Madigrii ya mawaziri yamtatiza Spika Sitta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madigrii ya mawaziri yamtatiza Spika Sitta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ustaadh, Nov 1, 2009.

 1. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2009
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  [​IMG] Sasa apeleka suala lao kwa Mwanasheria Mkuu
  [​IMG] Asema huko ndiko uamuzi dhidi yao utatolewa
  [​IMG] Athibitisha vyuo walivyosoma havitambuliwi

  Spika wa Bunge, Samuel Sitta, amesema suala la mawaziri sita na wabunge wanne wanaotuhumiwa kuwa na vyeti vya taaluma vyenye mushkeli, atalipeleka serikalini ili likaamuliwe huko, kwa vile vyuo vilikopatikana vyeti vyao vimeonekana kuwa havitambuliki.

  Tuhuma dhidi ya mawaziri na wabunge hao, ziliwasilishwa ofisini kwa Spika na Mwanaharakati, ambaye kitaaluma ni Mwanasheria, Kainerugaba Msemakweli, kwa njia ya barua na viambatanisho, Septemba 15 na 16, mwaka huu.

  Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu kutoka mjini Dodoma jana, Spika Sitta, alisema barua na viambatanisho hivyo viliwasilishwa ofisini kwake, amevisoma na kujiridhisha kwamba, hakuna kosa la jinai, ambalo Bunge linastahili kuchukua hatua dhidi ya wabunge hao.

  Sitta alisema ofisi yake itavipeleka vyeti hivyo serikalini na kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) atajua nini la kufanya.

  “
  Itabidi tulirejeshe serikalini ili waamue huko la kufanya. Kwa sababu vyeti wamepewa, lakini vyuo havitambuliki. Ni tofauti na kughushi kwamba, mtu kaamua kujitengenezea cheti. Ila vinaonekana ni vyeti havitambuliki. Sasa tutalirejesha serikalini wakaonyane wenyewe huko,” alisema Spika Sitta.

  Alikemea kitendo cha mtu kumiliki vyeti vya taaluma, ambayo hakuisomea.
  “
  Sijambo zuri kwa mtu kuwa na vyeti, ambavyo wengine wamesomea,” alisema Spika Sitta.

  “
  Pamoja na hivyo, kibunge, hakuna kitu chochote cha kufanya kosa la jinai. Kiserikali Mwanasheria Mkuu wa Serikali atatizama nini la kufanya.”

  Mawaziri na wabunge hao walihusishwa na kashfa hiyo kufuatia utafiti huru uliofanywa na Msemakweli kwa msaada wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), katika kipindi cha mwaka mmoja na kubaini kwamba wanasiasa hao walitumia vyeti vya kughushi na kuwasilisha katika ofisi za umma kwamba wana elimu hiyo, kitu ambacho si kweli.

  Kwa mujibu wa Msemakweli, utafiti huo ulianza kufanyika Juni 25, mwaka jana hadi Oktoba 9, mwaka huu katika nchi za Marekani, India na Uingereza, ambako vigogo hao wanadaiwa kuwa walisoma na kupata shahada hizo.

  Baada ya kubainika kwamba, hawana sifa za elimu wanazodai kwenye wasifu wa elimu zao, Msemakweli alisema ripoti hiyo ilikabidhiwa kwa Ofisi ya Spika wa Bunge.

  Alisema kitendo cha kuwasilisha nyaraka za hizo katika ofisi ya umma ni kinyume cha Ibara ya 68 na 56 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia, ni kuvunja sheria ya Vyuo Vikuu ya mwaka 2005 (58) na sheria ya makosa ya jinai sura ya 16 (333).

  Msemakweli alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Oktoba 18, mwaka huu na kusema kwamba, alilazimika kufanya utafiti huo baada ya kuingiwa na wasiwasi kuhusu elimu ya vigogo hao.

  Alidai vigogo hao walighushi taaluma kwa baadhi yao kujiwasilisha kuwa wana shahada za masuala ya kimataifa na diplomasia, biashara na utawala, wengine shahada za uzamili, udaktari wa falsafa, na wengine shahada za ualimu nakadhalika, wakati si kweli.

  Msemakweli alisema katika taarifa aliyowasilisha kwa Ofisi ya Spika wa Bunge, aliomba iwawajibishe vigogo hao kwa kashfa hiyo na kwamba, anaendelea na utafiti kwa vigogo wengine tisa na kwamba, atauarifu umma mara tu atakapokamilisha.

  Alidai vigogo hao waliwaghilibu wananchi wa majimbo wanayoyawakilisha na kuwafanya wapate ubunge na kwamba, kwa kutumia shahada hizo za kujipachika, wameweza kuaminiwa na kupewa nafasi za kisiasa na kiutawala.

  Msemakweli alidai ana ushahidi wa kutosha juu ya madai anayoyatoa dhidi ya vigogo hao kwani amefanya utafiti wa uhakika na kwamba, kigogo yeyote atakayehisi kuwa ameonewa aende kwenye vyombo vya sheria na yuko tayari kwenda kuthibitisha madai yake.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hapa naona kitu kimoja tu!

  Jamaa wamesoma, vyeti wamepata lakini vyuo hivyo sio acredited na mamlaka fulani fulani...

  Hilo sio kosa la jinai.
   
 3. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #3
  Nov 1, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawajasoma. Hivyo vyeti vimepritiwa tu kwenye computer.Hakuna kwenda darasani, wala kucollect data na kuanalyse. Hivyo vyuo ni kama kampuni ya Richmond ni za mfukoni.Hata wewe ukitaka tuma pesa tu watakupa pHD or master ukitaka.kwaiyo ni kosa la jinai.
   
 4. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  hawajasoma, hivyo vyeti unalipia wanakupa na wanaweka kwenye recordi zao shuleni
   
 5. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2009
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo nikianzisha chuo changu kisichosajiliwa hapo Manzese kwa mfuga mbwa nikatoa vyeti vitakubalika kwenye mamlaka husika bila kuhoji uhalali wake? Nadhani kutumia vyeti kutoka vyuo visivyotambulika si sahihi na inadumaza usomi.
   
 6. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2009
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Spika wa Bunge, Samuel Sitta, amesema suala la mawaziri sita na wabunge wanne wanaotuhumiwa kuwa na vyeti vya taaluma vyenye mushkeli, atalipeleka serikalini ili likaamuliwe huko, kwa vile vyuo vilikopatikana vyeti vyao vimeonekana kuwa havitambuliki.

  Tuhuma dhidi ya mawaziri na wabunge hao, ziliwasilishwa ofisini kwa Spika na Mwanaharakati, ambaye kitaaluma ni Mwanasheria, Kainerugaba Msemakweli, kwa njia ya barua na viambatanisho, Septemba 15 na 16, mwaka huu.

  Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu kutoka mjini Dodoma jana, Spika Sitta, alisema barua na viambatanisho hivyo viliwasilishwa ofisini kwake, amevisoma na kujiridhisha kwamba, hakuna kosa la jinai, ambalo Bunge linastahili kuchukua hatua dhidi ya wabunge hao.

  Sitta alisema ofisi yake itavipeleka vyeti hivyo serikalini na kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) atajua nini la kufanya.
  “Itabidi tulirejeshe serikalini ili waamue huko la kufanya. Kwa sababu vyeti wamepewa, lakini vyuo havitambuliki. Ni tofauti na kughushi kwamba, mtu kaamua kujitengenezea cheti. Ila vinaonekana ni vyeti havitambuliki. Sasa tutalirejesha serikalini wakaonyane wenyewe huko,” alisema Spika Sitta.

  Alikemea kitendo cha mtu kumiliki vyeti vya taaluma, ambayo hakuisomea.
  “Sijambo zuri kwa mtu kuwa na vyeti, ambavyo wengine wamesomea,” alisema Spika Sitta.

  “Pamoja na hivyo, kibunge, hakuna kitu chochote cha kufanya kosa la jinai. Kiserikali Mwanasheria Mkuu wa Serikali atatizama nini la kufanya.”

  Mawaziri na wabunge hao walihusishwa na kashfa hiyo kufuatia utafiti huru uliofanywa na Msemakweli kwa msaada wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), katika kipindi cha mwaka mmoja na kubaini kwamba wanasiasa hao walitumia vyeti vya kughushi na kuwasilisha katika ofisi za umma kwamba wana elimu hiyo, kitu ambacho si kweli.

  Kwa mujibu wa Msemakweli, utafiti huo ulianza kufanyika Juni 25, mwaka jana hadi Oktoba 9, mwaka huu katika nchi za Marekani, India na Uingereza, ambako vigogo hao wanadaiwa kuwa walisoma na kupata shahada hizo.
  Baada ya kubainika kwamba, hawana sifa za elimu wanazodai kwenye wasifu wa elimu zao, Msemakweli alisema ripoti hiyo ilikabidhiwa kwa Ofisi ya Spika wa Bunge.

  Alisema kitendo cha kuwasilisha nyaraka za hizo katika ofisi ya umma ni kinyume cha Ibara ya 68 na 56 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia, ni kuvunja sheria ya Vyuo Vikuu ya mwaka 2005 (58) na sheria ya makosa ya jinai sura ya 16 (333).

