Madhara yatokanayo na matumizi ya mirungi katika mwili wa mwadamu

kiwenini

Member
Nov 25, 2018
73
43
1544515739225.png


Mirungiu ni mmea ambao una majina mengi kulingana na eneo husika ambao unatumika , mfano wapo wanaita gomba, miraa, mirungi na majina mengine kama hayo. Ulaji wa mirungi ulianzia Ethiopia, ukaenea hadi nchi za Afrika Mashariki, Yemen, Zimbabwe, Zambia, Malawi na hata Afrika kusini.

Mirungi ilionekana kuwa ni moja ya madawa ya kulevya hivyo ikakatangazwa na umoja wa mataifa UN na kupigwa marufuku mwaka 1971 kwasababu ya ufanano wa kemikali iitwayo amphetamine.

Yafuatayo ndiyo madhara ya kutumia mirungi.
Mtumiaji wa mirungi yupo katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo.

Kupungukiwa msukumo wa kufanya tendo la ndoa (low sex drive) na pia kuwahi kumaliza haraka na kutoweza kudumu kwenye tendo la ndoa kwa muda mrefu.

Ukosefu wa haja kubwa (constipation) .

Utumiaji wa muda mrefu husababisha ini kushindwa kufanya kazi,pia meno kubadilika rangi, kudhoofika,fizi kuuma na harufu mbaya mdomoni .

Upungufu wa usingizi.

Humpelekea mlaji kutawaliwa nayo (addiction).

Madhara ambayo bado kinamama walaji Mirungi hawajagundua ni kwamba mtoto anayezaliwa na mama mlaji Mirungi mara nyingi hukataa kunyonya titi la mama yake kwa sababu ladha ya maziwa inabadilika kwa ajili ya utumiaji wa madawa (pesticides) unaotumiwa na wakulima wa Mirungikama inavyoeleza utafiti uliofanyika na Chuo Kikuu Cha Aden (Aden University).

Utafiti mwengine kule Ethiopia unatueleza ya kuwa mtoto wa mama mwenye kula Mirungi kwa wingi huwa hana uzito wa kawaida wakati wa kuzaliwa.


Hivyo kila wakati epuka sana kutumia mirungi kwani si salama kabisa katika afya.
 
Nimechanja gomba kidogo miaka ya 2013/2014 nishaacha

Niliambiwa vile vichembechembe vyake vikiingia mwilini hukimbilia kwenye njia ya mkojo nakusababisha matatizo
Nikaacha. Asante Mwenyez mungu niliacha maana gomba lina stimu na andasi za kufa raia(but haimaanishi ujaribu na ww unaesoma hapa)





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom