Madhara ya Spika na/au Naibu kuwa Mteule wa Rais sasa yanaonekana

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,319
72,747
Sio siri tena kuwa Dr. Tulia aliteuliwa na Dr. Magufuli awe Mbunge kwa lengo la kupata nafasi ya Unaibu Spika baada ya mpango wake wa kugombea Uspika kuonekana kugonga mwamba.

Aliyemshinikiza Rais Magufuli kuwa Dr. Tulia ana weledi wa kuweza kuwa Naibu Spika hatumjui lakini ni wazi alimdanganya au Tulia mwenyewe ndiye amejisahau na kudhani kwa vile cheo hicho kapigiwa chapuo na Rais basi Spika sio chochote wala wabunge hawana cha kumfanya.

Ni wazi analivuruga bunge na litavurugika hasa. Haelewani na uongozi wa Bunge kwa kukurupuka kwake, na ana haribu mahusiano ya serikali na wabunge wa pande zote kwa kudhani anaiokoa serikali ya mteule wake.

Amesaidia kuweka wazi kuwa mteule wa Rais hapaswi kuongoza muhimili unaoisimamia serikali. Njia sahihi kabla mambo hayajaharibika kabisa ni yeye kujiuzulu.
 
Mwenye tatizo kubwa nadhani ni wabunge wenyewe wa CCM, kwa kutumia wingi wao bila hekima serikali ya CCM imefanikiwa kuwayumbisha na kuwafanya bendera fuata upepo, ni aghalabu mbunge wa CCM kutumia akili kwa hoja inayoletwa na serikali ya chama chake.

Kabla ya kuletewa dk Tulia ni uzoefu gani aliokuwa nao katika kuendesha bunge? Kuna wenyeviti wa bunge wenye uzoefu, hekima na staha. Hajawahi kukaa bungeni kwa maana ya kuwa mbunge, ni dhahiri ameletwa kwa kazi maalum nayo ni kulisimamia bunge lisiisimamie serikali, na kwa sababu Ndugai uwezo wake mdogo kazi hiyo imefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90.

Kweli ni aghalabu kitu kizuri kikatoka CCM
 
Sio siri tena kuwa Dr Tulia aliteuliwa na Dr Magufuli awe Mbunge kwa lengo la kupata nafasi ya Unaibu Spika baada ya mpango wake wa kugombea Uspika kuonekana kugonga mwamba.
Aliyemshinikiza Rais Magufuli kuwa Dr Tulia ana weledi wa kuweza kuwa Naibu Spika hatumjui lakini ni wazi alimdanganya au Tulia mwenyewe ndiye amejisahau na kudhani kwa vile cheo hicho kapigiwa chapuo na Rais basi Spika sio chochote wala wabunge hawana cha kumfanya.

Sikupendi kwa unafiki wako kuhusu Lowasa. Lakini kwa roho nyeupe naunga mkono hoja yako hii, bunge la sasa linatumika na Serikali.
 
Sio siri tena kuwa Dr Tulia aliteuliwa na Dr Magufuli awe Mbunge kwa lengo la kupata nafasi ya Unaibu Spika baada ya mpango wake wa kugombea Uspika kuonekana kugonga mwamba.
Aliyemshinikiza Rais Magufuli kuwa Dr Tulia ana weledi wa kuweza kuwa Naibu Spika hatumjui lakini ni wazi alimdanganya au Tulia mwenyewe ndiye amejisahau na kudhani kwa vile cheo hicho kapigiwa chapuo na Rais basi Spika sio chochote wala wabunge hawana cha kumfanya.
Ni wazi analivuruga bunge na litavurugika hasa. Haelewani na uongozi wa Bunge kwa kukurupuka kwake, na ana haribu mahusiano ya serikali na wabunge wa pande zote kwa kudhani anaiokoa serikali ya mteule wake.
Amesaidia kuweka wazi kuwa mteule wa Rais hapaswi kuongoza muhimili unaoisimamia serikali. Njia sahihi kabla mambo hayajaharibika kabisa ni yeye kujiuzulu.

