ARUSHA: Diwani mwingine wa CHADEMA kata ya Moita jimbo la Monduli amejiuzulu

JINOME

JF-Expert Member
May 29, 2017
958
1,424
Ni diwani wa kata ya Moita ambapo ni mojawapo ya kata zilizo katika jimbo aliyekuwa mbunge wa Monduli na waziri mkuu mstaafu Mh Edward Ngoyai Lowassa.

Akizungumza na shirika la utangazaji la TBC, diwani huyo amesema amefikia hatua hiyo baada ya kuona anakosa ushirikiano toka kwa Mwenyekiti wa halmashauri na mbunge wake. Hata hivyo madiwani wengine wamekuwa wakimpa ushirikiano.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Monduli Steven Ulaya amethibitisha kwa njia ya simu kupokea barua ya kujiuzulu kwa diwani huyo. Na amezitaka mamlaka zinazohusika kuandaa utaratibu wa uchaguzi katika kata hiyo.

Wananchi wa kata yake wamefurahiwa na maamuzi hayo na kumtaka kuachana na siasa za malumbano.

 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom