Madhara ya Mume na Mke kufanya kazi ofisi moja...!

Museven

JF-Expert Member
Aug 22, 2011
629
447
Habari za majukumu waungwana wa JF? Naomba busara zenu kuhusu athari za kimahusiano zinazowezekana kujitokeza iwapo mume na mke au mtu na mpenzi wake wanafanya kazi sehemu moja. Mfano, wote ni walimu wanaofundisha shule moja au wote ni wahudumu wa afya wanaofanya kazi kituo kimoja. Nawasilisha!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
tatizo litakuja pale mtakapogombana nyumbani,ndani ya gari kwenda kazini kila mmoja kamnunia mwenzie,kasheshe itakuja ofisini kama mko kitengo kimoja na inabidi mfanye group discussion,hapo sasa mama ana crack a joke meza nzima inacheka we mzee mzima unauchuna,wenzio watakucheki na hawatakumaliza,hahahahahaha....
 
Kama ni watu mnaoelewa maana ya kazi, na mna ufahamu wa idea ya conflict resolution, na mnajua kuweka mipaka kati ya mambo ya nyumbani na kazini, wala hii haina shida!
Kwa wengine hii inakuwa ni advantageous zaidi, maana kwa namna fulani wanabebana!
Ila kama kuna mmoja anapenda dogodogo mhhhh!, lazima siku moja kutatokea kituko ofisini!
 
mhhhhhhhhhhh.....na ukisikia uzushi mkeo kapitiwa na boss wa headoffice????
 
Sio kitu complicated sana kufanya kazi ofisi moja ila inahitaji matured partners, vinginevyo sehemu zote mbili zinaweza pasikalike neither nyumbani nor ofisini, but kwa partners wenye communication nzuri wanaweza kabisa kufanya kazi sehemu moja
 
sidhani kama inaleta maana sana ... kwani kuna mambo mengi sana yanaweza kutokea kama
  1. magomvi ya nyumbani kuhamia ofisini
  2. kutokuelewana na wafanyakazi wenzako kwa wivu hii inatokana na historia ya mtu uliyenaye karibu
  3. historia yenu kabla ya ndoa itakuwa inawahukumu
  4. utendaji wa kazi utashuka kama mko mapenzin hasa mtataka kuwa karibu muda mwingi
 
Kwa masilahi ya ndoa na ofici pia haifai kbs,tukubaliane na ukweli hata km mko matured kiasi gani ubinadamu unabaki pale pale, so its better kuwa ofic tofauti na kukutana hm au kupitiana kwa ajili ya usafiri.
 
Habari za majukumu waungwana wa JF? Naomba busara zenu kuhusu athari za kimahusiano zinazowezekana kujitokeza iwapo mume na mke au mtu na mpenzi wake wanafanya kazi sehemu moja. Mfano, wote ni walimu wanaofundisha shule moja au wote ni wahudumu wa afya wanaofanya kazi kituo kimoja. Nawasilisha!

Kwenye uchumi/uwekezaji kuna concept ya 'diversification' (kwa lugha nyepesi usiweke mayai yako yote kwenye kikapu kimoja). Labda kwa ajira za serikalini (ambazo zipo relatively stable) lakini kwenye sector binafsi kuna makampuni kufilisika, kufa, kupunguza wafanyakazi(redundacy) nk hivyo kama nyote mpo sehemu moja risk inakuwa kubwa zaidi. Waajili wengi pia hawapendelei kuajili watu wa namna hiyo......mkifiwa/mtoto anaumwa/etc...nyote wawili hamji kazini na hivyo kwa mwajiri ni hasara kubwa zaidi.

Lakini hata katika mahusiano pia kuna changamoto zake, inabidi muwe wavumilivu/waelewa kweli. Naona wengine wamezitaja hapo juu.
 
Kwa kweli hii kitu ni ngumu sana italeta ugumu na kusababisha kushuka kwa ufanisi
 
wanaume wanapenda kufanya kazi ofisi moja na hawara zao siyo na wake zao. hata kwenye gari mtu akiwa na mke wake utajua tu manake kila mmoja anatazama upande wake, hakuna kuongea wala kutazamana.
 
kuna bosi wangu mmoja alikuwa anafanya kazi na mke wake kabla mke hajaamishwa..basi ilikuwa ukiingia kwa ofisini kwa bosi yule mama kiroho juu,ukitoka haongei na wewe na ugomvi usioisha kwa staff wa kike..basi ikatokea siku yule mama akaumwa,utaratibu kama unaumwa ni kuja ofisini au kumtuma mtu alete ed kwa bosi..basu ikabidi yule mama atoke home na mumewe then akabidhi id...in short ilibidi yule mama ahamishwe tawi jingine
 
....dah,hiyo hali ni mashaka sana!!me naona sio poa kivile japo mkiwa watu wakuelewa sio tatizo pia
 
Hiyo haifai kabisa kah!! hasa kama mwanamke ni bosi halafu mwanaume ni mfanyakazi wa kawaida, ubosi atataka aupeleke hadi nyumbani!
 
wapo wengi tu hata sie tunao sasa omba wasowe dept ile yenye kuwa na access na pc za watu atasoma weeee mpaka!
mi naona mkipatana kuoana mmoja a give up ila kazi ili muweze kuheshimiana na kupeana nafasi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom