Madhara ya Serikali ya Mseto

Labda ni maneno tu ndio yanatofautiana maana lakini kitu ni kile kile.

Zanzibar wanaunda serikali ya mseto kwa mantiki ya kuwa, viongozi wa mihimili ya serikali wanatokana na vyama tofauti.

Lakini huu mseto wa samia, una lengo la kuwaleta watu wa vyama tofauti kuwa watendaji wa serikalini.

Kuna tofauti kati ya "viongozi" na "watendaji" katika serikali.

Mseto wa zanzibar ni viongozi, lakini mseto wa Tanzania ni watendaji.

Mfano mzuri ni Anna Mghwira RC wa Kilimanjaro.
Akifanyà hivyo atapata upinzani mkubwa roka chama chake kule Zanzibar inawezekana sababu ni takwa la kikatiba na nguvu za kisiasa hazipishani
 
Nimeona wapinzani wetu wanamshangilia Rais Samia kuwaalika waingie Serikalini.

Bila shaka, Mama atawateua wale wapinzani wenye majina makubwa kwa malengo fulani ya kisiasa, pamoja na kuunda umoja wa kitaifa kama anavyodai.

Wasiwasi wangu ni kuwa, hawa wapinzani sijui kama wanajielewa.

Sijui kama wanaelewa madhara ya mfupa wanaotupiwa wautafune.

Wale wawindaji wanafahamu jinsi ya kumpoteza fisi anayekukimbiza. Unamtupia fupa ahangaike nalo wakati wewe unatokomea.

Wapinzani watakapojiloga kupokea hizo nafasi, kwanza watakuwa wameua vyama vyao kwa sababu hawawezi kufanya tena siasa za kipinzani wakiwa serikalini.

Pili, Mama Samia atakuwa amefanikiwa vizuri kutumia kanuni ya "divide and rule".

Wapinzani na wafuasi wao wataparaganyika huku na kule na hawatakua wanaelewa waunge mkono juhudi za serikali ya mseto ama waendeleza siasa zao za kipinzani.

Mama atakuwa amefanikiwa kuiua demokrasia kwa njia tulivu na ya kisayansi, tofauti na mtangulizi wake aliyewashugulikia wapinzani waziwazi.
Mkuu kuna tofauti kati ya serikali ya mseto na maamuzi ya Rais kushirikisha/kuteua upinzani kwenye utendaji. Lakini pamoja na utofauti huo bado ni turufu nzuri zaidi kwa upinzani kama mtu atakuwa mzalendo yaani kufanya kazi kwa maslahi mapana ya taifa, ila tatizo la nchi zetu viongozi wetu wote wapo kimaslahi yao binafsi. Na hapo ndio mama atakapo rubuni wapinzani kwa njia za busara, utapewa nafasi ili uonje kwanza halafu ndio linakuja sharti la kwamba kama una taka kubaki kwenye hiyo nafasi toka huko jiunge upande huu ama baki kwenye chama chako na hiyo nafasi tumpe mwingine mwenye shida nayo.
 
Uwepo wa vyama vingi una umuhimu zaidi kwa taifa kuliko kushirikishwa moja kwa moja kwenye serikali.
Intelijensia ya kimataifa inaonesha kwamba vyama mbadala husaidia taifa kuuma na kupuliza mataifa mengine.
Kwa mfano serikali ya CCM iliwahi kuingia mikataba ya hovyo ambayo siyo rahisi kuivunja.
Kinaingia chama kingine kinavunja na baadaye CCM ikirudi inawabembeleza walalamikaji kwa makubaliano mapya yenye unafuu.
 
Nimeona wapinzani wetu wanamshangilia Rais Samia kuwaalika waingie Serikalini.

Bila shaka, Mama atawateua wale wapinzani wenye majina makubwa kwa malengo fulani ya kisiasa, pamoja na kuunda umoja wa kitaifa kama anavyodai.

Wasiwasi wangu ni kuwa, hawa wapinzani sijui kama wanajielewa.

Sijui kama wanaelewa madhara ya mfupa wanaotupiwa wautafune.

Wale wawindaji wanafahamu jinsi ya kumpoteza fisi anayekukimbiza. Unamtupia fupa ahangaike nalo wakati wewe unatokomea.

Wapinzani watakapojiloga kupokea hizo nafasi, kwanza watakuwa wameua vyama vyao kwa sababu hawawezi kufanya tena siasa za kipinzani wakiwa serikalini.

Pili, Mama Samia atakuwa amefanikiwa vizuri kutumia kanuni ya "divide and rule".

Wapinzani na wafuasi wao wataparaganyika huku na kule na hawatakua wanaelewa waunge mkono juhudi za serikali ya mseto ama waendeleza siasa zao za kipinzani.

Mama atakuwa amefanikiwa kuiua demokrasia kwa njia tulivu na ya kisayansi, tofauti na mtangulizi wake aliyewashugulikia wapinzani waziwazi.
Chief nimekuelewa. Ila kunakijimkwamo Fulani hivi kinacholitesa taifa. Kinatokana na uchaguzi uliopita. Hivi unadhani kwanini Ndugai anawang'ang'ania covid 19. Ngoja tusubiri tuone
 
Hahahaa.... yaaniii....

Mimi siku zote nina mashaka na hawa wanaoitwa wapinzani. Hawaelewi nini wanachotaka.

Hakuna Mtanzania mwenye “monopoly” ya upinzani. Bila shaka unaongelea CHADEMA hapa. Basi ni bora uwataje wao kabisa na uijue misimamo yao rasmi wala isiwe kusoma kauli za manazi hapa JF.

In any case, “upinzani” na “wapinzani” is too general. Sidhani kama bandiko lako linawahusu vyama kama UDP, NCCR, ACT, n.k.
 
we umeelewaje?
 
Back
Top Bottom