Madini ya bati yatishia kasi ya kilimo mkoani

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Imeandikwa na Deus Gabone, Karagwe;

Tarehe: 15th October 2011

KUIBUKA ghafla kwa soko la madini ya bati yanayopatikana katika wilaya mpya ya Kyerwa mkoani Kagera, huenda kukaathiri jitihada za serikali za kufufua kilimo kupitia sera ya Kilimo Kwanza.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, kilo moja ya madini hayo huuzwa kwa kati ya Sh 17,000 na Sh 20,000, hali iliyochangia kuwavutia wengi, hasa wakulima ambao wameamua kutelekeza mashamba yao na kukimbilia katika biashara ya madini ya bati ambayo soko lake lipo nchi jirani ya Uganda.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wachimbaji hao wamedai kuwa, wameyachukuliwa madini kama mkombozi wao, baada ya kulima kwa muda mrefu, lakini mazao yao yakikosa soko la uhakika na hivyo kupata usumbufu katika kuchangia shughuli za maendeleo, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule za kata na zahanati.

"Lakini sasa madini yanalipa, hatuwakimbii tena wanaochangisha fedha za miradi ya maendeleo," anasema mmoja wa wakazi wa kijiji cha Nyaruzumbula yalipo machimbo hayo.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kaitambuzi, Deodatus Kainamula amethibitisha wakazi wengi kuchangamkia madini ya bati na kuongeza kuwa, kwa takribani miaka miwili sasa, wananchi wana uwezo wa kuchangia shughuli za maendeleo bila ya usumbufu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
 
Imeandikwa na Deus Gabone, Karagwe;

Tarehe: 15th October 2011

KUIBUKA ghafla kwa soko la madini ya bati yanayopatikana katika wilaya mpya ya Kyerwa mkoani Kagera, huenda kukaathiri jitihada za serikali za kufufua kilimo kupitia sera ya Kilimo Kwanza.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, kilo moja ya madini hayo huuzwa kwa kati ya Sh 17,000 na Sh 20,000, hali iliyochangia kuwavutia wengi, hasa wakulima ambao wameamua kutelekeza mashamba yao na kukimbilia katika biashara ya madini ya bati ambayo soko lake lipo nchi jirani ya Uganda.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wachimbaji hao wamedai kuwa, wameyachukuliwa madini kama mkombozi wao, baada ya kulima kwa muda mrefu, lakini mazao yao yakikosa soko la uhakika na hivyo kupata usumbufu katika kuchangia shughuli za maendeleo, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule za kata na zahanati.

“Lakini sasa madini yanalipa, hatuwakimbii tena wanaochangisha fedha za miradi ya maendeleo,” anasema mmoja wa wakazi wa kijiji cha Nyaruzumbula yalipo machimbo hayo.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kaitambuzi, Deodatus Kainamula amethibitisha wakazi wengi kuchangamkia madini ya bati na kuongeza kuwa, kwa takribani miaka miwili sasa, wananchi wana uwezo wa kuchangia shughuli za maendeleo bila ya usumbufu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

gazeti gani mkuu!
 
Back
Top Bottom