Madhara ya michoro mwilini (Tattoo)

kwann mwenye tatoo haruhusiwi kuchangia damu hata kama atapimwa na ataonekana hana ugonjwa wowote

Kuna magonjwa inachukua hata mwaka hadi kuanza kuonekana. Tattoo si kitu kizuri, vifaa wanavyotumia sehemu nyingi havioshwi vizuri watu wanaishia kuambukizana magonjwa tu, kumbuka machine ya kuchora tattoo imegusa damu ya kila mtu aliyeitumia.
 
Acha kupotosha chale ndio tattoo na Mungu hapendi huo ujinga na amekwisha weka tahadhari

Hata uandike vipi kwa akili/hekima za kibinadamu ila ni kinyume na Mungu pamoja na kuwa zilitumiwa enzi na enzi haikupi uhalali wa kujichora leo wewe uliyepewa maarifa zaidi ya wale

Acha kumuingiza Mungu kwenye mijadala ambayo hamuhushi yeye. Mungu hapendi vitu vingi hata hiyo simu unayotumia kuchat Mungu hapndi kwa maana humo kwenye simu kuna mauchafu yako kibao tu.

So zifanye fikra zako ziwe pana
"Kwa maana yeye alishatupa Nguvu na akili za kutawala Dunia"
 

" jambo lolote lenye kumuhusu binadamu na ukakuta wanadamu wanajadili gafla akatokea mtu akaingia Nguvu za Mungu, basi hapo ndio ukomo wa binadamu kufikiri"

Sasa ndugu hapa tunajadili masuala ya Tattoo kwa mitazamo ya kawaida na sio ya Kishirikina. Unaposema chale maana yake unaingiza mambo mengine hasa ya Uchawi.

Kuna tofauti za kimatumizi na dhamira kati ya Tattoo na Chale.
Usichanganye mambo[/QUOTE]Soma vzuri.. Uelewe.... Sio chale tu. Mzeee hata alama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili la tattoo nilishasema acha dhambi nipate tu, It took me about two (2) damn years kufikiria maamuzi yangu ya kuchora tattoo, finally nimechora tattoo yangu ya kwanza ambayo ina maana kubwa sanaa kwenye maisha yangu, si urembo wala ubishoo. Sijutii kabisa na sitojutia na kama tunapata dhambi kwa uasherati, ulevi, fitina na usengenyaji, hii la tattoo ni dhambi kama hizo tu. Only God can Judge me.
 
Kwa mtu wa Tanzania kutofahamu Tattoo ni kitu gani, ni kitu cha Kawaida sana .Kwa maana Tattoo wengi tunaziona kwa Watu maarufu ambao wengi wana maisha ya ajabu ajabu kama ya ha Wakina Irene

Lakini mtoa mada na wadau wengine nataka kukwambia kuwa Tattoo ni kitu muhimu sana kwa jamii tena za kiafrika kwani Tattoo ilikuwepo hata kabla ya Ukoloni.

Na Tattoo wakati huo hazikupakwa kama sehemu ya Urembo hapana, na haikuwa kwa ajili ya Watu maarufu pia.

Wakat huo tattoo ilikuwa ni kwa jamii nzima na ilikuwa ni sehemu ya Utamaduni. Kupitia Tattoo watu waliweza kuwasiliana na kupeana Utambulisho kwa mfano Kabila la Wamakonde

Lakini pia ukija huko Amerika hasa kwa Hao Watu weusi Tattoo zilikuwa sehemu ya Harakati za Ukombozi. Kwani ilikuwa kazi ngumu kusimama hadharani na kudai uhuru mbele ya Watu weupe uko Amerika.

Hivyo kupitia Tattoo watu walijichora na kuwalilisha Ujumbe kadri wawezavyo bila watu wengine kujua.

Hivyo ni asilimia kubwa sana ukiwa USA ukikutana na Watu wamechor tattoo watakwambia sababu za kuchora, na sababu zao zinafungamana na historia halisi ya maisha aidha ya mtu mmoja au ya jamii nzima. Na ndio maana huko unakuta mtu kachora Tattoo ya Rosa Park.

Lakini huku kwetu kwa kuwa tunaiga kupitia Video na kuona tu Wanawake wanaovaa vichupi na wanaume ambao ni Wasanii. Hudhani kuwa Tattoo ni kitu cha Starehe na hivyo ni kinyume na Dini zetu wa hapa Afrika.

Hapo hapo kuna mtu ambaye pengine yeye ni Mwislamu bado haelewi Tattoo ni kitu gani wakati huo huo kuna Wanamke kavaa ijabu na bado kapaka Ina. Ambayo kimsingi ni michiro ile ile na rangi ni zile zile. Na ina dhamira sawa na waliochora Tattoo.

️Hoja zangu hizi zinasimama kwa watu wanaoamini kuwa Tattoo ni Dhambi na wale wanadhani Tattoo ni Uhuni pia. Kwani kuna Watu wana Tattoo za Yesu, nao tunawaweka kwenye kundi gani??

Dhambi ya tattoo ni ipi? Kile ulichochora au tabia zako baada ya kuchora?

Leo hii Lil Wayne wa Cash Money akija Tanzania na kutaka kutoa ufadhiri wa ujenzi wa kanisa, kuna watu watamkataza kisa ana Tattoo mwilini?

Ni kweli kuna madhara yake lakini jamii pia lazima ifahami Tattoo ni kitu gani na sio tu kuwa majibu ya Kidini dini bila kujua historia kamili.
View attachment 1322625
vipi kuhusu kuvaa hereni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana nakwambia kuwa tulio wengi hapa Tanzania hatufahamu mengi juu ya Tattoo na wengi huchora tu bila kuwa na sababu.

Ukikutana na Mdada wa Buza huko ukamuuliza sababu ya Tattoo yake utakupq jibu la jumla kuwa urembo tu.

Japo wapo wachache watakwambia sababu za wao kuchora.

Mimi ni mwalimu nafundisha shule fulani katika nchi fulani hapa barani Afrika. Ni mwalimu wa Historia na hapa shuleni nafundisha Mada za Black American History pamoja na Pure African History. Mwilini mwangu nina Tattoo Nane.

1. Ramani ya Afrika
2. Mwalimu nyerere
3. Olauda Equano
4. King Haile S.
5. Nelson Mandera
6. Neno la Ubuntu
7. Rosa Park
8. Neno history

So ndugu natamani nikueleze mengi kuhusu Tattoo lets me end here.
mzee mimi pia napenda sana black history.nahitaji tuungane katika kushare documentaries na vitabu vya kusoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili la tattoo nilishasema acha dhambi nipate tu, It took me about two (2) damn years kufikiria maamuzi yangu ya kuchora tattoo, finally nimechora tattoo yangu ya kwanza ambayo ina maana kubwa sanaa kwenye maisha yangu, si urembo wala ubishoo. Sijutii kabisa na sitojutia na kama tunapata dhambi kwa uasherati, ulevi, fitina na usengenyaji, hii la tattoo ni dhambi kama hizo tu. Only God can Judge me.
umeichorea bongo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili la tattoo nilishasema acha dhambi nipate tu, It took me about two (2) damn years kufikiria maamuzi yangu ya kuchora tattoo, finally nimechora tattoo yangu ya kwanza ambayo ina maana kubwa sanaa kwenye maisha yangu, si urembo wala ubishoo. Sijutii kabisa na sitojutia na kama tunapata dhambi kwa uasherati, ulevi, fitina na usengenyaji, hii la tattoo ni dhambi kama hizo tu. Only God can Judge me.
Hata dhambi ya uasherari, ulevi nk watu hujutia mkuu.. tunza comment yangu muda unakuja lazima utajutia kuchora tatoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom