Madhara ya rais kuteua wanasheria wengi kwenye bunge la katiba

Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
14,210
13,724
Ingawa inasemekana kinadharia kuwa Rais ndio anayeteua wabunge watakaoingia kwenye bunge la katiba ukweli ni kwamba mawaziri wawili wa sheria [ wa sasa na aliyeanzisha mchakato] ndio watakaokuwa wahusika wakuu wa kuchambua majina ya waliopendekezwa. Hawa wawili wote ni wanasheria na ingawa kuna mwongozo wa jinsi ya kuteua kufuatana na makundi lakini nachelea kuwa watakaochaguliwa wengi watakuwa na background ya sheria kwani kuna dhana potofu kuwa wanasheria ndio watunga katiba!!!

Ikumbukwe kuwa katika Katiba kuna mambo mengi yanayohusu ustawi wa jamii kwa ujumla wake ; itakuwa busara basi kama wanataaluma wengine kama vile wachumi wakapata nafasi ya kuwa kwenye hilo bunge ili waweze kutoa mchango wao kwenye maeneo yanayohusu taaluma zao. Bunge letu la sasa halina wachumi wengi na waliobobea kiasi cha kuamini kuwa watasaidia katika kuboresha rasimu ya katiba ;uhaba huo unajidhihilisha na uteuzi wa mawaziri uliofanywa hivi karibuni kuongoza wizara ya fedha na mipango!!
 
Mleta mada samahani sijaona madhara yoyote ambayo umeyadadadvua ili tujadili mada kwa kina. Kwa mtazamo wangu naona umeonyesha hisia zikiwa zinapambwa na wasi wasi badala ya kuchambua madhara. Aidha unajichanganya zaidi pale unapo kiri kuwepo kwa mwongozo wa uteuzi.
 
Mkuu Bulesi

Umetanabaisha jambo la msingi kabisa. Nikweli kabisa kuwa katiba kamwe haiwezi kutungwa na watu toka kada ya taaluma moja pekee, na hii si kwa katiba tu bali pia kwa sheria na kanuni karibia zote. Kwa mfano wanasheria pale ofisi ya AG ama LSRP peke yao hawawezi kujifungia na kutunga sheria ya mawasiliano pasipo kuwahusisha wadau wa sekta husika ya mawasiliano. Utungwaji wa sheria nyingi huusisha wadau wa sekta husika pamoja na bunge ambalo ukiacha kuwa ni chombo cha uwakilishi pia hujumuisha mseto wa watu wenye taaluma tofauti.

Nadhani sisi tumeanza vema katika mchakato huu hasa katika uundwaji wa ile tume ya Jaji Warioba, ukiacha kuwa ilikuwa na wanasheria waliobobea kama Prof. Kabudi, Dk. Mvungi na Advocate Said el Maamry bado kulikuwa na uwiano mzuri wa wajumbe kutoka taaluma mbalimbali. Hakika ulikuwa ni mseto bora kabisa.

Ni ukweli usiopingika ukiwaweka wanasheria pekee kusimamia mchakato kama huu wa katiba hatari kubwa iliyopo ni kupata katiba isiyotekelezeka. Lakini pia bado kuna uwezekano mdogo wa kupata wanasheria wengi katika bunge la katiba kupindukia idadi ya wajumbe wote. Kwa wajumbe tu tulionao sasa toka bunge la JMT na Baraza la Wawakilishi hilo haliwezekani.

Halafu mbona unawesemea wachumi pekee kama ndiyo taaluma inayohitajika sana katika mchakato huu? Hili si sahihi kabisa maana katiba ni mseto wa mambo mengi katika jamii hivyo inahitaji uwiano sawa wa wajumbe toka kila taaluma, rika, jinsia na hata sekta. Lakini mkuu hata hili la wachumi unaweza kweli kutilia shaka uwezo wa kitaaluma wa mtu kama Prof. Tibaijuka ama Dk. Kigoda na hata Dk. Cyril Chami?
 
Last edited by a moderator:
East to west, soouh to north of the world, wanasheria make the best of politicians
 
Nia yangu hasa ilikuwa kuonesha umuhimu wa taaluma nyingine mbali na wanasheria kujumuishwa kwenye hilo bunge la katiba; wachumi ilikuwa ni mfano tu!! Hao wakina Tibaijuka, Kigoda na Chami sina imani nao kwani wakishaingia huko ccm akili zao huwa hazifanyikazi kama utendaji wao kwenye wizara wanazoongoza/walizowahi kuongoza ulivyodhihilisha!! Moreover, wameishakuwa ccm zealots without any independent thinking kwasababu ya njaa!!!Kikwete is leading them by the nose.
 
Back
Top Bottom