Madhara ya Dawa na kemikali za kichina mtaani

sinajinasasa

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
2,287
2,000
Kumekuwa na biashara holela ya Dawa za kuuwa mende, mbu na wadudu wengineo. Hizi dawa hazijaandikwa ingredients za kilichomo ndani ya kemikali hizo.

Zinauzwa hovyo mtaani. Dawa nyingi na kemiikali lazima ziandikwe side effects kama tunavyoandikiwa kwenye drugs za binadamu, kila sehemu zimesambaa hadi dawa za meno za kichina, hatujui madhara yake ni nini ukizidisha, mbona dawa za meno zinazotengenezwa kama colgate huandikwa hadi vilivyomo ndani nikimaanisha element au compounds zilizomo humo.

Za kichina hazina hata chembe ya taarifa, mamlaka husika ipo, sijui kama ni TFDA ndo inahusika, mmelala usingizi wa pono au mmehongwa nyie, nchi inakuwa kama haina mamlaka zinazohusika? Au na ninyi mna agenda ya siri ya watu wadhurike?

Mbona TBS hukamata vitu visivyo na ubora na kuviteketeza, ila vitu vinavyogusa maisha ya binadamu mnajifanya hamna habari, bulshit!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom