Madini ya makaa ya mawe yanavyonufaisha Wahindi, Waarabu na Wazungu na kuwaachia mashimo wenye madini yao

Haco You

Member
Jul 2, 2022
8
7
Kwa udogo wangu wa uelewa nimekua nikifanya uchunguzi mdogo wa jinsi sekta ya madini inavyo watajirisha wageni na kutuachia mashimo na faida chache ya Kodi ambayo ukiifatilia bado ni ndogo ukilinganisha na thamani ya madini husika.

Tanzania tumebarikiwa madini mengi sana kama dhahabu, almasi,Tanzanite na mengineyo lkn mm ntaongea kidogo kuhusu makaa ya mawe madini ambayo mikoa mikubwa mitatu kwa maana ya Njombe,Ruvuma na Mbeya imebarikiwa nayo.

Madini haya yameanza kuchimbwa kwa wingi sana katika mikoa hii miwili ya Ruvuma (mbinga) na Njombe (Ludewa) wawekezaji wengi kutoka nje na ndani wamejitokeza kuwekeza katika uchimbaji huo lkn kinachosikitisha wawekezaji hawa wengi wao ni wahindi,waarabu na wazungu wachache.

Wahindi na waraabu hawa wengi wao sio raia wa Tanzania au wamepitia kwa wahindi na waraabu wenzao ambao wamefanikiwa kupata urai na kuanzisha kampuni Tanzania na kuwaficha hawa wenzao kutoka njee.

Wawekezaji hawa wamekua wakichimba madini,kusafirisha na kuyauza na kupata faida kama biashara zingine lkn ukifatilia sana faida zao hazibaki nchi kuindeleza nchi yetu. Wengi wamekua wakiishi Bongo lkn baba zao na babu zao wako asia na ulaya huko na ndiko pesa kama faida hasa zinakoenda.

Wabongo wachache sana ambao wameweza kuingia kwenye uchimbaji huu ambao kiuhalisia ndio wangeweza kuifanya faida hii kubaki nchini na kuongeza mzunguko wa pesa na uchumi kwa ujumla.

Kama hali itabaki hivi tukubali kwamba midini haya yatachimbwa yatauzwa yataisha tutabaki na mashimo makubwa na faida ndogo kupitia kodi tu.

Lazima serikali ione namna ya kuwasaidia wawekezaji wazawa tema wenye uraia kamili wa kuzaliwa na kukua ili waweze kunusuru faida hizi kwenda nchi zingne.
 
Kama sisi tumelala tufanyaje sasa, KILA mtu akipata pesa ukimbilia biashara moja ya kuigana mfano kununua mabus au malori, then baada ya mda anafilisika, kubuni fursa kubwa na za uhakika kama hizi za uchumi hatuwezi. Eti leo Mchina katoka kwao kaja kutengeneza nguzo za zege anawauzia tanesco sisi hatuwezi ona fursa.
Sisi ni walinzi wa mali wao ndo wanufaika wa hizo mali
 
Wenye macho ya kuziona fursa nchini ni wachina na sio sisi.
Fursa zipo nyingi Sana hasa kipindi hiki cha upandaji vitu bei, we zalisha mbadala wake uwe tajiri. Watu upenda mbadala kwa bei nafuu.
Ngoja wachina wavune fursa.
 
Bila kusahau wachina na mabonanza (kamari) yao yapo mpaka vilabu vya pombe za kienyeji
 
Tuacheni roho za kwanini na kuonea wivu wageni,,kwani watu wa nje wana shida gani ikiwa uendeshaji wao wanaendesha kihalali na kufuata sheria!!

Halafu Waafrika sio watu wa kazi, wachache waliochangamka/fungua akili.
 
Ishu ni mtaji, ila hayo makaa ya mawe yanalipa sana. Nimewahi pata muongozo kuhusu hiyo biashara, aisee nilibaki nashangaa kutokana na ile faida inapatikana.
 
