dimango
New Member
- Jul 7, 2022
- 3
- 1
Ni siku nyingi mambo ambayo Wazazi wenye Watoto wao wanaosoma katika shule ya SEKONDARI Mnyambe Wilayani Newala wamekuwa wakisikitishwa nayo na si Wazazi pekee bali jamii kwa ujumla haielewi kwanini hali hii imekuwa ikiendelea kwani Wanafunzi wamefanya Kazi za kuchimba msingi, kubeba tofali,kuchimba kisima ambacho nusura kutokee maafa kwa Mwanafunzi mmoja kama suruali yake isingedakwa na kipande kigumu ambacho kilitokeza na Kazi ingine ni kuchota mchanga kwa kutumia mikono ambayo haina kinga yoyote maana kwenye sehemu ambazo Wanafunzi hao wanalazimika kuzoa mchanga huo ni mifereji/ mitaro ambayo inabeba taka mbali mbali ikiwamo Watu kujisaidia humo haja kubwa na ndogo, na humo humo na vitu kama vipande vya bati,vyuma nyembe na kadhalika.
Je hii ni halali? Wanafunzi hao wanakutana na kipigo kikali pindi wanapo kosa kutimiza maagizo hayo kutoka kwa Waalimu wao. Kuna Wazazi kadhaa ambao wameondoa Watoto wao baada ya kupata taarifa za mambo wanayofanyiwa Watoto wao.
Kuna mengi sana ambayo ni tofauti kabisa ambayo yanaendelea pale ambayo Mamlaka husika inapaswa kuangalia bila kuchelewa.