Madhara yatokanayo na ulaji chips

LOMBOGO

New Member
Oct 13, 2012
2
0
JF Doctor, naomba unifafanulie ni jinsi gani chips inamwathiri mwanaume na madhara hayo ni yapi na solution yake ni ipi?

1470155789986-jpg.375020
 
Ukila sana chips perfomance inakuwa poor sana,goli moja halijai hata kwenye kizibo cha soda
na ukishapiga goli moja chali mpaka asubuhi:majani7:
 
Chips zina mafuta. Na mojawapo ya sehemu mafuta(fats) zinapohifadhiwa ni around the heart.. Pia kutoka m.a..t..a.k.o Ukila saana inasababisha m.a.t.a.k.o kuwa makubwa.. So kama huwezi kuacha kabisa bac kula atleast once per week! Mimi binafc chips kula ni nadra saana.. I can say once per month!
 
Mie nina mwaka tokea niachane nazo,nilihisi perfomance yangu inashuka nikastuliwa kuwa chipsi zinachangia,ila yawezekana kuna ukweli maana tokea niziache niko fiti sana.
 
Hapana, chips kama chips hazina shida hizo. Shida ni hizo chill sauce na tomato sauce mnazonyunyiza juu yake ndo huleta upungufu wa nguvu za kufanya kazi, huwa mnasoma vibandiko vya hizo chill sauce na tomato sauce mkajuwa ni vitu gani vinatumika kuzihifadhi zisiharibike?. Kula chips na kachumbari nzuri na ya kutosha ni kinga pia kwa magonjwa kadhaa.
 
Chips kinga? Viazi vilivyokaangwa?kweli kuna kirutubisho hapo? Hyo kachumbari ndo itakuwa inavirutubisho if kama itakuwa imeandaliwa vzuri,la sivyo inaweza ikakusababishia minyoo..
 
Nasikia chips yai ni invention ya kibongo, kuna wageni hukishangaa alafu wanajifunza wanaenda ringishia makwao, wanasema piza ya yai mixture viazi, dah ila kitamu sana aisee, ukipata yule anajua pika fresh walahi kama hujala siku mingi upo katika risk ya kujing'ata.
 
Zama zinabadilika kila uchao...

Zamani wazee wetu walikuwa wanakula mtama umechanganywa na ulezi, hio ikapita.

Wakaja wakoloni wakaleta muhogo toka Amerika ya Kusini, mtama na ulezi vikapunguza umaarufu, wazee wetu waliwashangaa sana watu wa kizazi chao kwa kukumbatia muhogo na kuacha mtama na ulezi wakasahau kuwa hata wao waliacha kula mizizi na matunda wakakumbatia mtama na ulezi.

Baadaye yakaingia mahindi kutokea huko huko kwa mkoloni, watu wakaacha muhogo wakachangamkia mahindi, wazee wa wakati huo wakawashangaa sana kwa nini kuacha muhogo kukumbatia mahindi "vyakula vya watu weupe visivyo na faida mwilini"??.

Baadaye ukaingia mchele, wazee wanaokula mahindi wanawashangaa sana wanaoukumbatia mchele kwa kuwa ni "chakula cha kuja".

Sasa ulaji wa chipsi unaingia kwa kasi kama vile ambavyo vingine viliingia kwa kasi na watu wakashangaa pia kwa nini watu kukumbatia "mavyakula ya wazungu".

Ni zama tu zinabadilika mkuu, baadaye tutaingia kwenye ngano na mavyakula ya makopo na watu watapuzia chipsi pia.

Madaktari wamejikita kueleza madhara ya chipsi badala ya kutueleza na faida zake pia, haya ni madhaifu makubwa sana katika kuleta judgement ya kitu, huwezi kusikia one sided story peke yake.

Zama mpya zinakuja, za zamani zinapotea, lakini all in al hakuja jipya chini ya jua.

Vijana kuleni kiepe yai, kwa kuwa hizi ni zama zenu.
 
Hii kitu ni noma unakula daily lakini hauchoki, bei nzuri. Tatizo tunazidi kunenepa!
 
Chipsi yai hata Europe hawajui chips yani na chakula kiku cha South America Aswa Nicaragua ...Guatamara kidogo Paragwai hao mdio mlo wao mkuu Bongo ilianza kuingia hiyo Style kwenye miaka ya 1980 baada ya watanzani wengi wakati ule walikua wana ludi kwenye Ubaharia ndio ilianza Dar na Tanga pale Majestic na mbowe Dar na kuanza kuenea mitaani lakini nyuma ya hapo Wa TZ.walikua hawajui CHIPIS YAI...iliku viazi kwenye mchuzi na nyama na wakati huo viazi hakua na Soko kama sasaivi kila mji TZ wanajua CHIPS YAI
 
Back
Top Bottom