  Msemakweli alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Oktoba 18, mwaka huu na kusema kwamba, alilazimika kufanya utafiti huo baada ya kuingiwa na wasiwasi kuhusu elimu ya vigogo hao.
  Alidai vigogo hao walighushi taaluma kwa baadhi yao kujiwasilisha kuwa wana shahada za masuala ya kimataifa na diplomasia, biashara na utawala, wengine shahada za uzamili, udaktari wa falsafa, na wengine shahada za ualimu nakadhalika, wakati si kweli.

  Msemakweli alisema katika taarifa aliyowasilisha kwa Ofisi ya Spika wa Bunge, aliomba iwawajibishe vigogo hao kwa kashfa hiyo na kwamba, anaendelea na utafiti kwa vigogo wengine tisa na kwamba, atauarifu umma mara tu atakapokamilisha.

  Alidai vigogo hao waliwaghilibu wananchi wa majimbo wanayoyawakilisha na kuwafanya wapate ubunge na kwamba, kwa kutumia shahada hizo za kujipachika, wameweza kuaminiwa na kupewa nafasi za kisiasa na kiutawala.
  Msemakweli alidai ana ushahidi wa kutosha juu ya madai anayoyatoa dhidi ya vigogo hao kwani amefanya utafiti wa uhakika na kwamba, kigogo yeyote atakayehisi kuwa ameonewa aende kwenye vyombo vya sheria na yuko tayari kwenda kuthibitisha madai yake.

  CHANZO: NIPASHE 31/10/2009
  ***********************************************************

  Ndugu zagu,

  Mbona Spika anaongeza maswali zaidi ya maelezo yanayoeleweka?

  1. Kama amejiridhisha kuwa hakuna kosa la jinai kwa nini alipeleke kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali au Mwandishi wa habari hii ndiye kachemka?

  2. Je atakemeaje mtu (sijui nani) kumiliki vyeti vya taaluma, ambayo hakuisomea bila kuona kuwa mtu huyo kweli kafanya kosa? Na anaposema kuwa kibunge hakuna cha kufanya? Je karipio / kemeo la Spika si chochote na haliingii katika rekodi za Bunge tukufu?

  3. Sehemu ya 4 ibara ya 25 ya Kanuni za Bunge Toleo la 2004 inatueleza kuwa kila Mbuge amekula kiapo cha uaminifu akisema yafuatayo:-

  Je, Mbunge kumiliki vyeti vya taaluma, ambayo hakuisomea au visivyotambulika na au kuweka rekodi zake kwa umma wa Watz kuwa ana elimu fulani ambayo hakika hana je huo ni UAMINIFU. Je hajakiuka kanuni ya Bungemaana kiapo ni sehemu ya kanuni za Bunge.

  Je, anailinda na kuitetea vipi katiba ya JMT(1977) ambayo Ibara ya 132:5( c ) inaongelea misingi ya maadili wa viongozi wa umma wakiwamo Wabunge ambapo inapiga marufuku mienendo inayopelekea Kiongozi kuonekana hana UAMINIFU?

  Ni sawa kabisa kulisogeza suala hili kwenye Sheria na hata kwenye Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma lakini si sawa kabisa Spika kusema kuwa Bunge halina cha kufanya (onyo la Spika pekee ni tayari kitu kimefanyika!).
  Aidha hakukuwa na haja ya kujaribu kuona kuwa kosa hilo si la sawa na kughushi na kumalizia kuwa ‘ wao waamuwe huko la kufanya! Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa ufeki wa elimu / vyeti vyao unaozungumzwa si wa aina moja kwa wote.
   
 7. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2009
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nchi ya "kitu kidogo"
   
 8. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2009
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mod samahani hii iunganishe ambapo palikwisha anzishwa thread hii mapema
   
 9. f

  fatakifataki Member

  #9
  Nov 3, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 75
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  inawezekana kwamba madigrii hayo walikoyapata huko yanatamabulika na vyuo na nchi walikoyapatia how comes iwe discusion in tanzania? la haiwezekani kama wametumia rasilimali za watz ambao hawawezi kujikimu ha.ta chembe kwa chakula japo mlo mmoja tu kwa siku.

  mwanakijiji
   
 10. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2009
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  nathkia kidhungudhungu mimi......:rolleyes:
   
 11. O

  Omseza Mkulu Member

  #11
  Nov 3, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ndg Fataki Fataki.
  Karibu jamvini.
  wewe umeingia wiki hii unaafiki mtu kuwa na cheti cha taaluma ambayo hana kwa vile tu unaona vyuo hivyo walikopata vinatambulika? pole naona wewe ni mmoja wapo na umeumia!
   
Loading...