Mhabarishaji
JF-Expert Member
- Oct 5, 2010
- 1,006
- 598
Chama legelege chenye "sera" ya kulindana, kinachoogopa kuwafukuza wanachama wake wenye utovu wa nidhamu, kwa "kuogopa Chama kusambaratika", kitazaa vilevile serikali inayoogopa kuwafukuza watumishi wa serikali wenye utovu wa nidhamu, na kuwalinda tu au kuwahamisha mahali pao pa kazi. Leo, utovu wa nidhamu katika kuzingatia bajeti na matumizi, ufisadi, uvivu kazini, n.k; vimeshamiri kwa sababu ya serikali inayoogopa kuwafukuza watumishi wa serikali, iliyotokana na Chama chenye "sera" ya kulindana.