CCM) na Mahadhi Nangona (CUF), ambapo kwa nafasi ya kuingia vikao vya Baraza la mji mdogo, wagombea walikuwa Haji Mulike, Mwanaisha Lindu, Ismaili Nalinga na Abdallah Abbasi.

  Kawawa alizuiliwa wakati wa upigaji kura kumchagua Makamu Mwenyekiti, ambapo diwani wa kata ya Lihimalyao Nangoka (CUF) alisimama na kuomba mwongozo kutoka kwa mwenyekiti wa kikao hicho, Farida Kikoleka, juu ya haki ya mbunge Kawawa kupiga kura katika kikao hicho.

  Kufuatia swali hilo, mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri aliyemaliza muda wake Farida Kikoleka na madiwani wengine wa CCM walijaribu kumtetea mbunge huyo aweze kupiga kura, lakini hawakufanikiwa.​
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ni bora hawakumuuwa kama walivyouwa Chadema.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hilo haliwezi kutokea kwa vile wao ni nyumba moja, kwani ni nyumba ndogo na kubwa, hapa ni wivu tu wa kimapenzi.
   
 4. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  family affairs; mke na mume!
   
 5. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,286
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  wivu wa kimapenzi tu hapo , ukifika usiku wanajifunika shuka moja!
   
 6. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  bi mkubwa anapomsaliti mmewe ni tabu sana........
   
 7. S

  Seif al Islam JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 2,158
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 160
  Wamekumbuka shuka asubuhi watalivuta mpaka walichane.
   
 8. B

  Bob G JF Bronze Member

  #8
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hivi viti maalumu vifutwe hata Arusha mbunge wa viti maalumu alichangia kuvuruga uchaguzi wa meya,
   
 9. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  sheikh mpaka kipindi hiki mnachofunga bado unaendeleza chuki na husuda? unatia aibu kwa waislamu wenzako
   
Loading...