Huyu alikuwa naibu mwanasheria mkuu wa serikali kwa hiyo hajui kazi nyingine zaidi ya kuitetea serikali. Pia inaonekana hajiamini na ana inferiority complex = kwamba akikubaliana na hoja za upinzani wabunge wa ccm watamdharau, kumbe ndipo angejipatia sifa kutoka kwa wananchi kwa kutopendelea upande wowote. Kama yupo humu asome anavyojadiliwa na ajirekebishe na aache kiburi kwani sisi wananchi tunachohitaji ni mijadala na hoja makini kwa ukweli na uwazi.
 
Mwenye tatizo kubwa nadhani ni wabunge wenyewe wa CCM, kwa kutumia wingi wao bila hekima serikali ya CCM imefanikiwa kuwayumbisha na kuwafanya bendera fuata upepo, ni aghalabu mbunge wa CCM kutumia akili kwa hoja inayoletwa na serikali ya chama chake.

Kabla ya kuletewa dk Tulia ni uzoefu gani aliokuwa nao katika kuendesha bunge? Kuna wenyeviti wa bunge wenye uzoefu, hekima na staha. Hajawahi kukaa bungeni kwa maana ya kuwa mbunge, ni dhahiri ameletwa kwa kazi maalum nayo ni kulisimamia bunge lisiisimamie serikali, na kwa sababu Ndugai uwezo wake mdogo kazi hiyo imefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90.

Kweli ni aghalabu kitu kizuri kikatoka CCM
Unajua Maana Ya Aghalabu? Maana Yake Ni Mara Nyingi Iwezekanavyo
 
Atoke bado mapema manake anampunguzia sifa aliyemteua,Elimu yake isiwe kigezo cha kuharibu Bunge
Hapo hakuna elimu, maana elimu kubwa mara nyingi inaendana na maarifa na busara kubwa hivyohivyo. Huenda alipata elimu hiyo kwa kukariri tu. Kuongoza Bunge lenye watu wenye tofauti ya mawazo na mtizamo unahitaji Busara zaidi ya Ubabe.

Lakini si kila kitu kinatakiwa ubishi. Suala la watoto wa chuo kuondolewa bila mpangilio ni suala linalohitaji kujadiliwa kwa dharura, kilichofanywa na huyu binti/mama naibu spika hakikubaliki kabisa. Kama mambo yakipelekwa hivyo, maana ya Bunge itakuwa ni nini?
 
Sikupendi kwa unafiki wako kuhusu Lowasa. Lakini kwa roho nyeupe naunga mkono hoja yako hii.....bunge la sasa linatumika na Serikali.
Sawa mkuu, naona hata Jana wabunge wa ccm wameamua kuonyesha kile wanachokiamini. Sasa huo waweza kuwa mwanzo mbaya kwa serikali kama itaendelea kutegemea uungwaji mkono hata pale inapopotoka.
Jana lilikuwa jambo dogo tuu la kutumia hekima
 
NAKUBALIANA NA WANAJAMVI WANAOSEMA WALIOKOSEA NI WABUNGE WA CCM KTK UCHAGUZI HUU WA NAIBU, NILIKIONA KICHWA CHA MAMA MMOJA WA UKAWA NI MZURI NA MZOEFU LKN KILICHOTOKEA.....
 
itatuchukua miaka 100 mbele kufikia utawala bora, hakika nawaambia. PARTY SUPREMACY IS THE BIGEST PROBLEM IN THIS COUNTRY, THEY WANT TO MAINTAIN PARTY SUPREMACY AND THEIR STATUS QUO
 
Huyu dada anaharibu bunge kwa kujiamulia anachotaka...hata bunge nalo linaonyesha udhaifu mkubwa sana kupitia kamati zake
 
Back
Top Bottom