Madini yanamwagika ovyo matombo jamani;chukua likizo ukale shushu

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,144
Dhahabu yafumka Matombo
na Joseph Malembeka, Morogoro


ENEO la Matombo, wilaya ya Morogoro Vijijini limevamia na makundi makubwa ya watu kutoka sehemu mbalimbali nchini kutokana na eneo hilo kusadikiwa kuwapo madini aina ya dhahabu.
Kutokana na msongamano wa watu uliopo eneo hilo kuna hofu ya kutokea maafa na mlipuko wa magonjwa kutokana na wachimbaji hao kutokuwa na zana za kisasa za kuchimbia pamoja na kutochukua tahadhari ya magonjwa.

Waandishi wa habari waliotembelea eneo la machimbo hayo kandokando mwa barabara itokayo kijiji cha Matombo kuelekea Tawa, walishuhudia msongamano wa watu wakiwemo wachimbaji hao wakiendelea na kazi.

Aidha walishuhudia eneo hilo kutokuwa na vyoo huku baadhi ya wachimbaji hao wakitumia madini aina ya mekyuri kwenye maji ya mto unaotumika na baadhi ya wakazi vijiji jirani kusafisha udongo unaotolewa kwenye mashimo hayo.

Baadhi ya wachimbaji waliozungumza na waandishi walisema machimbo hayo yenye takriban miezi mitano yamewanufaisha.

“Unajua vijana hatuna ajira za kutuwezesha kujikimu, hivyo tunahangaika kutafuta riziki...tunaiomba serikali ituboreshee zana za kuchimbia hapa hela ipo ila tatizo ni mtaji,” alisema Kisheki Mihangwa kutoka mkoani Mbeya.

Akizungumzia suala hilo, mkurugenzi mtendaji wa halamashauri hiyo, Eden Munisi, alikiri kuibuka kwa machimbo hayo na kuongeza kuwa halmashauri inakusudia kuyaboresha kwa kupata mwekezaji atakayeiwezesha halmashauri kuongeza chanzo cha mapato. Kuhusu wachimbaji wadogo, alisema mpango mzuri wa kuwawezesha unaandaliwa na wataalamu wa machimbo ili na wao waweze kuendeleza shuguli hizo kwa faida na tija badala ya kutumia njia ya kubuni ambayo haina faida.
 
Gama unabana unasema chile uku unajaza form za likizo siyo
 
Dhahabu yafumka Matombo
na Joseph Malembeka, Morogoro

.......Aidha walishuhudia eneo hilo kutokuwa na vyoo huku baadhi ya wachimbaji hao wakitumia madini aina ya mekyuri kwenye maji ya mto unaotumika na baadhi ya wakazi vijiji jirani kusafisha udongo unaotolewa kwenye mashimo hayo. Baadhi ya wachimbaji waliozungumza na waandishi walisema machimbo hayo yenye takriban miezi mitano yamewanufaisha...........

Matumizi ya mercury kwenye maji ya mto unaotumika na baadhi ya wakazi vijiji jirani bila kuzingatia masuala ya elimu ya mazingira ni hatari sana kwa binadamu, ni muhimu Halmashauri na Serikali kuu zichukue hatua za haraka kudhibiti uharibifu wa mazingira kabla maafa yatokanayo na mercury/zebaki hayajaanza kujitokeza!!!
 
Back
Top Bottom