Madhara ya kuweka dawa za kuongeza hamu ya ngono ukeni, hatarini kupata saratani ya shingo ya kizazi

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
344
1,326
Wanawake wameshauriwa kuacha mara moja kuweka dawa za kuongeza hamu ya ngono ambazo hazijapimwa na wataalamu katika sehemu zao za siri, kwa kuwa wako katika hatari kubwa ya kupata saratani ya shingo ya kizazi ambayo ni tatizo kubwa kwa wanawake wengi nchini.

Amezungumza hayo Mtaalamu na Mshauri Mwandamizi mwenye uzoefu wa Afya ya Umma, Jinsia na Maendeleo ya jamii, Dkt. Katanta Simwanza alipokuwa katika semina ya HIV/AIDS na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Tanzania Standard Limited (TSN) jijini Dar es Salaam.

Dkt. Simwanza amesema kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2021 kutoka katika kituo cha Saratani Ocean Road, aina ya magonjwa ya saratani yanayowapata wanawake wengi ni pamoja na saratani ya shingo ya kizazi (43%), Saratani ya matiti (14.2%) na Saratani ya koo (3.8%).

"Kuna hatari kubwa ya wanawake kuambukizwa Saratani ya shingo ya kizazi kutokana na sababu kama vile utumiaji wa dawa za kusisimua mwili ambazo hazijapimwa, ngono zisizo salama, kushiriki tendo la ndoa mapema na kujamiiana na wanaume wasiotahiriwa, amesema.

Hata hivyo ameongeza kuwa kuna ongezeko la kesi za wanawake kutumia virutubisho mbalimbali kama potasiamu ili kuongeza hamu ya ngono na kubainisha kuwa miongoni mwa hatari nyinginezo ni kuondolewa kwa harufu ya asili ukeni, maambukizi ya njia ya uzazi na kuongeza hatari ya unyanyasaji wa kijinsia.

Vagina.jpg

Source: SwahiliTimes
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom