Madini Mrahaba Asilimia Tatu 3% ni haki kweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madini Mrahaba Asilimia Tatu 3% ni haki kweli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fredrick Sanga, Feb 1, 2011.

 1. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Botswana has 3 major mineral resources, namely diamonds, copper/nickel and soda ash all of which contribute significantly to GDP and exports. Diamonds, with dwarf all others, contribute significantly to Government Revenue. In 1998/99, mining contributed 32.5% of GDP, 74.0% of exports and 55.6% of Government revenue

  All the mining ventures are operated as private companies, although Government has significant shareholding. With respect to the Debswana Mining Company, it is owned on 50:50 basis between Botswana Government and De Beers Centenary AG of Switzerland. Ownership of BCL, the copper/nickel mine, is approximately 33% each by Government of Botswana and Anglo American Corporation with the balance held by members of the public. Botswana Ash, the soda ash mining company, is owned 50:50 between the Government of Botswana and a group of private companies including Anglo American Corporation, De Beers, African Explosives and Chemicals Industries (PTY) Ltd. And three South African banks. (UNCTAD, 2000)

  Kwa kutumia wadhifa wake kama Waziri wa Fedha, alishinikiza kampuni ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation ya Washington DC, Marekani kupewa kazi ya kukagua mahesabu ya makampuni ya uchimbaji dhahabu. Chini ya mkataba wake na Serikali ya Tanzania, Kampuni hiyo inalipwa asilimia 1.9 katika ya asilimia 3 za mrahaba inaolipwa Serikali ya Tanzania na makampuni ya madini ya dhahabu. (Uadilifu Blog)

  [FONT=Courier, Monospaced]WAKATI makampuni ya madini yameweza kujikusanyia jumla ya Sh2,339.63 bilioni katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, serikali imeambulia Sh72.37bilioni tu kama mrabaha kutokana madini. Mbaya zaidi, fedha hizo za mrabaha pia zimemegwa kwa ajili ya kuilipa kampuni ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation (Asagbc), kiasi cha Sh38.7 bilioni na kufanya mapato halisi ya serikali katika kipindi hicho kubaki Sh33.6 bilioni tu. Takwimu hizo zinatokana na hesabu iliyokokotolewa na watalaam wa Wizara ya Nishati na Madini na kutolewa bungeni na Naibu Waziri, Bernard Membe, wakati akijibu maswali ya wabunge.

  Hata hivyo, Membe aliweka mkazo zaidi katika kiasi cha fedha ambazo serikali imeilipa Kampuni ya ukaguzi wa gharama za uwekezaji na uendeshaji migodi ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation (Asagbc), akisema kutokana na ukubwa wa gharama, serikali inafikiria kuangalia upya mkataba na kampuni hiyo.

  Kumekuwapo na malalamiko ya muda mrefu juu ya kiwango kidogo cha mrabaha ambacho serikali inayatoza makampuni ya madini, baadhi ya watu wakiulinganisha utaratibu huo na uporaji wa wazi wa rasilimali ya Watanzania.

  Akizungumza bungeni mjini hapa jana Membe, alisema serikali inailipa kampuni hiyo fedha nyingi kila mwezi na kwamba kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka huu, imeshalipwa dola za Marekani 31 milioni (zaidi ya Sh38 bilioni).

  Kwa mkataba uliopo, serikali inalipwa asilimia tatu ya mapato ya madini, lakini kutokana na kukodi kampuni ya kusimamia uendeshaji na uzalishaji katika migodi hiyo, inatumia asilimia 1.9 ya fedha hizo na yenye ikibakia na
  asilimia 1.1 tu.

  Kiasi hicho cha fedha kilicholipwa kwa kampuni hiyo kimeelezwa kuwa ni kikubwa kuliko gharama zilizotumika kujenga jengo jipya la kisasa la Bunge lililogharimu Sh31 bilioni.

  Kutokana na gharama kubwa inayoingia serikali kuilipa kampuni hiyo fedha nyingi kila mwezi, Membe alisema sasa inafikiria kuuangalia upya mkataba wa kampuni hiyo ili kuipunguzia mzigo serikali.

  Alisema Juni, 2003, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa niaba ya serikali, iliingia mkataba wa miaka miwili na kampuni hiyo kwa lengo la kuhakiki uzalishaji na gharama za usafirishaji wa dhahabu pamoja na uwekezaji na uendeshaji wa migodi mikubwa nchini na kwamba mkataba huo ulimalizika Juni mwaka jana.

  Hata hivyo, Naibu huyo Waziri wa Madini na Nishati, alisema baada ya mkataba huo kumalizika BoT haikuitisha tenda nyingine kama ilivyofanya mwaka 2003 na ikaipatia tena kampuni hiyo mkataba wa miaka miwili zaidi kwa kutumia kifungu namba 2.4 cha mkataba huo kinachoruhusu BoT kuongeza muda wa mkataba iwapo inaridhika na utendaji kazi wa kampuni hiyo.
  Membe alikuwa akitoa maelezo hayo wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu (CCM), Aziza Sleyum Ally, aliyetaka kujua kampuni gani iliyopata tenda hiyo na kama ni kampuni hiyo iliyomaliza mkataba wake na je tenda hiyo ilitangazwa lini na ilipitishwa na nani.
  Source - Mwananchi
  [/FONT]  Tell me now, why 3% in Tanzania, Hebu majasusi wa tanzania tuelezeni, maana kwenye JF hamuonekani.
   
 2. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Inafurahisha, maana mapato yetu yatadondoka kutoka juu si ndio ee.
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  tumekosea tangu mwanzo
   
 4. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Sasa tunaacha hivi hivi, mbona kama tumelaanika hivi. hivi nani anaweza kukukodisha hata shamba lake kwa mrahaba kama huo?
   
 5. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mhhh vaaa Sanga haya mambo bwana wenye uchungu nao ni wale wenye akili ya UJASILIA MALI lakini wakwele hawa hata hawafikilii hilo, wanaona sawa tuu! SI WAMEZOEA VYA KUPEWA IJUMAA.
   
 6. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  MAJADILIANO yaliyodumu kwa takribani mwaka mmoja sasa baina ya Serikali na kampuni ya uchimbaji madini ya Anglogold Ashanti (AU) ya Afrika Kusini kuhusu mkataba mpya wa madini, sasa yamekamilika na mkataba huo unatarajiwa kusainiwa wakati wowote kuanzia sasa.

  Pamoja na mambo mengine, mkataba huo mpya umeifutia kampuni hiyo msamaha wa kodi baada ya kufanya kazi zake nchini kwa miaka kadhaa sasa.

  Jarida la Dow Jones Newswires limesema katika toleo lake la Jumatatu wiki hii kuwa mkataba huo mpya utasainiwa siku yoyote wiki hii jijini Dar es Salaam.

  Hata hivyo jarida hilo lililotoa taarifa hiyo kwa kumnukuu afisa mmoja wa Wizara ya Nishati na Madini linasematangu mwaka jana, Tanzania imekuwa ikipitia mikabata yote ya madini nchini kwa lengo la kuiboresha na kuifanya sekta ya madini ili kulinufaisha taifa zaidi kuliko wawekezaji.

  Kukamilika kwa makubaliano hayo kumekuja muda mfupi baada ya serikali kupitia upya mikataba yake na kampuni za madini za Barrick Gold Corp (ABX) ya Canada na Resulute Mining Ltd (RSGAU) ya Australia.

  Katika mikabata hiyo mipya makampuni yote ya madini nchini yatatakiwa kuilipa serikali hadi dola za Marekani 200,000 kwa mwaka ambazo ni pamoja na asilimia 15 ya kodi ya mgodi na asilimia 30 kodi inayotokana na mauzo ya madini kutoka kwenye mgodi husika

  Kampuni ya AngloGold Ashanti ndiyo mmiliki wa mgodi wa Geita ambao ni mkubwa kuliko yote nchini ukiwa na uwezo wa kuzalisha hadi uzani wakia 600,000 za dhababu kwa mwaka.

  Kwa ujumla wake Tanzania inazalisha kiasi cha wakia 1.75 milioni za madini kwa mwaka ikiwa inashika nafasi ya tatu barani Afrika baada ya Afrika Kusini na Ghana.

  Source: Mwananchi


  Hivi sasa mrahaba ndio unafutwa au vipi, kwani kuna tofauti ya kodi na mrahaba?
   
 7. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  [FONT=Courier, Monospaced]WAKATI makampuni ya madini yameweza kujikusanyia jumla ya Sh2,339.63 bilioni
  katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, serikali imeambulia
  Sh72.37bilioni tu kama mrabaha kutokana madini.

  Mbaya zaidi, fedha hizo za mrabaha pia zimemegwa kwa ajili ya kuilipa
  kampuni ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation (Asagbc),
  kiasi cha Sh38.7 bilioni na kufanya mapato halisi ya serikali katika kipindi
  hicho kubaki Sh33.6 bilioni tu.

  Takwimu hizo zinatokana na hesabu iliyokokotolewa na watalaam wa Wizara ya
  Nishati na Madini na kutolewa bungeni na Naibu Waziri, Bernard Membe, wakati
  akijibu maswali ya wabunge.

  Hata hivyo, Membe aliweka mkazo zaidi katika kiasi cha fedha ambazo serikali
  imeilipa Kampuni ya ukaguzi wa gharama za uwekezaji na uendeshaji migodi ya
  Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation (Asagbc), akisema
  kutokana na ukubwa wa gharama, serikali inafikiria kuangalia upya mkataba na
  kampuni hiyo.

  Kumekuwapo na malalamiko ya muda mrefu juu ya kiwango kidogo cha mrabaha
  ambacho serikali inayatoza makampuni ya madini, baadhi ya watu
  wakiulinganisha utaratibu huo na uporaji wa wazi wa rasilimali ya
  Watanzania.

  Akizungumza bungeni mjini hapa jana Membe, alisema serikali inailipa kampuni
  hiyo fedha nyingi kila mwezi na kwamba kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka huu,
  imeshalipwa dola za Marekani 31 milioni (zaidi ya Sh38 bilioni).

  Kwa mkataba uliopo, serikali inalipwa asilimia tatu ya mapato ya madini,
  lakini kutokana na kukodi kampuni ya kusimamia uendeshaji na uzalishaji
  katika migodi hiyo, inatumia asilimia 1.9 ya fedha hizo na yenye ikibakia na
  asilimia 1.1 tu.

  Kiasi hicho cha fedha kilicholipwa kwa kampuni hiyo kimeelezwa kuwa ni
  kikubwa kuliko gharama zilizotumika kujenga jengo jipya la kisasa la Bunge
  lililogharimu Sh31 bilioni.

  Kutokana na gharama kubwa inayoingia serikali kuilipa kampuni hiyo fedha
  nyingi kila mwezi, Membe alisema sasa inafikiria kuuangalia upya mkataba wa
  kampuni hiyo ili kuipunguzia mzigo serikali.

  Alisema Juni, 2003, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa niaba ya serikali,
  iliingia mkataba wa miaka miwili na kampuni hiyo kwa lengo la kuhakiki
  uzalishaji na gharama za usafirishaji wa dhahabu pamoja na uwekezaji na
  uendeshaji wa migodi mikubwa nchini na kwamba mkataba huo ulimalizika Juni
  mwaka jana.

  Hata hivyo, Naibu huyo Waziri wa Madini na Nishati, alisema baada ya mkataba
  huo kumalizika BoT haikuitisha tenda nyingine kama ilivyofanya mwaka 2003 na
  ikaipatia tena kampuni hiyo mkataba wa miaka miwili zaidi kwa kutumia
  kifungu namba 2.4 cha mkataba huo kinachoruhusu BoT kuongeza muda wa mkataba
  iwapo inaridhika na utendaji kazi wa kampuni hiyo.
  Membe alikuwa akitoa maelezo hayo wakati akijibu swali la mbunge wa viti
  maalumu (CCM), Aziza Sleyum Ally, aliyetaka kujua kampuni gani iliyopata
  tenda hiyo na kama ni kampuni hiyo iliyomaliza mkataba wake na je tenda hiyo
  ilitangazwa lini na ilipitishwa na nani.
  Source - Mwananchi
  [/FONT]


  Haijafanyiwa kazi na wenye nchi. Tunashambuliana kwenye mambo ya udini tu. We are remotely controlled
   
Loading...