Madhara ya Kamari zinaoendelea: Serikali isithamini tu kodi, angalieni kwa jicho la pili!

Mambo ya Mungu

Senior Member
May 6, 2019
106
93
Hakuna ataye kuwa salama kwenye hili na matokeo mtayashudia mkiwa bado mnapumua. Kamali zimekuwanyingi katka awamu hii ya utawala na imekuwa halali eti kwa kuwa wwanakula kodi yao lakini je mmejua kwa undani mnatengeneza Taifa la namna gani?

Kuna kamali za mitandaoni ambazo zimekuwa kero kwetu watumiaji wa simu yaan hadi usiku wa manane ni sms tu. Ila ipo hii mbaya zaidi maarufu kama dubwi au mashine ya mchina.

Hii imewasomba watu wa rika na jinsia zote licha ya kuwekwa masharti ya umri. Mi nionavyo yamkini baada ya miaka michache kwanza hela utakuwa adimu sana nchini kwakuwa pesa nyingi zinabebwa na mchina.

Ila mbili ni kuharibu nguvu kazi ya Taifa kwani watu wengi wanashinda kwenye kamali badala ya kuumiza kichwa afanye nini licha ya tatizo la ajira kuongezeka.

Nimeshuhudia hadi watoto wadogo wanacheza tena kwa wingi akipewa 200 ya kula shule anaipeleka akajaribu bahati akipata anawavuta na wengine wengi.

Ukweli: serikali mnasema haina dini ila hakuna kiongozi wa serikali asiye na dini falsafa yetu ina laana ndani yake huwezi kuwa serious kiongozi wa shetani kisha ukaenda mbinguni.

Mi najua kuwa maslahi ya mwanasiasa ni yeye kwanza sasa vipi nyinyi viongoz wetu hamna maslahi na roho zenu. Hivihizi nyumba za ibada tunazoingia ni fasheni tu au huwa tunafakari kuingia na kutoka kwetu?

Ushauri: Japo sio lazima kuupokea kamali ni dhambi na ni kuharibu nguvu kazi ya Taifa. Muisaidie jamii ipate historia nzuri ya utawala wenu.

Sitaki kunukuu maandiko mtasema nawahukumu Ila mjue kila atendae dhambi ni mtumwa wa hiyo dhambi na kwake kwa milele ni ziwa likalo moto. Mbadilike na mbadilishe falsafa zenye laana ili msiongoze taasisi zenye laana.

Hizo pesa,vyeo na majumba na magari ya kifahari kila kitu vitabaki mtaondoka na roho zenu. Vyeo na nafasi mlizonazo zisiwafanye mjisahau kuwa ninyi ni wanadamu na ipo siku mtasimama mbele ya hukumu.
 
Yaani mkuu uko sawa kabisa
Tena serikali inatakiwa ifanye kitu kuhusu haya makorokoro ya mchina before its too late
Maana saiv yamesambazwa kila mahali na wanaoingia humo kutoka ni ngumu.
 
mwanaume huchezi kamali..sawa siyo issue

ila issue ni pale hata mwanaume mwenzio akicheza unamind
 
mwanaume huchezi kamali..sawa siyo issue
ila issue ni pale hata mwanaume mwenzio akicheza unamind
Mkuu mi sikuonei wivu kucheza Ila madhara yake kweli labda kama huna mtoto anaekuwa lakini kama unae pia hujyaajua kama hii ni kikwazo kwa malezi mazuri maana hutaenda nae kila mahali, atajiingiza huko na kupoteza mwelekeo kabisa. Na vp kuhusu pesa yetu kusombwa kwa pesa au unadhn ile hela wanyokusanya wataizungusha hapa nchini?
 
Back
Top Bottom