Madikteta na Mafisadi Africa wazidi Kushughulikiwa, Binti wa rais wa zamani Angola atorokea Ulaya

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Hii ni furaha kwa wanyonge kwa Rais Dos Santos kushughulikiwa

Alifikiri kutafuta mtu atakayemrithi itakuwa nafuu kwake..

======

pic+binti+rais.jpg

Kwa ufupi
  • Binti huyo alikuwa kiongozi wa shirika la mafuta la Serikali la Sonagol wakati wa utawala wa baba yake, Jose Edardo dos santos
Luanda, Angola/AFP.Welwitschia "Tchize" dos Santos, mmoja wa mabinti wa rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo dos Santos na ambaye alikuwa mwanasheria wa chama tawala, amedai kuwa amelazimika kuikimbia nchi yake baada ya kupata vitisho.

"Nilipata vitisho kutoka kwa kiongozi wa kundi la bunge na maofisa wa usalama," anasema Welwitschia katika sauti iliyorekodiwa na kutumwa kwa vyombo vya habari juzi Alhamisi.

"Nilikimbia baada ya kumteka mbunge kwenye ndege" mwezi Januari alisema.

Manuel Antonio Rabelais, waziri wa zamani na mbunge wa chama tawala cha MPLA (People's Movement for the Liberation of Angola), alizuiwa kuondoka nchi hiyo wakati alipokuwa akipanda ndege kwenda Lisbon kutokana na tuhuma za rushwa.
Juzi, MPLA ilipendekeza kumzuia Welwitschia kuingia bungeni baada ya kutoweka nchini Angola kwa siku 90, kwa mujibu wa barua aliyoandikiwa spika baada ya mkutano wa wabunge wa chama hicho.

Welwitschia ni mkosoaji mkubwa wa rais aliyemrithi baba yake, na anaituhumu MPLA kwa kujaribu kumshusha hadhi.
Wakati wa kampeni zake za urais, Lourenco, waziri wa zamani wa ulinzi, aliahidi kutomshughulikia dos Santos.

Kwa sasa Welwitschia yuko Uingereza akiwa na dada yake, Isabel dos Santos, ambaye pia ni binti wa dos Santos na ni mwanamke tajiri kuliko wote barani Afrika.

Isabel amekuwa akipuuza wito kadhaa kutoka kwa wachunguzi nchini Angola wanaochunguza malipo yaliyofanywa wakati binti huyo alipokuwa kiongozi wa kampuni kubwa ya serikali ya mafuta, Sonangol.

Binti huyo anaweza kukamatwa wakati atakaporejea Angola.

Kaka yake, Jose Filomeno dos Santos pia amezuiwa kuondoka Angola na aliwekwa mahabusu kwa miezi sita kutokana na tuhuma za rushwa.

Jose Eduardo dos Santos alikuwa rais wa Angola kwa miaka 38 hadi mwaka 2017.

Chanzo: Mwananchi
 
Kati ya mabint niliokua najua hawatasgughilikiwa ni huyu ila mpaka sasa yupo kinh
 
Nyumba ya vioo halafu unachokoza
Angetulia akala na vipofu
Na tukienda huko Algeria pia kaka wa Rais wa zamani nae yuko ndani ananyea debe

Dunia ya utandawazi uchafu wote hadharani siku hizi na bado wengine
 
Viongozi wote wa afrika wanafanana matendo.

Huyu binti wa santos anashughulikiwa tu kwa sababu ni wapinzani wa serikali iliyoingia madarakani.

Huyo binti angekuwa muimba mapambio wa rais lourenco usingeona anafanyiwa haya.

Ukitaka uendelee kupiga madili na makaburi yako yasifukuliwe hakikisha unafunga mdomo wako na ukitaka uendelee kufaidi vizuri jiunge na kusifu sifu na mapambio fc, hakuna wakukusumbua.
 
sure mkuu mambo yamebadilika watawala wasipojitahidi kutengeneza mazingira mazuri huko gerezani wataishia kulalama kama bashir wa sudan pindi madaraka yatakapoisha
 
Siku naingia madarakani, JIWE na Baraza lake la Mawaziri nitawchinja hadharani pale maeneo ya FERI. huyu RC wa Mjni yeye atasulubiwa kwenye Mbao eneo la SINZA. Spika na Naibu wake wao watapigwa mawe hadharani pale Nyerere Square Dodoma.
 
Ila hapa bongo yuke kijana wa mkuu 'inayesemekana' kila petrol station hapa mjini mpya ilikua yake yuko anadunda tu kitaa na ni mbunge na mama yake akazawadiwa ubunge fresh kabisaa.
......
 
Kutegemea kuwa mrithi wako atakulinda na maovu yako ni kitu hatari sana na ndio maana hawa madikteta wanashawishika kukomalia madarakani.
 
Hii ni furaha kwa wanyonge kwa Rais Dos Santos kushughulikiwa

Alifikiri kutafuta mtu atakayemrithi itakuwa nafuu kwake..

======

pic+binti+rais.jpg

Kwa ufupi
  • Binti huyo alikuwa kiongozi wa shirika la mafuta la Serikali la Sonagol wakati wa utawala wa baba yake, Jose Edardo dos santos
Luanda, Angola/AFP.Welwitschia "Tchize" dos Santos, mmoja wa mabinti wa rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo dos Santos na ambaye alikuwa mwanasheria wa chama tawala, amedai kuwa amelazimika kuikimbia nchi yake baada ya kupata vitisho.

"Nilipata vitisho kutoka kwa kiongozi wa kundi la bunge na maofisa wa usalama," anasema Welwitschia katika sauti iliyorekodiwa na kutumwa kwa vyombo vya habari juzi Alhamisi.

"Nilikimbia baada ya kumteka mbunge kwenye ndege" mwezi Januari alisema.

Manuel Antonio Rabelais, waziri wa zamani na mbunge wa chama tawala cha MPLA (People's Movement for the Liberation of Angola), alizuiwa kuondoka nchi hiyo wakati alipokuwa akipanda ndege kwenda Lisbon kutokana na tuhuma za rushwa.
Juzi, MPLA ilipendekeza kumzuia Welwitschia kuingia bungeni baada ya kutoweka nchini Angola kwa siku 90, kwa mujibu wa barua aliyoandikiwa spika baada ya mkutano wa wabunge wa chama hicho.

Welwitschia ni mkosoaji mkubwa wa rais aliyemrithi baba yake, na anaituhumu MPLA kwa kujaribu kumshusha hadhi.
Wakati wa kampeni zake za urais, Lourenco, waziri wa zamani wa ulinzi, aliahidi kutomshughulikia dos Santos.

Kwa sasa Welwitschia yuko Uingereza akiwa na dada yake, Isabel dos Santos, ambaye pia ni binti wa dos Santos na ni mwanamke tajiri kuliko wote barani Afrika.

Isabel amekuwa akipuuza wito kadhaa kutoka kwa wachunguzi nchini Angola wanaochunguza malipo yaliyofanywa wakati binti huyo alipokuwa kiongozi wa kampuni kubwa ya serikali ya mafuta, Sonangol.

Binti huyo anaweza kukamatwa wakati atakaporejea Angola.

Kaka yake, Jose Filomeno dos Santos pia amezuiwa kuondoka Angola na aliwekwa mahabusu kwa miezi sita kutokana na tuhuma za rushwa.

Jose Eduardo dos Santos alikuwa rais wa Angola kwa miaka 38 hadi mwaka 2017.

Chanzo: Mwananchi
Huyu ni mtoto wa raisi wa chama tawala , na sisi tukianza kuwashika watoto wa wakuu wa waliopita segerea haitatosha, nijibu kama unataka kushughulikia mafisadi au kuwadai ransom money kama mnavyofanya, ukitaka tuanze na yule alijenga kituo cha mwendokasi jangwani au kivuko cha bagamoyo, au majumba ya serikali
 
Hapana

Nashauri kuwe na Tume ya Msamaha na Upatanishi - TAIFA liungane, tusimame

Viongozi warudishe mali na pesa

SWISS irudishe pesa zetu za 10%

Na matajiri waliouziwa mali kwa rushwa waongeze pesa au warudishe
 
Inasemekana rais Dos Santos aliwekwa madarakani na KGB baada ya kushirikiana kumpoteza Dr Augustino Neto. I guess this is pay back
 
Back
Top Bottom