Madiwani 18 chadema jiji la mbeya wasusia kikao cha madiwani

ipogolo

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
6,241
5,915
Habari zilizopatiikana kutoka katika jiji la mbeya zinasema kuwa jumla ya madiwani 18 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) wametoka nje ya ukumbi wa mkutano kupinga ajenda zilizowasilishwa mbele yao kwa madai kuwa zilipitwa na wakati. Miongoni mwa ajenda ni suala la mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi katika jiji la Mbeya. Madiwani hao wakiongozwa na Mbunge wa CDM jimbo la uchaguzi Mbeya mjini Mh Mbilinyi aka SUGU walitaka miongoni mwa ajenda ijumuishwe inayohusu tatizo la kuungua kwa masoko mjini Mbeya. HOJA YAO NI YA MSINGI NA INA MASHIKO.
 

Mbugi

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,489
256
kuungua kwa masoko si tatizo dogo hivyo kulipaswa kuwepo kwa briefing/Taarifa ya Mkurugenzi inayoenda sambamba na ufafanuzi wa namna zoezi lilivyoenda ktk kuzima, na changamoto zake na kutoa pole kwa namna ya pekee kama viongozi/wawakilishi wa wananchi. Hoja ya kusimamia kanuni/taratibu ni ya msingi lakini ikumbukwe tu kuwa inafanya kazi pale tu taratibu hizo zinapoenda sambamba na mazingira yaliyombele yaliopo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom