Madhara yawapatayo namba kubwa ya wasomi mitaani

Mtandu jr

New Member
Sep 10, 2021
1
1
Asilimia kubwa ya familia zilizopo Tanzania wazazi na walezi wameweka imani yao katika Elimu na hata kuwaza kwamba pasipo elimu hakuna mafanikio hali hii imeathiri hadi watoto wa wazazi hao na kusababisha wanafunzi kuweka imani yao katika masomo pekee, na kwamba bila kusoma kwa bidii hakuna mafanikio. Sipingani na jamii hizo lakini kuna kitu cha ziada ili kunufaika na vyeti au masomo tuyapatayo sehemu mbalimbali.

Kwa nini wasomi wanaathilika katika jamii?
1. Mabadiliko/maendeleo:- Dunia ina tabia ya kubadilika na asilimia kubwa na wanafunzi wanasoma vitu vilivyo chapishwa kipindi kirefu na hakina uhusiano na tabia hii ya mabadiliko ya dunia hivyo basi wasomi wamekuwa ni watu waathirikao zaidi katika jamii.

2. Udumavu wa vipaji: Asilimia kubwa ya watu waliosoma wanaamini katika vyeti walivyovipata na sio katika vipaji. ukweli ni kwamba watu wanaofahamika zaidi duniani ni watu walioamua kuvitumia vipaji vyao na kuvifanya kuwa biashara yenye kuwaingizia kipato. Tabia ya wasomi kuzika vipaji walivyonavyo inaongeza idadi ya watu wasio na ajira mitaani licha ya kwamba wangeweza kujiajili katika vipaji walivyonavyo.

Ushauri wangu kwa wasomi ili wanufaike zaidi na kuwa matajiri.
1. Usikubali cheti chako kuziba kipaji chako ulicho jaaliwa na mwenyezi Mungu.

2.Katika dunia hii yenye kubadilika huenda ukapewa ajira ya kitu ambacho hukifahamu kiundani, Ushauri wangu kwa wasomi ni kwamba fanya kazi hiyo na utajifunza wakati wa kufanya kazi usiruhusu mdomo wako kusema siwezi bali jifunze kujaribu kila kitu

3. Kwa wanavyuo tumia muda wa angalao masaa mawili au matatu kwa wiki kuwaza kitu chochote uwezacho kifanya tofauti na elimu uisomayo hii itakuwezasha kujiajili na kupanuka zaidi kifikra
 
Hay mambo mkuu graduate wanasemwa sana kuliko mwanamke aliyezaa kwao bila ya kuolewa life imechange sana .Vijana wengi wa mtaa wanatamani graduate siku moja akose ajira wamtolee mfano ila usidanganywe na motivational speaakers assume mtu mpaka anahitimu almost miaka 23 kuna mpaka 30

Aanze upya kitaa unazani ni mchezo ila usilolijua kwamba graduate hususani watu wangu wa karibu naona wanapamabana sana kwa kweli usisome maneno ya mitandaoni na unaona kabisa wana kitu fulani kimeongezeka kichwani hawako lelemama

Wapo wanaanzisha projects mbalimbali ila matatizo ni yale yale wakumbana nayo ishu ni worldwide kikubwa kupeana fursa mbalimbali

Ila wazazi bhana hawaelewi kabisa nishasoma nyuzi watu wanaambiwa watoke kwao wakajitafutie kisa wamesoma sana ila point kubwa umaskini nao unachangia wzazi wanakuwa na over-expectation kwa watoto kwanza elimu wamempatia kweny mazingira magumu hali ya nyumbani ngumu mtoto anapambana inafika stage hana jinsi anarudisha mpira kwa kipa

Na jamii nayo ni ivyo ivyo kuwasema graduates kila kukicha ajira ni very competitive
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom