Madhara ya msaada wa Millenium

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
947
Soko la hisa linazidi kudidimia, tulidharau ule msaada wa millenium wa dola trillion1 za kimarekani kwa ukaidi wa serikali ya awamu hii haya ndio madhara yake,msaada huo ulikuwa na mchango mkubwa sana kwenye bajeti ya Tanzania.

Naumia kusikia taifa langu linadaiwa deni kubwa sana, na badala ya kuandaa mikakati maalumu ya kulipa deni hili ndio linazidi kuwa kubwa. Serikali isikatae misaada kwa sasa au kukopa kwa sasa hatuna namna na kama haitaki kukopa basi ilibidi iandae mikakati maalumu ambayo haitokuwa na hasara kama ilivyo sasa.

Kila kukicha uchumi wetu unadolola, huku vyanzo vya ndani vikidai uchumi wetu unakua. ila ukifuatilia kiundani ripoti za IMF zinasema uchumi wetu unashuka kwa sera mbovu za uchumi.

Gharama ya maisha inazidi kupanda, nae raisi wetu akisema ni raisi wa wanyonge, wafabiashara wadogo wakilia kodi kuwa kubwa na TRA wanasema wamekusanya pesa nyingi katika kipindi hiki cha miaka miwili ya Mhe. Raisi.

Usalama wa taifa na wananchi upo lehani, kweli tutawavutia wawekezaji wa nje waje kuwekeza nchini? usalama upo kwa watu wachache, maendeleo yanaletwa na usalama wa nchi. Hakuna mwekezaji anaweza kuwekeza katika taifa la watekaji kama hili.

Uchumi wetu unashushwa na vitu vingi sana ikiwemo utawala wa sasa, ukosefu wa usalama nchini, sera mbovu za uchumi..
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Back
Top Bottom