Madhara Ya Simu za Mchina, Kenya Uganda zazipiga Marufuku. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madhara Ya Simu za Mchina, Kenya Uganda zazipiga Marufuku.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by mgt software, Sep 11, 2012.

 1. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,725
  Likes Received: 1,631
  Trophy Points: 280
  Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa simu nyingi za kichina hazina viwango vya FCC , hivyo kwa kuwa nyingi hutengenezwa kupitia viwanda vidogo vidogo huingizwa nchini kwa njia ya magendo.
  Utafiti huu unaweza kudhibitika kwa yafutayo.

  1. Simu nyingi hazina majina halisi, nyingi zina chip inaitwa MTK, Spedrum, Infineon ambazo ni chip nyepesi sana ambazo hazihimili kiwango cha umeme kwa siku nyingi, ndio maana simu nyingi uganda wakati wa kuwaka. Utakuta simu inaitwa nokla, simsungu ipone ilimladi tu iweze kushaabiana na original.

  2. Simu hivi zina madini hatari sana ambayo yanaitwa li-ione ambayo yanatengeneza muwako ambao unaweza kuunguza au kutumika kutengeneza mabomu. Madini hayo huwekwa kwenye betery ya kichina ambazo sio imara kwani zimetengenezwa kwa kuzungushia karatasi nyepesi.

  3. Viwango vya spika sio sahii kwani vinaweza kumfanya mtu awe kiziwi akitumia simu hizi kwa muda mrefu.

  4. kwa kuwa simu nyingi zina vioo vya taachi, au shika shika vioo hivi hualibika mara kwa mara hivyo mafundi wengi wanaotumia dawa ya kubandua kioo na kubandika huungua mfumo wa uvutaji hewa kwani dawa hii (soldering Paste)mafuta haya yanasumu kali.

  5. Utafiti unaonyesha Tanzania inatumia kiasi kikubwa cha fedha za kigeni kuagiza bidhaa mbovu za simu, ambazo hudumu muda mfupi.

  6. Simu hizi zimeongeza mianya ya rushwa upande wa TRA na TBS kwani ndio wanaoruhusu bidhaa hii mbofu mbofu.

  7. Imekatisha tamaa makampuni makubwa yanayolipa kodi kama vile Sansung, Nokia, Siemens, Iphone ,Sony Ericsson kwani simu nyingi zimeigwa kwa kutumia ujuzi wa kampuni hizi.

  8. Mafundi walipa kodi na wenye vipaji wameanza kupotea kwani kazi hii imeonekana kudhaulikwa, kwa kuwa ukitengeneza simu hizi unatengeneza ugomvi na wateja wako kwani kila siku matatizo hayaishi.

  9. Zimu hizi zinaongeza wizi wa mitandao kwa kuwa nyingi zina chip ambazo hazitambuliki kimataifa hivyo kuziingiza kwenye mtandao wa kudhibiti vyombo hivi kuwa mgumu, kwani no. zinazotambulika ni MSID na ICCID au PIN au product Code No.

  Namalizia kwa kusema basi kama hatuwezi tuige mfano wa Kenya na Uganda wamezipiga marufuku
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,688
  Likes Received: 82,553
  Trophy Points: 280
  ...TBS wamechapa usingizi na kuziacha bidhaa mbali mbali zisizo na viwango vya kimataifa zikiingia nchini kwa idadi kubwa.
   
 3. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  Kenye wamezifunga zote kuanzia 1st September na wanasema Uganda zinafungwa 1st November, sijasikia tamko lolote kutoka hapa kwetu! Hivi vigezo ulivyoelezea hapa juu ya madhara inawezekana ni kweli ndizo zimepelekea hawa wenzetu kufanya hivyo mbali na sababu za kibiashara!
  http://www.monitor.co.ug/artsculture/Reviews/+Made+In+China++does+not+necessarily+mean+fake/-/691232/1503526/-/iusyse/-/index.html

  Review01pix.gif
   
 4. m

  makeda JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Lingekua jambo zuri km hilo lingewezekana.lakini kwa nnavoijua shamba la bibi,inaweza ikawa too late,labda hata wanaotengeneza wameshafunga na mashine zao majumbani,hivyo wanazisukia hapahapa.
  Anywy ngoja tbs waje,labda watatuelezea vizuri.
   
 5. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,725
  Likes Received: 1,631
  Trophy Points: 280
  mpaka ninavyoandika sasa hivi maduka mengi yamejaa vio vibovu, haosingi mbovu, hata speaker za masikioni zina waya nyembamba ambazo kikijinyonga mara hansini hakuna mawasiliano. Vitu hivi vinatengezwa majumbani mwa watu hata ambao sio wachina. Utakuta nyingine zina majina yao. Jamani TBS TRA kuweni wazalendo muokoe mfumuko wa bei. Unapoingiza simu za million 400 zikapita bila ushuru unategemea nini?
   
 6. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,725
  Likes Received: 1,631
  Trophy Points: 280
  Kashfa betri bandia za simu Kariakoo yawagusa vigogo

  Mary Victoria

  Toleo la 231
  21 Mar 2012


  [​IMG]


  • Waziri wa Biashara afichua maovu Tume ya Ushindani
  • Mambo mazito, Bosi wa Tume adaiwa kuandika barua ya kujiuzulu

  WIZARA ya Viwanda na Biashara imeingia katika mvutano na Tume ya Ushindani wa Bidhaa, kuhusu usimamizi wa sheria ya alama za bidhaa, mgogoro ambao msingi wake ni baadhi ya maduka yanayotuhumiwa kuuza betri bandia za simu eneo la Kariakoo Dar es Salaam, kufungiwa na tume hiyo na kisha wizara kuamuru yafunguliwe.
  Mvutano huo unahusisha pia wamiliki wa Kampuni ya Bright Pacific Ltd ya Dar es Salaam, ambao Desemba 2, mwaka 2011, waliwasilisha malalamiko yao Tume ya Ushindani. Katika malalamiko yao, wanadai bidhaa zao, betri za simu za mkononi zenye nembo ya executive zilikuwa zikihujumiwa kwa kuuzwa zikiwa bandia na baadhi ya wafanyabiashara Kariakoo na kwa hiyo, tume iingilie kati suala hilo.
   
 7. Penguin-1

  Penguin-1 JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 400
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kuna kitu kinaitwa "interference"...
  Imegundulika kuwa kutokana na kutotengenezwa kwenye standards zinazokubalika..simu hizi huchangia sana kuleta muingiliano wa mawimbo na kusababisha hata mawasiliano kupotea katika eneo flan....
   
 8. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,738
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Zikipigwa marufuku Kenya na Uganda, zitauzwa Tanzania kama mtumba. Mafuta yalipigwa marufuku Rwanda na Congo DRC bali yakakubalika Tanzania.
  Simu zote zilizo chini ya kiwango huko Kenya na Uganda zitakusanywa na kuletwa kwenye 'soko huria' Tanzania; nchi hii ni shimo kla taka. Hii inatishia uingizwaji wa bidhaa halisi hapa chini.
   
 9. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,109
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  haya January makamba amebaki kupiga domo wakati wizara yake ndio inahusika tunajua mmeshindwa kusimamia makampuni ya simu kulipa kodi lakini hata afya zetu zinazotoka na simu zisizo na viwango
   
Loading...