Madhara ya kiafya yatokanayo na dawa za nywele (Relaxer)

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Relaxer ni dawa ya nywele inayofanya nywele za mtu mwenye ngozi nyeusi wa asili ya Afrika zilainike na kunyooka kama nywele za wazungu, waasia au waarabu, watu wengi hasa wanawake wanapenda kutumia relaxer ili nywele zao ziwe na mwonekano tofauti.

Kihistoria matumizi ya relaxer yalianza kama matokeo ya watu weusi kubaguliwa, watu weusi walipoona hivyo waliamua kuiga maisha ya kizungu ili kufanana fanana na wazungu kwa rangi ya ngozi na nywele ili wathaminiwe na kupewa upendeleo wa kupata fursa za mafanikio na watawala wetu enzi za ukoloni.

Sayansi inaonyesha kuwa matumizi ya relaxer za nywele yanaweza kusababisha au kuongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo, kupungua kwa uwezo wa kiakili katika kufikiri na kupambanua mambo, kuungua kwa ngozi ya kichwa na muwasho wa ngozi.

Matatizo mengine ni saratani ya matiti, mabonge katika mji wa mimba (Leiomyomata), upungufu wa kinga ya mwili na kubalehe mapema kwa wasichana.

Katika utafiti uliofanywa na wanasayansi Lauren A. Wise na wenzake (Wise et al, 2012: Hair Relaxer Use and Risk of Uterine Leiomyomata in African-American Women) na kuchapishwa katika jarida la American Journal of Epidemiology (2012) vol. 175(5):432-440, ilibainika kuwa matumizi ya relaxer yanaongeza hatari ya kupata mabonge katika mfuko wa kizazi.

Mabonge yanaweza kusababisha ugumba hasa pale yanapokuwa makubwa na kulazimisha tiba ya upasuaji ya kuondoa kizazi (hysterectomy). Katika jamii za wanawake wanaotumia relaxer kwa kiwango kikubwa, chanzo kikubwa cha upasuaji wa kuondoa mfuko wa uzazi ni mabonge. Inasemekana kuwa katika nchi ya Marekani wanawake weusi wanakabiliwa na tatizo la mabonge mara mbili hadi mara tatu zaidi ya wanawake wengine. Hii inaweza kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na matumizi makubwa ya vipodozi kama relaxer.

Viambato vilivyomo ndani ya dawa hii hupenya na kuingia katika mfumo wa damu na kwenda kuvuruga mfumo wa vichocheo vya ujinsia hasa homoni za kike. Relaxer nyingi za nywele zina kiwango kikubwa cha kemikali kama vile lye (Sodium hydroxide au Caustic soda), calcium hydroxide, guanidine carbonate, thioglycolic acid salts na monobutyl phthalate.

Chanzo: Hivi Sasa
 
Best hair styles kwangu mie
dbdb33a54e863af082070f9fa75dfec8.jpg
images (20).jpg
 
mwanamke aniwekee dread au anyoe hapo tutaelewana. hayo mengine madawa mkiwa kitandani utadhani mpo maabara ya kemikali mimi hapana.
 
Dah..ngoja nimtumie hii link mtu mmoja mbishi sana. Kuweka dawa nywele ili zifanane na wazungu ni aina kichaa kabisaa! Ni matokeo ya kutojiamini ambayo humsababisha mwenye tatizo hilo ajione km hajakamilika bila kujifananisha na wengine.

Tatizo hilo huwa haliishi hapo,ukishapata hicho kichaa hutaishia kwenye nywele tu,utataka kubadili kila kitu.
 
Nimeanza kuelewa kwa nini kila hospitali ninayokwenda wagonjwa asilimia kubwa ni akina mama.
 
Utumiaji huu wa nywele Mi naona ni kutijiamini kwa mwanamke mwenyewe utakuta mtu anweka manywele bandia tena kwa gundi kwenye kichwa yake hivi unategemea nini
 
Mwanamke ni kiumbe mwenye roho ngumu sana.
Yani ukifikiria anabond nywele kwa magundi na najihisi comfortable kabisa.
Anabandika mikucha na gundi anajifeel comfortable.
anajpaka yale ma makeup sawa tu nakujipaka unga anajifeel comfortable.
anabandika nyusi kwenye jicho yani sehemu delicate kama hiyo anajifeel comfortable.
Anaweka contact lens kubadili muonekan wa macho bado yuko comfortable...
Bado avae mchuchumio siku nzima mgongo sijui hamuumi...
Kweli hiki kiume siyo cha kisport sport
 
u
Utumiaji huu wa nywele Mi naona ni kutijiamini kwa mwanamke mwenyewe utakuta mtu anweka manywele bandia tena kwa gundi kwenye kichwa yake hivi unategemea nini
umesahau pia anazishika au anatikisa kichwa ili zikae vizuri kama watasha:D:D:D
 
Dah..ngoja nimtumie hii link mtu mmoja mbishi sana. Kuweka dawa nywele ili zifanane na wazungu ni aina kichaa kabisaa! Ni matokeo ya kutojiamini ambayo humsababisha mwenye tatizo hilo ajione km hajakamilika bila kujifananisha na wengine.

Tatizo hilo huwa haliishi hapo,ukishapata hicho kichaa hutaishia kwenye nywele tu,utataka kubadili kila kitu.
Kuna na wale ambao wakimuona mtu ni mweupe wanasema ana pesa yule au ameng'aa sababu ana hela
 
Back
Top Bottom