Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

Nikuishiwa na maji kwan hutumika kupunguza sukari mwilini. Kwa chaziada alafu unaweza kusema nn madhara zaid mwenyewe fanya hivi chukua kipande cha mfupa kiweke kwenye glasi/bilauri kisha weka coca wacha kwa saa 48 utaona mabadiliko, kwan mfupa unaweza kupungua ukubwa au kupotea wenyewe. FAIDA: koka unaweza kutumia kusafisha masinki na vitu vye asili hiyo
 
KUNA mjadala mkali unaendelea kuhusu vinywaji baridi hususani soda, baada ya utafiti wa hivi karibuni kuonyesha kuwa soda inaweza kuwa na madhara zaidi kiafya kuliko hata sigara!

Hii inaweza kuwa changamoto nyingine kubwa kumkabili binadamu katika masuala ya afya, kwani makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji baridi yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo yake bila kutaja madhara ya vinywaji vyao.

Soda inahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa watoto na watu wazima, yakiwemo matatizo ya kuongezeka unene kupita kiasi (obesity), ugonjwa wa ini (liver disease) na hata tabia za vurugu (violent behavior). Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, unywaji wa vinywaji baridi mara kwa mara unachangia tabia ya ugomvi kwa asilimia kati 9-15!

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa nchini Marekani, soda huwekwa ‘fructose’ (sukari) nyingi ikiwa katika mfumo wa sirapu (fructose corn syrup) ambayo inaongoza kwa kusababisha magonjwa ya unene, kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine sugu yanayowakabili Wamarekani wengi hivi sasa na dunia kwa ujumla.

Dk. Mercola, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya lishe asilia na tiba mbadala anasema: ” Ninaposema kunywa soda ni hatari sawa na mtu anayevuta sigara au pengine zaidi, siyo jambo la kutia chumvi, bali ndiyo ukweli halisi”.

Dk. anaendelea kusema kuwa unywaji wa soda kwa njia nyingi ni mbaya kuliko uvutaji wa sigara, ila kutokana na kampeni kubwa ya matangazo inayofanywa na makampuni haya, inafanya vinywaji hivi vyenye sukari kuonekana havina madhara kwa watu wasio na hatia, hasa watoto wetu!

SABABU KUBWA YA KUDHARAU SODA

Unayesoma makala haya kuhusu madhara ya soda kwa mara ya kwanza bila shaka utakuwa unashangaa na kujiuliza; soda ina ubaya gani? Kwa mujibu wa Dk. Mercola, hakuna sababu yoyote ya kuendelea kunywa soda, labda ujikute uko katikati ya jangwa na hakuna kinywaji kingine isipokua soda!

Kiafya, unywaji wa soda au vinywaji vingine baridi vyenye ‘fructose’ una madhara. Unywaji wa kiasi cha kopo moja tu la soda kila siku, utakuongezea uzito wa mwili wa kilo 10 kila mwaka na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari (diabetes) kwa asilimia 85!

‘FRUCTOSE’
‘Fructose’ ni kirutubisho kilichomo ndani ya sukari na kiwango kinachowekwa wakati wa utengenezaji wa soda ni kingi kuliko kawaida. Inaelezwa kuwa miaka 100 iliyopita, Mmarekani mmoja alikuwa akitumia kiasi cha gramu 15 ya sukari (fructose) kwa siku, tena kwa kula matunda. Miaka 100 baadaye, (yaani hivi sasa), robo ya Wamarekani wote wanatumia kiasi cha gramu 135 (kutoka 15) kwa siku, tena kwa kunywa soda!

Ulaji wa sukari (fructose) kiasi cha gramu 15 kwa siku hauna madhara kiafya, labda uwe na ugonjwa wa kisukari (high uric acid levels). Hata hivyo, kwa kula sukari mara kumi zaidi ya kiwango cha gramu 15 kinachokubalika kiafya, inakuwa ndiyo chanzo cha unene wa kupindukia na magonjwa mengine hatari yanayoibuka mwilini (degenerative diseases).

Utafiti unaonesha kuwa vinywaji vingi baridi vina sukari nyingi kuliko wastani unaotakiwa. Badala ya kuwa na asilimia 55 ya ‘fructose’ na asilimia 45 ya ‘glucose’, vingi vina asilimia 65 ya ‘fructose’, ikiwa ni karibu asilimia 20 zaidi na inavyotakiwa.

Utafiti zaidi umeonesha kuwa ‘fructose’ ndiyo chanzo kikubwa cha tatizo la ugonjwa wa ini kwa watoto wengi nchini Marekani, ingawa hawatumii kilevi chochote (alcohol). Inaelezwa kuwa ‘fructose’ huleta madhara kwenye ini kama inavyofanya pombe.

Me ndio maana huwa nawashauri watu kunywa BIERE kwa afya zao,kwenye BIERE kuna mambo mazuri sana (1)tunaongeza damu(2)tunakutana na watu mbali mbali na kupeana michakato ya kimaisha mbali mbali nk nk nk..........
 
Nipe ushahidi wa kisayansi kuonyesha kuwa Beer inaongeza damu. Bila shaka wewe ni mmoja wa wale wanaodanganywa kuwa ukinywa bia unaongeza damu.
 
Me ndio maana huwa nawashauri watu kunywa BIERE kwa afya zao,kwenye BIERE kuna mambo mazuri sana (1)tunaongeza damu(2)tunakutana na watu mbali mbali na kupeana michakato ya kimaisha mbali mbali nk nk nk..........

aisee mie naogopa kutembea kwa miguu minne bawana. Ila hii kitu soda nilishaisikiaga long time kitambo, sema ilikuwa kwa coca cola, sikujua kwamba ni kwa soda zote. na kuna tetesi kwamba mgunduzi wa soda mwenyewe aliipiga marufuku familia yake kunywa hii maneno kwa sababu ya hatari inazoambatana nazo
 
kwa hiyo hunywi kabisa? Nifanyeje ili niache? Niliambiwa konyagi inasaidia ku loose weight, kumbe si lolote, nimenenepa zaidi sasa nina 83 kg, jamani! Halafu kuiacha imekuwa taabu
 
Ww unanenepa shauri ya kupendwa,lol!
Hiyo ya konyagi kusaidia kupungua sio kweli manake inashawishi kutokula kwa balance. Nyamachoma and stuff.
kwa hiyo hunywi kabisa? Nifanyeje ili niache? Niliambiwa konyagi inasaidia ku loose weight, kumbe si lolote, nimenenepa zaidi sasa nina 83 kg, jamani! Halafu kuiacha imekuwa taabu
 
Back
Top Bottom