Madhara ya Usimba na Uyanga yameigharimu timu ya Taifa Stars

libeva

JF-Expert Member
Mar 25, 2015
4,367
3,382
Zile tetesi kwamba kuna chuki za kocha wa Taifa Stars dhidi ya kuuvaa mkenge wa Usimba na Uyanga leo umedhihirika baada ya timu aliyoiteua kutofua dafu kwa Taifa dogo la Rwanda na kutoka suruhu Kocha inabidi ajitathimini kama hii CHAN inahusu wachezaji wa ndani kwa nini hawasiliniani na makocha wa timu zingine zinazoshiriki ligi kuu ili achague the best player akaachana na huu Usimba na Uyanga leo unamchafua kwamba timu ya Taifa haijafanya vizuri kwa sababu ya mapenzi binafsi ya kocha.
 
Zile tetesi kwamba kuna chuki za kocha wa Taifa Stars dhidi ya kuuvaa mkenge wa Usimba na Uyanga leo umedhihirika baada ya timu aliyoiteua kutofua dafu kwa Taifa dogo la Rwanda na kutoka sruhu Kocha inabidi ajitathimini kama hii CHAN inahusu wachezaji wa ndani kwa nini hawasiliniani na makocha wa timu zingine zinazoshiriki ligi kuu ili achague the best prayer akaachana na huu Usimba na Uyanga leo unamchafua kwamba timu ya Taifa haijafanya vizuri kwa sababu ya mapenzi binafsi ya kocha.

Kabisa ayce....

Tena ukiwaita vijana wadogo ndo watafanya vizuri kuliko hawa mastar

Makocha wanaangalia simba na yanga tu....
 
Soka la Tanzania huwa linaudhi na linakera, hivi timu ya taifa ni lazima iundwe na yanga na simba tu?

sent from tekno ya shilingi elfu saba na mia tano.
 
Soka la bongo halieleweki...usipoweka wachezaji wa Simba Yanga au Azam bado watu watalalamika...Muarobaini wa hili tatizo sijui ni lipi
 
Tulishatolewa tangu mechi ya kwanza Mwanza, ni kosa kubwa sana kuruhusu adui apate goli mechi ya ugenini kwake then mkarudiane kwao na kwako ametoka moja moja, heri ingekuwa Bila Bila, hata hivyo kupata suluhu Rwanda kwetu ni ushindi japo hauna faida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuacheni utani hivi Ajib kaichezea lini Yanga hata iwe ni mechi ya kirafiki? Ajib huyu alipokuwa Simba si ndiyo yule alikuwa anawekwa benchi?

Inawezekana Mayanga ana damu ya kunguni au anaponzwa na jina lake la MAYANGA.Lakini ukiangalia sehemu kubwa ya first eleven ya Yanga ni wageni hali kadhalika kwa Simba pia. Unamlaumu vipi kocha hapo?

Tukubali mpira wetu upo chini na unachezwa kwenye magazeti tu sisi ni vibonde haswaa wa soka.

Kule South Africa michuano ya COSAFA kilichotusaidia nchi nyingi zilileta aidha vikosi vya pili au timu za vijana.

Hebu fikiria wakati michuano ya COSAFA ikiendelea nchi hizo hizo vilabu vyake vilikuwa vinashiriki aidha michuano ya ligi ya kikombe cha shirikisho la CAF na ligi ya klabu bingwa Africa (CAF Champions League).
 
Ajibu hajawahi ichezea Yanga hata hao kina BoKo na Manula bado hawajaichezea simba. Hapa lawama zianzie TFF kwa kuzibeba timu hizi mbili hata ligi kuwa ni ya simba na Yanga. Lawama hawazikwepi maana kila siku huwa tunapinga maamzi ya marefa watanzania kulalia timu ndogo. Kama matimu hayatapendelewa tutawapata wachezaji wenye uchungu na Nchi yao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom