• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Madhumuni ya Chama Cha Mapinduzi Kwa Tanzania ( CCM ) na upotashaji wao kwa wana nchi.

Z

Zero One Two

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2007
Messages
9,381
Points
0
Z

Zero One Two

JF-Expert Member
Joined Sep 16, 2007
9,381 0
Malengo na Madhumuni ya CCM yatakuwa yafuatayo:-
1) Kushinda katika Uchaguzi wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa Tanzania Bara na Zanzibar ili kuunda na kushika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande mmoja na Zanzibar kwa upande wa pili.
2) Kulinda na kudumisha Uhuru wa Nchi yetu na raia wake.
3) Kuhimiza ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea kwa mujibu wa Azimio la Arusha.
4) Kusimamia utekelezaji wa Siasa ya CCM pamoja na kuendeleza fikra za viongozi waasisi wa vyama vya TANU na ASP, kama zilivyofafanuliwa katika maandiko mbali mbali ya Vyama hivyo
5) Kuona kwamba kila mtu anayo haki ya kupata kutoka katika Jamii hifadhi ya maisha yake na mali yake kwa mujibu wa sheria.
6) Kuona kwamba katika Nchi yetu kila mtu aliye na uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi; na kazi maana yake ni shughuli yoyote halali inayompatia mtu riziki yake.
7) Kusimamia haki na maendeleo ya Wakulima, Wafanyakazi na wananchi wengine wenye shughuli halali za kujitegemea; na hasa kuona kwamba kila mtu ana haki ya kupata malipo yanayostahili kutokana na kazi yake.
8) Kuona kwamba kwa kutumia Vikao vilivyowekwa, raia anayo haki ya kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi wa mambo ya Taifa na yanayomhusu, na kwamba anao uhuru wa kutoa mawazo yake, wa kwenda anakotaka, wa kuamini Dini anayotaka na kukutana na watu wengine,maadamu havunji Sheria au Taratibu zilizowekwa.
9) Kuona kwamba Nchi yetu inatawaliwa kwa misingi ya kidemokrasia na ya kijamaa.
10) Kuhifadhi, kukuza na kudumisha imani na moyo wa kimapinduzi miongoni mwa Watanzania pamoja na ushirikiano na wanamapinduzi wenzetu kokote waliko.
11) Kuweka na kudumisha heshima ya binadamu kwa kufuata barabara Kanuni za Tangazo la Dunia la Haki za Binadamu.
12) Kuona kwamba Dola inakuwa Mhimili wa Uchumi wa Taifa.
13) Kuona kwamba Serikali na Vyombo vyote vya Umma vinasaidia kwa vitendo kuanzishwa na kuendeleza shughuli za Ushirika na za ujamaa, na shughuli nyinginezo halali za wananchi za kujitegemea.
14) Kuona kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya Wananchi na hasa jitihada za kuondosha umasikini, Ujinga na Maradhi.
15) Kuona kwamba Serikali na vyombo vyote vya umma vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wanawake na wanaume bila kujali rangi, kabila, Dini, au hali ya mtu.
16) Kuona kwamba katika nchi yetu hakuna aina yoyote ya dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu na/au upendeleo.
17) Kuendelea kupiga vita Ukoloni Mamboleo, Ubeberu na Ubaguzi wa aina yoyote.
18) Kuimarisha uhusiano mwema na Vyama vyote vya Siasa vya Nchi nyingine vyenye itikadi kama ya CCM ambavyo kweli vinapinga Ukoloni, Ukoloni Mamboleo, Ubeberu na Ubaguzi wa aina yoyote.
19) Kushirikiana na Vyama vingine katika Afrika, kwa madhumuni ya kuleta Umoja wa Afrika, na kuona kwamba Serikali inaendeleza na uimarisha ujirani mwema.


# 16: Haipo sawa chuluma inafanyika gamba mwana CCM yote anaebisha aje alikanushe hili.

# 15: Imeshindwa kusimamia usawa kwa wana nchi wake pia, mwanachama anaeona si kweli aje hapa.

#. 14: Mali ya Tanzania imekua ya watu wachache sanaaa, pia ujinga ndani ya Tanzania unakua, Kama inafikia hadi atua ya watoto kufaulu pasipo jua kusoma, afya wasiongee hapa wakae kimya.

#. 12: Dola imekua muhimili wa CCM kuhakikisha inafikia malengo yake na sio uchumi wa taifa

#. 9: nchi wameshindwa kuiweka katika mfumo wa kidemokrasi, ila wanaiga mfumo wa kidemokrasia

#. 7: hakuna haki yoyote wanayo fanyiwa wakulima, walimu na baadhi ya sehemu , JK shaidi

#. 6: kazi wanapata watoto wa vigogo, mtoto wa mlala hoi mnamuambia asilalamike kukosa ajira, akajisajiri bodi ya sijui ya nini ile kwa 50000, huku wakijua tenda wana watu wao wa kuwapa, na Je? Kuhusu mtaji

#. 3: Azimio la Arusha limekua histori.

 
Z

Zero One Two

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2007
Messages
9,381
Points
0
Z

Zero One Two

JF-Expert Member
Joined Sep 16, 2007
9,381 0
Ahadi za hiki chama na mipango yake ni tofauti na utelekezaji wake
 
K

KIRUMO

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2012
Messages
376
Points
195
K

KIRUMO

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2012
376 195
Hayo yalikuwa madhumuni ya CCM ya enzi za mwalimu Nyrere. Saasa madhumuni ni mengine kabisa. Kwa mfano moja ya dhumuni ni kuwa kila aliyeko katika nafasi inayomwezesha, achukue chake mapema. Ndo maana kumekuwepo na mambo ya EPA, Richmond, Mikataba isiyo halali ya madini na rasilimali za taifa kwa mabepari wanaoitwa wawekezaji, Wananchi kunyanganywa ardi yao ya asili na kupewa wageni kwa kisingizio cha uwekezaji, Utoroshaji wa fedha za kigeni na kuzificha Uswiss, Kutorosha wanyama walio hai kwa ndege, meno ya tembo kutoroshwa na kuuzwa nje na mengi unayoweza kuongezea kuthibitisha kuwa madhumuni katika makaratasi na kile ccm inachofanya ni tofauti kabisa. Hiki ni chama cha kuwanyonya wanyonge kwa sasa.
 
P

Precise Pangolin

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2012
Messages
12,481
Points
2,000
P

Precise Pangolin

JF-Expert Member
Joined Jan 4, 2012
12,481 2,000
Madhumuni ya chama cha mabwepande ilikuwa ni kunyonya rasilimali za hii nchi
 
Naibili

Naibili

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Messages
1,677
Points
1,225
Naibili

Naibili

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2011
1,677 1,225
madhumuni ya sasa ni kuhakikisha chaguzi za ccm zinafadhiliwa na fedha zasizo na kazi BOT i.e Epa
kuhakikisha mikutano unajaa kwa kusomba watu na
magari
kuhakikisha kura zinachakachuliwa hata ikiwezekana kwa nguvu i.e segere, shinyanga etc
 
Mungi

Mungi

JF Gold Member
Joined
Sep 23, 2010
Messages
16,981
Points
1,500
Mungi

Mungi

JF Gold Member
Joined Sep 23, 2010
16,981 1,500
Ahadi za ccm zinatekelezeka na wanatekeleza bila ubishi kwenye makaratasi.
Hongera yake Jk mwenyekiti wa chama chetu
 
Ronal Reagan

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
4,834
Points
2,000
Ronal Reagan

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
4,834 2,000
Pamoja na kushindwa vibaya kifalsafa, kisera, kisiasa, kisheria, kijamii, na kimkakati ktk hayo hapo juu (na mengine ktk ilani zao za chaguzi) ....lakini CCM wameendelea kulaghai wananchi ktk baadhi ya maeneo vijijini kuwa wameyatekeleza kwa ufanisi hayo maadishi.

Elimu ni ADUI mkubwa sana wa CCM. Ujinga ni RAFIKI mkubwa sana wa CCM.
 

Forum statistics

Threads 1,404,953
Members 531,857
Posts 34,472,748
Top