Hawa wahindi wengi ni wezi wakishirikian na viongozi wetu, ndio maana hata hivi majuzi dewji alikomalia wamasai waondoke loliondo waende walikopangiwa na serikali, sasa anajiuliza huyu muhindi anatoa wapi guts wa kumwambia mwafrika atoke eneo lake la asili?
 
Kama vijana mada zao ni hizi za kula tunda kimasikhara kila siku na dawa za kuongeza nguvu za kiume basi tutakuja kuuzwa siku moja na sisi.
 
Kwa udogo wangu wa uelewa nimekua nikifanya uchunguzi mdogo wa jinsi sekta ya madini inavyo watajirisha wageni na kutuachia mashimo na faida chache ya Kodi ambayo ukiifatilia bado ni ndogo ukilinganisha na thamani ya madini husika.

Tanzania tumebarikiwa madini mengi sana kama dhahabu, almasi,Tanzanite na mengineyo lkn mm ntaongea kidogo kuhusu makaa ya mawe madini ambayo mikoa mikubwa mitatu kwa maana ya Njombe,Ruvuma na Mbeya imebarikiwa nayo.

Madini haya yameanza kuchimbwa kwa wingi sana katika mikoa hii miwili ya Ruvuma (mbinga) na Njombe (Ludewa) wawekezaji wengi kutoka nje na ndani wamejitokeza kuwekeza katika uchimbaji huo lkn kinachosikitisha wawekezaji hawa wengi wao ni wahindi,waarabu na wazungu wachache.

Wahindi na waraabu hawa wengi wao sio raia wa Tanzania au wamepitia kwa wahindi na waraabu wenzao ambao wamefanikiwa kupata urai na kuanzisha kampuni Tanzania na kuwaficha hawa wenzao kutoka njee.

Wawekezaji hawa wamekua wakichimba madini,kusafirisha na kuyauza na kupata faida kama biashara zingine lkn ukifatilia sana faida zao hazibaki nchi kuindeleza nchi yetu. Wengi wamekua wakiishi Bongo lkn baba zao na babu zao wako asia na ulaya huko na ndiko pesa kama faida hasa zinakoenda.

Wabongo wachache sana ambao wameweza kuingia kwenye uchimbaji huu ambao kiuhalisia ndio wangeweza kuifanya faida hii kubaki nchini na kuongeza mzunguko wa pesa na uchumi kwa ujumla.

Kama hali itabaki hivi tukubali kwamba midini haya yatachimbwa yatauzwa yataisha tutabaki na mashimo makubwa na faida ndogo kupitia kodi tu.

Lazima serikali ione namna ya kuwasaidia wawekezaji wazawa tema wenye uraia kamili wa kuzaliwa na kukua ili waweze kunusuru faida hizi kwenda nchi zingne.
yeah unachokisema ni kweli lakini tukumbuke serikali imefanya pakubwa kuwezesha wazawa kufanya biashara hizi kubwa. kuna sheria ya loca content, kuna mabenki yanatoa mikopo.n.k. tunachokikosa kikubwa ni MAARIFA. na pia ubinafsi wa watu wachache wenye madaraka serikalini. kumbuka issue ya hayati mzee Mengi na vitalu vya gesi. kwa kiasi kikubwa tunakosa maarifa ya kuzirukia fursa tunasubiri kuiga. acha tu wafaidike hivi ndio tunajifunza vizazi vijavyo pengine vitakuwa na maarifa
 
Hawa wahindi wengi ni wezi wakishirikian na viongozi wetu, ndio maana hata hivi majuzi dewji alikomalia wamasai waondoke loliondo waende walikopangiwa na serikali, sasa anajiuliza huyu muhindi anatoa wapi guts wa kumwambia mwafrika atoke eneo lake la asili?
Wewe naye kaibe kama waona rahisi
 
Hivi majuzi nilikwenda Rombo hakika huko njiani nilikutana na magari makubwa aina ya FAW yakipishana kutoka/kuingia nchini Kenya mwanzo mwisho! Nikawa najiuliza kwa staili hii miaka kadhaa ijayo Tanzania kutabaki na kitu kweli! Yalikuwa yamebeba makaa ya mawe
 
Back
Top Bottom