Madiwani Aruaha kupongwzana leo ktk ukumbi wa manispaa kwa kumaliza tofauti zao.

Willegamba

Member
Apr 14, 2011
44
5
Ktk hali ambayo siielewi ktk suala la siasa hasa ktk jiji la Arusha, leo majira ya kuanzia saa 8:30 asubuhi limepita gari la matangazo almaharufu RAHA PROMOTION la jamaa mmoja anaejulikana kwa jina la Rama akiwatangazia wananchi wa viunga vyote vya jiji la Arusha kujumuika kwa pamoja ktk ukumbi wa Manispaa ktk hafla iliyoandaliwa kuwapongeza madiwani hao kwa kumaliza tofauti zao na kuamua kufanya kazi pamoja bila kuangalia itikadi zao za vyama. Vipi uongozi wa juu wa chama cha CHADEMA mbona hamtujulishi kulikoni?
 
Sina tatizo na watu kupengezana, ila ningependa kuwauliza madiwa hawa CHADEMA -ARUSHA, wana ujumbe gani kwa wazazi, watoto na ndugu wa marehemu 3 waliouwawa siku ya 5 January? Kwamba sasa wameshapata vyeo kwa hiyo mambo swafi? Hivi walikuwa wanaandama kwa sababu gani January 5?
 
Hata mimi nawapongeza!!!!
Tujifunze kwa yaliyotokea Zanzibar kabla na baada ya mwafaka. Tusigombee fito.......!! Madiwani wa CCM na CDM mnawajibika kuwaletea wananchi wenu wa Arusha maendeleo sio migogoro isiyo na maana!!
NAWATAKIA KILA LA KHERI!!!
 
Jibu analo Mhe Lema na militants wenzake.
Hata hivyo ujue kuwa wale marehemu ni wahanga ambao ilibidi watolewe kafara na CDM ili kupata umaarufu wa kisiasa.
Suala la Jan 5 limeisha, sasa wanatafutwa wahanga wengine kupitia maandamano dhidi ya Mgao wa Umeme.

Hiyo ndiyo sera ya chama.
 
Ktk hali ambayo siielewi ktk suala la siasa hasa ktk jiji la Arusha, leo majira ya kuanzia saa 8:30 asubuhi limepita gari la matangazo almaharufu RAHA PROMOTION la jamaa mmoja anaejulikana kwa jina la Rama akiwatangazia wananchi wa viunga vyote vya jiji la Arusha kujumuika kwa pamoja ktk ukumbi wa Manispaa ktk hafla iliyoandaliwa kuwapongeza madiwani hao kwa kumaliza tofauti zao na kuamua kufanya kazi pamoja bila kuangalia itikadi zao za vyama. Vipi uongozi wa juu wa chama cha CHADEMA mbona hamtujulishi kulikoni?[/QUOTE]

Kinachoendelea ndio hicho, ulitaka kila jambo liamuliwe na Slaa au Mbowe ndio liwe sahihi? au wao ndio wamiliki wa CDM?
 
Strategist wa hao madiwani hana maono hicho Kitendo kama ni kweli kitasaidia kamati kuu kufikia uamuzi mzuri ambao utakitikisa chama lakini mwisho wa siku wataibuka Imara Arusha.
 
Jibu analo Mhe Lema na militants wenzake.
Hata hivyo ujue kuwa wale marehemu ni wahanga ambao ilibidi watolewe kafara na CDM ili kupata umaarufu wa kisiasa.
Suala la Feb 5 limeisha, sasa wanatafutwa wahanga wengine kupitia maandamano dhidi ya Mgao wa Umeme.

Hiyo ndiyo sera ya chama.
Wewe nae acha ujinga na uchochezi wa Ki CCM, imeuwa serikali ya CCM iweje sasa muwalaumu CDM ni sera ya CCM kuuwa kwa kutumia polisi na wala hamkuanza leo, mwembechai, zanzibar, tarime, mbarali kutaja sehemu chache! Lakini pia nawapongeza hao madiwani kwa kumaliza tofauti zao, jamani " tusifukue makaburi" yamekwisha sasa madiwani fanyeni kazi kwa maendeleo ya AR
 
Itafika wakati Watanzania wataamini hakuna kiongozi anaepigania maslahi ya watanzania wote ila maslahi yake na famia yake
 
Sikuwa na maana ya fikra finyu kama ulivyoelewa kutokana na upeo wako au kikomo cha uwezo wako, sisi kama kimbilio la viongozi wetu wa chama tunahaki ya kujulishwa ni kitu gani kimefanyika na kwa maslahi gani kwa jamii au chama sababu hakuna chama bila wanahama na sisi ndio waathirika wakubwa wa maandamano ya January 5, walibaki yatima, wajane na majuruhi. Utawambia nini watu kama Hawaii?
 
Hata mimi nawapongeza!!!!
Tujifunze kwa yaliyotokea Zanzibar kabla na baada ya mwafaka. Tusigombee fito.......!! Madiwani wa CCM na CDM mnawajibika kuwaletea wananchi wenu wa Arusha maendeleo sio migogoro isiyo na maana!!
NAWATAKIA KILA LA KHERI!!!

Madai ya msingi yameshughulikiwa? Au ukipindisha sheria ukaua watu,halafu watu wanaopinga hayo nao ukawafungulia mashtaka halafu baadaye eti mnakaa kujadili mgao wa madaraka bila kujadili kilichotokea! Huo ndo muafaka?
 
Hata mimi nawapongeza!!!!
Tujifunze kwa yaliyotokea Zanzibar kabla na baada ya mwafaka. Tusigombee fito.......!! Madiwani wa CCM na CDM mnawajibika kuwaletea wananchi wenu wa Arusha maendeleo sio migogoro isiyo na maana!!
NAWATAKIA KILA LA KHERI!!!

Tatizo ni ndoa ya pamoja.
ni sisi tuliosema cuf kule zanzibar ni ccm b. je, na chadema kwa arusha tuwaite ccm b?
 
Strategist wa hao madiwani hana maono hicho Kitendo kama ni kweli kitasaidia kamati kuu kufikia uamuzi mzuri ambao utakitikisa chama lakini mwisho wa siku wataibuka Imara Arusha.

Kuliko kugawana na CCM vyeo, ni bora kubaki wapinzani tu, ule ni upuuzi kabisa.
Ningelikuwa mjumbe kwenye mkutano mkuu ningeomba madiwani wote wa chadema kupigwa chini uchaguzi uanze upya!
najua tutashinda tu.
 
mimi kwa ushauri wangu wale wote walioguswa na vifo vya vijana wa3 wajitokeze kwenye sherehe hizo wakiwa na mabango yanayohoji sababu za maandamano ya jan 5 yaliyosababisha vifo za vijana hao na damu ya vijana hao imeleta mabadiliko gani au imesalitiwa? Cdm amkeni mnachofanya mtaulizwa hata na Mungu
 
Back
Top Bottom