Madini yawe sehemu ya usalama wa taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madini yawe sehemu ya usalama wa taifa

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by darcity, Aug 8, 2012.

 1. darcity

  darcity JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 20, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 4,817
  Trophy Points: 280
  Kwanza nimefurahishwa na uamuzi wa Rais Kikwete kuhusu uamuzi wake wa kuhakikisha kwamba tunakuwa na katiba mpya.Hii inajenga msingi imara wa maendeleo ya demokrasia pamoja nauwajibikaji wa serikali na wananchi wa Tanzania kwa ujumla.

  Kama Mtanzania mwenye uchungu wa nchi yake, nachukua nafasi hii kutoa maoni yangu na ningependa Watanzania wenzangu mniunge mkono katika suala hili kwa manufaa ya taifa letu kwa siku zinazokuja.Ningependa maoni haya yasiishie kwenye mjadala huu tu wa kwenye website hii ya tume ya kukusanya maoni ya katiba, bali pia wakati wajumbe wanaokusanya katiba wakipita maeneo mbali mbali hapa nchini wayasikie midomoni mwenu. Ndiyo sauti ya wengi siku zote hushinda! kama wahenga wetu walivyopata kusema, ''wengi wape''

  Sekta ya madini hivi sasa inakuwa kwa kasi. Kwa watu makini hili ni ashirio zuri kwa taifa na hasa uchumi wa taifa. Lakini bado haimaanishi kwamba kukua huku kwa kasi kunaambatana n aukuaji wa kasi wa usalama wa taifa letu kiuchumi na kijamii.Tanzania ina hifadhi ya mamilioni ya tani za dhahabu,almasi,shaba,makaa ya mawe,chuma cha pua,gesi carat,nikel n.k lakini bado umaskini ni wa kutupwa kwa raia wake.Pitia mitandao mbali mbali uone tunavyosanifiwa kwa umaskini wa watu wetu na utajiri wa taifa letu. Pengine hili ndilo linalonifanya niandike maoni haya.

  Ili kuhakikisha usalama wa kiuchumi wa taifa letu inabidi sasa katiba mpya ibainishe wazi kwamba sekta ya madini ni miongoni mwa vipaumbele vya usalama wa taifa. Usalama wa taifa sio tu kuwa na amani ya kisiasa na amani ya mpakani bali pia amani ya kiuchumi, hii muhimu kwa taifa na hata mwananchi wa kawaida anayekabiliwa na umaskini wa kutupwa. Tumezoea kuambiwa kwamba tanzania ni nchi yenye amani,lakini ukweli ni kwamba amani hiyo haipo kwani mamilioni ya wananchi wake wako katika dhiki kubwa huku nafsi zao zikiwa na hofu ya kuamka kesho na kupata riziki zao.

  Wakati tunatumia jitihada nyingi kulinda mipaka yetu na maadui wa ndani,tumesahau kwamba hivi sasa kumeibuka wimbi la maadui wapya wa ndani, hawa ni wafujaji wa mali za umma,wala rushwa na wakwapuaji wa fedha za umma. Ndio, hawa ndio maadui wakubwa wa usalama wa taifa letu kwa hivi sasa wakiendeshwa na tamaa na ubinafsi wa kupindukia kupitia mamlaka waliyopewa kisheria kuingia mikataba mibovu isiyo na tija kwa taifa. Ni wakati muafaka sasa kupambana nao kupitia sauti zetu.Ni wakati wa kupigania madini na rasilimali zetu dhidi ya watu wachache wasio na uzalendo wala uchungu wa taifa lao.Ni wakati ambao tunapaswa kuiga taifa la Marekani ambalo baada ya kuona linatishiwa kunyimwa mafuta na mataifa ya kiarabu katika miaka ya sabini ikaamua kuweka mafuta kuwa miongono mwa vipaumbele vya usalama wa taifa lao! inakuwaje sisi wenye wingi wa rasilimali na madini tusifanye hivo?

  MUNGU IBARIKI TANZANIA
  MUNGU IBARIKI AFRIKA

  Mtoa maoini- darcity8@gmail.com  Shirikiri kwenye mjadala katika tovuti ya tume ya katiba mpya,

  MADINI YAWE SEHEM YA USALAMA WA TAIFA
   
 2. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na mtoa mada kwa asilimia mia. Ila kwa nchi kama tanzania tuweke kipaumbele kwenye madini ambayo hayapo sehemu nyingine duniani ambazo ni Tanzaniate, Mlima Kilimanjaro, Serengeti, Ngorongoro na Selous hivi tu vikiwa ni swala la usalma wa kitaifa hata vita tunayoitaka na Malawi hatutaiwazia. Hongera sana mtoa mada.
   
 3. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,491
  Trophy Points: 280
  Usalama wa taifa upi? Huu wa Dr. Ulimboka!? Madini yakiwekwa huku hata hyo 3% hatutaiona na itakuwa hakuna kuulizana maswali kuhusu vp tunafaidika na madini yetu.
   
 4. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  tatizo ishu za usalama wa taifa huwa hazihojiwi publically na siasa chafu zishajipenyeza ndani ya hiki chombo...IDEALLY ni sahihi kuweka mambo ya msingi chini ya usalama wa taifa...ila practically umefungua mwamya mwingine wa wizi usioweza hata kuhojiwa...

  kama huamini waulize vijana wa JWTZ wanavyodhulumiwa haki zao hasa wale wanaolinda amani nchi za nje na hakuna wa kuhoji kwa kuwa ni ishu ya jeshi

  mimi naona tuendelee tu kwa staili hii hii ipo siku tutafika...BORA NUSU SHARI KULIKO SHARI KAMILI....
   
 5. Jambazi

  Jambazi JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2017
  Joined: Jan 18, 2014
  Messages: 14,412
  Likes Received: 12,530
  Trophy Points: 280
  darcity Dar tumesha pigwa sana na bado cinema linaendelea
   
 6. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2017
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,522
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Yaani siku hizi JF wanafukua makaburi si mchezo, hii ni kuonesha
  kuwa hapa kuna great thinkers si mchezo maana mambo yaliyo
  zungumzwa miaka kadhaa iliyopita athari yake inaonekana leo
   
Loading...